Dar
es Salaam; 26 Julai, 2016, Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia
promosheni yake ya Tusker Fanya Kweli Uwini iliyomalizika wiki iliyopita
imeendelea kuwakabidhi washindi wa promosheni hiyo vitita vyao kutoka
mikoa mbali mbali nchini. Mwishoni mwa wiki baadhi ya washindi hao
walikabidhiwa pesa zao katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika
jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa washindi wakishindwa kuficha
hisia zao juu ya swala hilo.
Hafla
hiyo iliyopambwa na burudani mbalimbali ya muziki ilihudhuriwa na wadau
mbalimbali wakiwemo baadhi ya washindi wa promosheni ya Tusker Fanya
Kweli Uwini, wapenzi na watumiaji wa bia ya Tusker pamoja na viongozi
mbalimbali wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.
“Leo
mbele yenu tumewakabidhi washindi wetu pesa zao za ushindi Milioni moja
kila mmoja walizoshinda katika droo tulizochezesha tunaimani watatumia
katika masuala ya kimaendeleo. Kuwapongeza sana washindi wetu wote na
kwa nanma ya pekee hawa tuliowakabidhi pesa zao joini ya leo pia
nawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono siku zote kwani wao ndio
waliotuwezesha sisi kufika hapa leo.” Alisema Meneja wa Bia ya Tusker
Jasper Migambile.
Naye
mmoja wa washindi waliokabidhiwa Milioni moja Juliana Petro Mwasigara
aliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Tusker kwa
kumpatia pesa hizo na kueleza namna atakavyoitumia. “Nashukuru sana pesa
hii itanisaidia mimi na familia yangu kwani nina watoto wananitegemea
na sina mume, hivyo kwangu hii ni kama miujiza bado”, alisisitiza
Juliana.
“Mimi
nafanya biashara ya karanga lakini kwa pesa hii niliyopokea leo
ntabadilisha biashara mana nimepata mtaji wa kutosha nafikiria kununua
pikipiki niingie barabarani, bado siamini naangalia simu yangu kila
wakati kuhakikisha ujumbe mfupi nilioupata wa kupokea Tsh 1,000,000.”
Alieleza mshindi wa pili Ally Mkemi.
Washindi
waliokabidhiwa pesa zao katika hafla hiyo ni Juliana Petro Mwasigara,
Inai Ngwavi na Ally Mkemi wote kutoka Dar es Salaam. Bado washindi
mbalimbali wa promosheni hiyo wanaendelea kupokea vitita vyao huku ikiwa
tayari droo zote zimeshakamilika wiki iliyopita.
‘Tusker
Fanya Kweli Uwini’ ni promosheni iliyoanza takribani wiki tisa
zilizopita mikoa yote nchini na leo imekamilisha washindi 100 na
kufungwa rasmi kwa droo za promosheni hiyo.
Meneja
Mauzo wa Eneo Erick Pallangyo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya
Tsh Milioni moja mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli
Uwini Juliana Petro Mwasigara (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano
iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Meneja Mauzo wa eneo Erick Pallangyo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Tsh Milioni moja mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini Inai Ngwavi (kulia)
Mmoja ya wageni waalikwa Juma Ramadhani (katikati) akisoma ujumbe mfupi wa maandishi unaoonesha pesa iliyoingia kwa Ally Mkemi (kulia) mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini, kushoto ni Meneja Mauzo wa eneo(Area Sales Manager) Erick Pallangyo (kushoto).
Mmoja wa washindi wa Tusker Fanya Kweli Uwini Ally Mkemi(kulia) akionesha msg ya pesa aliyoshinda, pembeni yake ni Meneja Mauzo wa Eneo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Kikundi cha burudani cha amsha amsha kikitoa burudani wakati wa hafla ya makibidhiano kwa baadhi ya washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment