RC Rukwa Mh. Zelote Stephen
akiwaonesha waheshimiwa madiwani (hawapo pichani)risiti ambazo tayari
zimeshakatwa kabla ya kutumiwa.
RC Rukwa akiwaonesha waheshimiwa
madiwani (hawapo pichani) kitabu cha hoja za mthibiti na mkaguzi wa
serikali kwa Manispaa ya Sumbawanga.
RC Rukwa akitoa ufafanuzi.
…………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna
Mstaafu Zelote Stephen amezionya halmashauri zote mkoani Rukwa
kuhakikisha wanazitumia vizuri manshine za EFD kwa kuongeza mapato
katika halmashauri zao.
Ametoa onyo hilo kwenye kikao
maalum cha kujibu hoja za ukaguzi wa hesabu za serikali kwa madiwani wa
Manispaa ya Sumbawanga katika kumalizia ziara yake maalum kwa
halmashauri zote mkoani humo kujua namna Halmashauri zilivyojipanga ili
hoja hizo zisijirudie miaka inayofuata.
Akiongea huku akionesha risiti
alizozikamata katika maeneo mbalimbali ya mauzo alisema kuwa serikali
inafanya kila liwezalo katika kuhakikisha inakusanya maopato lakini bado
kuna watumishi wanatafuta namna ya kuiskosesha serikali mapato hayo.
“katika kila sehemu za mauzo
lazima mashine hizi ziwepo na kuwepo sio mtindo huu (akionesha msururu
wa risiti zilizokatwa tayari kwa matumizi) hizi nimezikamata maeneo
anajua Mkurugenzi, asubuhi watu wanagawana, ndio mchezo uliopo, pamoja
na jitihada tunazofanya bado watu wanatafuta mbinu za kuiba, hii sio
kwamba nimeleta iwe mfano, hapana, nimezikamata na mfahamu kuwa mimi ni
mtaalamu wa kukamata,”Alisema
Katika Kusisitiza suala la uwazi
wa matumizi ya fedha za halmashauri kwa waheshimiwa madiwani Mh. Zelote
alitaja majukumu kadhaa ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kusema kuwa moja
ya kazi za Mkurugenzi ni kuhakikisha kuwa madiwani wanapata taarifa za
fedha za halmashauri.
“Hapa mmezungumza na mmenionyesha
kwa kiasi kikubwa kwamba hamnazo taarifa na nikiangalia kazi moja wapo
ya waheshimkwa madiwani ni kiusimamia matumizi ya fedha za halmashauri
zao sasa mtasimamiaje ikiwa hamna taarifa,” Alisema.
Na kukumbusha kuwa Mkurugenzi ndio
katibu wa kamati ya fedha ya halmashauri lakini na kuonya kuwa kamati
hiyo ibebe sura ya halmashauri na sio sura ya kamati na kuwasisitiza
kufuata taratibu nyingine za ikiwa kurudisha mrejesho kwa wengine juu ya
mipango na maazimio yaliyofikiwa.
Katika kikao hicho Mh. Zelote
alimtambulisha mtaalamu wa TEHAMA ili awaelezee waheshimiwa madiwani
namna mifumo ya fedha inavyofanya kazi ili nao wawe na uelewa mpana
katika kufuatilia mapato na matumizi ya halmashauri.
“Suala la kukusanya mapato
limekuwa likiimbwa asubuhi, mchana na usiku, kuwa tuhakikishe
tunajipanga vyema kukusanya mapato ya halmashauri kwa kupitia utaratibu
uliopo, suala la kutumia hizi mashine sio la kuhoji tena mwisho ulikuwa
mwezi wa tatu ndio agizo lililopo kwa wakurugenzi kuwa mashine hizi
ziwepo na zinafanya kazi,” Alisema.
Na katika kuhakikisha kuwa vitabu
hivyo havipati nafasi Mh. Zelote alitoa siku saba vitabu hivyo
kurudishwa maghalani na kuongeza kuwa watumishi wanaokiuka miiko ya kazi
zao kuwajibishwa kulingana na madhara waliyosababisha na kuwaasa
kujenga uaminifu katika utumishi ndani ya halmashauri.
“Sitaki kusikia tena kuwa kwenye
mkoa wangu kuna halmashauri inanyooshewa kidole, mmeshanyooshewa kidole
mara moja sitaki kuona tena hicho kidole,” alimalizia.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa
Wilaya ya nSumbawanga Mh. Julieth Binyura alishanngazwa na wataalamu hao
kushindwa kudhiti hoja na hatimae wao kuwa chanzo kikuu cha kuzalisha
hoja.
“Mtu kama unaitwa mtaalamu na
serikali imekuamini kwanini tena unaizalishia serikali hoja, na suala la
fedha ni suala nyeti sana hivyo linahitaji umakini wa haloi ya juu ili
kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili na si vinguinevyo,”
Alisema.
Akifunga kikao hicho Mstahiki meya
wa Manispaa ya Sumbwanga Mh. Justin Malisawa alimuahidi Mkuu wa Mkoa
kusimamia yale yote aliyoyaelekeza na kuomba msaada wake pindi pale
watakapokwama.
No comments:
Post a Comment