Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited,
Dk. Ben Moshi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni
gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika
mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni
hiyo, Philippe Corsalettti,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika,Naibu
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo pamoja na
viongozi waanndamizi kutoka Wizara hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited Dkt.Ben Moshi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti mfano
wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali
yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma.
Anayeshuhudia katikati ni ,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika
Dk. Mpango akifafanua jambo kwa kusisitiza Taasisi mbalimbali za Serikali kuboresha huduma zao na kuipatia serikali gawio kubwa.
Dk Mapango akipongezana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti pamoja na Mwenyekiti wa Puma, Dkt. Moshi
Mwenyekiti
wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben
Moshi (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Philip Mpango (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Puma, Philippe Corsalettti wakati wa hafla ya kampuni hiyo kukabidhi
gawio la sh. bilioni 7 kwa serikali mjini Dodoma,pichani kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo na kulia
ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Mpango (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Puma, pamoja na manaibu makatibu wakuu.. Kutoka
kulia ni Katibu wa Bodi ya Puma, Gibson Mgima, Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha, Dorothy Mwanyika, CEO wa Puma, Corsaletti, Mwenyekiti wa Puma,
Dk. Moshi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, D.
Juliana Palangyo.
SERIKALI
imekubali kulifanyia kazi ombi la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy la
kutaka taasisi za umma ziweze kununua mafuta ya kampuni hiyo yenye ubia
wa asilimia 50 kwa 50 na Serikali ili faida inayopatikana itumike kwenye
kutatua changamoto za Watanzania.
Kauli
hiyo imetolewa Mjini Dodoma mapema leo baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya
Kampuni ya Puma Dk Ben Moshi kutoa ombi hilo kwa Waziri wa Fedha na
Mipango Dk Philip Mpango wakati wa tukio la kampuni hiyo kutoa gawio la
Sh bilioni 7 kwa Serikali ambayo ni faida iliyopatikana kutokana na
biashara ya mafuta.
Akikubali
ombi hilo Dk.Mpango alisema kuwa watalifanyia kazi ombi hilo hasa kwa
kutambua hata mchango wa kampuni ambazo zimewekeza nchini na zina ubia
na Serikali, huku akitoa angalizo kuwa pamoja na ombi hilo
kufanyiwa
kazi,hakuna sababu ya Puma kubweteka kwani lazima ushindani uwepo ili
kupatikana kwa bidhaa bora."Serikali tumefurahi kwa gawio hili ambalo
mmelitoa kwani fedha hizi zitakwenda kuhudumia Watanzania masikiniambao
wanahitaji kupata huduma muhimu.Hivyo niwahakikishie Puma ombi lenu
nimelisikia na tunalifanyia kazi lazima tuendelee kushirikiana ili kuwa
na uwekezaji wenye tija kwa nchi yetu,"alisema Dk.Mpango.
Pia
alitumia nafasi hiyo kuitaka kampuni ya Puma kuendelea kufanya kazi yao
kwa ufanisi zaidi ili mwaka ujao wa fedha, gawio liongezeke zaidi na
kuwahakikisha Serikali inalo jicho lake ambalo linaangalia kwa kampuni
zote na mashirika ambayo wana ubia nayo.
Awali
kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh bilioni 7 kwa Waziri wa Fedha
na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi yaPuma Dk. Mosha alisema kuwa wanatambua
majukumu yao kwenye kufanyabiashara ya mafuta na ndio kampuniambayo
inaongoza kwenye soko lakini ombi lao kwa Serikali ni kwamba itoe
maelekezo kwa taasisi na mashirika yaumma kununua mafuta kutoka kwao.
Alisema
wanaamini ombi hilo likifanikiwa wataongeza mapato na faida kwa kampuni
hiyo ambayo kwa sehemu kubwani kama ya Serikali na hivyo gawio
litaongezeka zaidi ya lilitolewa jana huku akisisitiza jukumu lililopo
mbele yao nikuhakikisha wanaendelea kuwa bora katika utoaji wa huduma ya
mafuta nchini.
"Kampuni
yetu ina ubia na Serikali, hivyo tunaomba kama Waziri utaona inafaa
mtoe maelekezo maalumu ili kuzifanya taasisi za umma kununua mafuta
kwetu.Hii itatuwezesha kupata fedha nyingi na hivyo kuongeza gawio kwa
Serikali
.Tunatamani
kuona tukija tena mwakani tunatoa fedha nyingi zaidi ya hizi Sh bilioni
7,"alisisitiza.Wakati huo huo, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania
Limited Philippe Corsaletti, alisema kuwa uongozi wa
kampuni
hiyo unapongeza juhudi za Rais John Magufuli ya kuhakikisha Serikali
inatekeleza mikakati yake ya kukusanyakodi na kutoa fursa kwa wawekezaji
wa nje na ndani.
Pia
alisema kuwa ufanisi wa kibiashara wa kampuni hiyo kwa mwaka 2016
ulikua mzuri kwa pande zote za mauzopamoja na mapato. "Ufanisi wetu
mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa
sisi ndiotunaongoza katika soko."
Alisisitiza
wakati wakitoa gawio hilo la Sh bilioni 7 kwa Serikali, jambo kubwa
ambalo linawapa faraja ni juhudi zaSerikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais ,Dk.John Magufuli ambaye pamoja na mambo mengine ya
kuletamaendeleo ameimarisha mfumo wa kukusanya kodi na kutoa fursa kwa
wawekezaji wa nje na ndani kamailivyooneshwa kwenye bajeti ya
2017/2018.
"Puma
imekuwa ikifuatilia kwa karibu utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya
tano, na kuridhishwa na utendaji wake,hivyo uongozi wa Puma Energy
utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku
zote.
"Pia
tunafurahishwa na hatua ambazo Rais wetu anachukua katika kuhakikisha
rasilimali zilizopo nchini zinawanufaisha Watanzania wote, hivyo Puma
tutaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano,"alisema.
Akifafanua
zaidi kuhusu gawio ambalo wamelitoa kwa Serikali Meneja huyo wa Puma
alisema kufikia mwisho wamwaka ulioishia Desemba 31 mwaka 2016 kampuni
hiyo ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla yaSh bilioni 35.5 na
kufafanua Puma Energy iliwekeza kwa nguvu katika kipindi cha mwaka 2016
ili kuboresha miundombinu yake ya ndani na rasilimali zake.
"Lengo
letu lilikuwa ni kuimarisha uwepo wake sehemu mbalimbali na kukuza
biashara yake. Hivyo kutokana na mazingira mazuri ya biashara bodi ya
wakurugenzi imependekeza gawio la Sh.bilioni kwa mwaka ulioishia 2016
iwezekulipwa kwa Serikali kutokana na utendaji mzuri wa kampuni.Mwaka
2015 gawio lilikua Sh bilioni 4.5 bilioni na hivyo
hiyo inawakilisha ongezeko la asilimia 56 ukilinganisha na mwaka jana na hii ni sambamba kabisa na mkakati wakampuni,"aliongeza.
Alitumia
nafasi hiyo kuelezea majukumu ya kampuni hiyo ni masoko na usambazaji
wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania na kufafanua wanao uwezo wa
kuhifadhi lita za mafuta milioni 94, vituo 47 vya mafuta maeneo
mbalimbalinchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.
No comments:
Post a Comment