Monday, October 2, 2017

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA: PSPF YAFUNGUA OFISI MPYA PEMBA NA UKEREWE




NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezindua ofisi mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

“Mtakumbuka kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, huadhimishwa wiki ya huduma kwa wateja duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili kuboresha zaidi huduma zetu.”

Akizungumzia mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”Bi. Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,hapa makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma kutoka taasisi hizo washirika.

Aliwataja washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu, (MCB).

Alisema, PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.Miongoni mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na maafisa wa PSPF.

“Kwa kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa uchapakazi wa namna hii.” Alisema.
Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa na Bi.Elizabeth Shayo, (kulia), makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Elizabeth Shayo, (katikati), Afisa Huduma kwa wateja wa PSPF, akitoa maelezo kwa Mwanachama aliyefika kupatiwa huduma.
Afisa wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. January Iman Buretta, (kushoto), akizungumza na wanachama wa Mfuko huo waliofika makao makuu kupatiwa huduma Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza jana, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Ntimi Mwakajila, Afisa wa Huduma kwa njia ya simu, (Call Centre), Mfuko wa PSPF, akiwa kazini
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Fatma
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, (mbele), Meneja Masoko, Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Fatma Elhady, (wapili kulia), na maafisa wa kitengo cha huduma kwa njia ya simu wakiwahudumia wateja wa Mfuko kwenye kituo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, akizungumza na mmoja wa wateja waliofika kupatiwa huduma
Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kulia), akipokea nyaraka kutoka kwa Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi.
Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi, (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laima Maghimbi.

No comments: