Tuesday, July 26, 2016

TANAPA YAIONGEZEA NGUVU TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA MASHINDANO YA OLIMIPIKI.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho kwa wanahabari na wageni wengine katika hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa, inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki yatakayoafanyika mwezi Agosti  nchini Brazil.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi,akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi Milioni tano kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki.
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki. 
Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi "Track Suit "maalumu zenye maandishi na nembo yanayotangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda timu ya taifa wanaojiandaa na mashindano ya Olimpiki
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi pamoja na mavazi maalumu kwa ajili ya wanariadha hao .
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) waliohudhuria hafla hiyo.kutoka kushoto Mkurugenzi wa Utalii na Masoko,Ibtahim Musa,Meneja Utalii Johnson Manase na Mhifadhi Vitalis Uruka.
Wanariadha watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Olimpiki katika jiji la Reo De Jeneiro nchini Brazil wakiwa katika mavazi maalumu yanaotangaza vivutio vilivyoko nchini.
Mkufunzi wa Wanariadha wanaojiandaa na mashindano ya Olyimpiki ,Francis John akizungumzia matarajio yake juu ya vijana hao.
Mmoja wa Wanariadha hao,Alphonce Felix Simbu akizungumza mara baada ya kupoke msaada kutoka  TANAPA.
Baadhi ya Wanahabari na wageni wengine waliofika katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kushuhudia makabidhiano hayo.
Mwanariadha Said Makuka atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Sara Ramadhan ,mwanadada pekee atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Alphonce Felix atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Fabian Joseph atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Wanariadha wanne watakao iwakilisha Tanzania katika Michuano ya Olyimpiki nchini Brazil wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Antony Mtaka ,wengine kutoka kulia ni Mkufunzi wa wanariadha hao,Francis John na anyefuatia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masokowa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza  kutumia fursa ya mashindano ya Olyimpiki yanayotarajia kuanza mwezi ujao katika jiji la Rio de Janeiro nchini Brazili kutangaza vivutio vya utalii kupitia wanariadha wa Tanzania.

Hadi sasa ni wanariadha wanne ,wakiume watatu na wa kike mmoja ndio waliofuzu kushiriki mashindano hayo na tayari wako kambini katika hosteli za Chuo cha Misitu cha FITI zilizoko West Kilimanjaro wilayani Siha.

Akiongea mjini Arusha wakati akikabidhi msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya wanariadha hao Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi amesema wameamua kutumia fursa hiyo pia kusaidia wanariadha hao wanaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo ili waweze kurejea na medali.

Akishukuru kwa msaada huo Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu AnthonY Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwakatia bima ya Afya mwaka mmoja wanariadha hao pamoja na familia zao ili wanapokua nchini Brazili wasiwe na mawazo mengi kuhusiana na familia zao walizoziacha hapa nchini.

Naye mmoja wa wanariadha waliofuzu kushiriki mashindano hayo Alphonce Felix pamoja na mkufunzi wa timu hiyo ya Riadha Francis John wameushukuru uongozi wa Riadha kwa kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini kwa miezi saba na kuahidi safari hii timu hiyo haiendi kushiriki bali kupambania medali.

Wanariadha waliopo katika timu hiyo ya taifa wanaotarajiwa kwenda Brazili ni mwanamke pekee Sara Ramadhani, Fabiani Joseph, Saidi Makuka na Alfonce Felix.

No comments: