Na Genofeva Matemu, WHUSM, Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka Bodi ya Filamu pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa kuendelea kusimamia kazi za sanaa na filamu ili ziweze kukidhi soko la ndani na la kimataifa.
Waziri Mwakyembe amesema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu.
“Bodi ya Filamu na BASATA wamekua wakifanya kazi nzuri ya kukinua vipaji katika tasnia ya filamu na muziki nchini. Ni wajibu wenu sasa kuendelea kusimamia tasnia hizo ili ziweze kukidhi matakwa ya nchi yetu pamoja na kuitangaza nchi kimataifa” amesema Mhe. Mwakyembe
Kwa upande wake Mhe. Grace Tendega amezitaka taasisi hizo kuweka mikakati thabiti ya kusimamia tasnia ya filamu na muziki hatua itakayowasaidia wanatasnia hizo kuboresha maudhui ya maadili katika kazi filamu na muziki.
Naye Mhe. Kasuku Bilago ameitaka Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya filamu nchini kwani sekta hiyo inayofasi kuhimu katika kuinua uchumi wa nchi kwa kasi zaidi kama ilivyo katika nchi za wenzetu
Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Selukamba amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuwa na ushirikiano na Serikali katika kubadili mtazamo wa kukuza sekta ya filamu na muziki nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii Mhe. Peter Selukamba (kushoto) akifungua kikao cha wizara na kamati hiyo kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bi. Pamela Palangio
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akiwasilisha taarifa ya Bodi ya Filamu wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
Mhe. Grace Tendega (kulia) akichangia mada wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Mhe. Sikudhani Chikambo
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akiwasilisha taarifa ya Basata wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Willium (kushoto) wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo na Huduma na Jamii kujadili maendeleo ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na maendeleo ya Bodi ya Filamu leo Mjini Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
No comments:
Post a Comment