Saturday, June 3, 2017

WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha kujiandaa kustaafu kwa amani.
Katika semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha BoT Capri-point  jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha nao wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
Wadau hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Mwalimu Commercial Bank, (MCB),Bw. Valence Luteganya, akizungumzia huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo. "Beni hii imeanzishwa hivi karibuni na wamiliki wa benki hii kwa karibu asilimia 30 ni walimu. na huduma tunazozitoa ni pamoja na utoaji mikopo nafuu, ushauri wa kifedha lakini pia katika jiyihada za kurahisisha huduma za kibenki, MCB imo kwenye mtandao wa Umoja Switch ambao umetapakaa nchi nzima." hayo ni baadhi ya maneno ya Bw. Lutenganya
 Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCB

Mkuu wa kitengo cha  wateja binafsi benki ya NMB, Bw.Omary Mtiga, akitoa somo kuhusu fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao watarajiwa wanaweza kuzipata. "Benki ya NMB ina matawi kote nchini na hivyo inaweza kukufikishia huduma hapo ulipo pasina shaka, kwenu nyinyi ambao wengi wenu ni wateja wetu, mnayo fursa ya kufungua Bonas account ambayo inakuwezesha kufikia malengo mbalimbali uliyojiwekea na inaweza kutunza amana zako kwa usalama na kufikia malengo yako ya baadaye uliyojiwekea, lakini kubwa zaidi hakuna gharama za kuendesha akaunti hii." alisema
 Mkurugenzi wa idara ya mikopo benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bw. Henry Bwogi, akizoa mada kwa washiriki ambapo alisema, "TPB ndiyo benki kongwe kuliko zote hapa nchini ikiwa na matawi yaliyosambaa kila kona ya nchi na hivyo kuwa rahisi kwa wateja kufikiwa na huduma zake, lakini pia benki hiyo tayari imeonyesha nia ya dhati ya kuwajali wastaaafu ambapo imekwisha toa mikopo ya mabilioni ya shilingi kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
 Bi Doris Mlenge, Afisa Masoko wa Mfuko wa UTT-AMIS, akiwapatia vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo. "Kwa mtu yeyote anayetegemea kupata kipato kwa mkupuo kutokana na pensheni au chanzo kingine cha fedha anatakiwa kuwekeza kwenye Mfuko huo ili aweze kupata kipato cha mara kwa mara na akasema kuwekeza kwenye mifuko ya kujikimu kama UTT-AMIS kunatoa faida kubwa ukilinganisha na uwekezaji wa namna hiyo kwenye masoko ya fedha.
 Bw. Denis Mwoleka, ambaye ni Meneja wa CRDB tawi la Chuo Kikuu cha SAUT jijini Mwanza, akizungumza kuhusu umuhimu wa wastaafu hao watarajiwa kujiunga nabenki hiyo kwa kutarajia kupata faida mbalimbali ikiwemo huduma mpya ya akaunti ya akiba ya dhahabu ambayo ni njia rahisi ya kujiwekea akiba ili kufanikisha malengo ya baadaye.
 Afisa kutoka Shirika la viwanda vidogo vidogo SIDO, akihamasisha wastaafu watarajiwa kuwekeza kwenye uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawawezesha kujikimu kimaisha na ksutaafu kwa amani. yeye alsiema SIDO iki tayari kutoa ushauri na mafunzo ya uanzishaji wa viwanda hivyo

 Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim,(kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wapili kushoto) na Meneja Mipango na Utafiti wa Mfuko huo, Bw.Luseshele Njeje
 Meneja wa Fedha wa PSPF, Bw.Lihami Masoli. (kulia), na Mtafiti Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw.Mapesi Maagi, (katikati), wakibadilishana mawazo na Katibu Msaidizi wa TSC wilaya ya Kwimba, Bw. Fundikira R.K. James, wakati wa mapumziko ya semina hiyo
 Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim, (kushoto), akifafanua mambo kadhaa kuhusu pensheni
Bw. Silayo (kushoto), akiteta jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi

No comments: