Mkurugenzi
wa Msama Promotions,Bwa Alex Msama akishiriki kushusha vifurushi vya
mchele,ambavyo baadae alivitoe kwa vituo vya watoto waishia katika
mazingira Magumu,makabidhiano ya msaada huo yalifanyika kwenye ofisi
zake Kinondoni jijini Dar.
Mkurugenzi
wa Msama Promotions,Bwa.Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula kwa
ajili ya sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya kwa mlezi wa kituo cha
kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Mwandaliwa-Boko
jijini Dar,Bi.Halima Mpeta.
Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa baadhi ya vituo vya watoto waishio katika mazingira magumu,vilivyopo jijini Dar Es Salaam.
Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa baadhi ya vituo vya watoto waishio katika mazingira magumu,vilivyopo jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza
na Wanahabari wakati wa makabidhiano ya msaada huo,Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama alisema kuwa kama ilivyo ada ya
kampuni yake,kila ifikapo mwishoni mwa mwaka hutoa sadaka kwa vituo
mbalimbali vya watoto waishio katika mazingira Magumu.
"Nimeamua
kufanya hivi pia kuwakumbuka wototo wetu wanaoishi katika mazingira
magumu,na wao washerehekee sikukuu kwa furaha kama wenzao,kwa hiyo
nimetoa unga,mchele,mafuta,viywaji mbalimbali na vingine ili watoto hao
nao kwa pamoja wafurahie msimu wa siku kuu",alisema Msama.
Nae mlezi
wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha
Mwandaliwa-Boko jijini Dar,Bi.Halima Mpeta ameishukuru Kampuni ya Msama
Promotions na Uongozi wake kwa kuwakumbuka katika msimu huu,wamemshukuru
na kumuombea Heri zaidi afanikiwe katika mambo yake ili azidi
kuwakumbuka na kuwasaidia wasiojiweza katika maeneo mbalimbali.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion Alex Msama akimkabidhi msaada wa vyakula mmoja wa
Viongozi wa kituo hicho cha watoto waishia katika mazingira Magumu cha
Maunga,Kinondoni jijini Dar Es Salaamu.
Mwakilishi
wa kituo cha TOVICHIDO,Bi Honoratha Michael akipokea msaada wa vyakula
kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama ,hafla
hiyo fupi ilifanyika ofisini kwake Kinondoni Jiini Dar
No comments:
Post a Comment