Tuesday, May 3, 2016

MBUNGE ABDALLAH ULEGA ADHAMIRIA KULIKOMBOA JIMBO LA MKURANGA KIMAENDELEO

Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai katika Mpango pili wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake la Mkuranga mkoani Pwani.

SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria kuwa Serikali ya mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.Rais Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda.

Wakati Serikali ikisisitiza kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono hilo kila mmoja amekuwa na kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo hilo.

Abdallah Ulega ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwa upande wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha dhamira na kiu ya kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo kuwa na viwanda.

Anasema kuwa lazima wao kama wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi haya kwani wameahidi hivyo lazima watende. Ulega anasema kuwa Jimbo la Mkuranga ni kubwa na linarutuba ya kutosha hivyo anakaribisha wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda vidogovidogo na vikubwa katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali Kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.

Anasema kuwa kuna jitihada kama Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba jimbo lake ni miongoni mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya Serikali ya kutaka mageuzi ya viwanda. “Kimsingi jimbo langu la Mkuranga ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo maana naomba wahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda.”anasema ulega

Anasema kuwa kutokana na utajili wa Ardhi yenye rutuba wanaweza kujenga viwanda vya kusindika mazao lakini pia kwa sababu eneo lao ni kubwa basi hata viwanda vya kubangua korosho na kujengwa Kwa viwanda hivyo kutasaidia kuleta ajira katika eneo hilo.

Anasisitiza kuwa ndio maana wakati akichangia mpango wa wa maendeleo wa Serikali Kwa miaka mitano ameomba Serikali na wahisani kujitokeza Mkuranga lakini Kwa upande wa Serikali kuiweka Mkuranga kuwa sehemu yenye hitaji la ujenzi wa viwanda. Anasema amebainisha wazi kiu ya wananchi wa jimbo lake la kutaka maendeleo na ajira hivyo bila kuwepo na viwanda hakuna ajira inayoweza kuwepo na zaidi vijana watazidi kulaumu serikali yao.

“Nimesema wazi kuwa Mkuranga kuna matatizo ya miundombinu mbalimbali ikiwamo barabara.Maji .kilimo na mambo mengine na katika baadhi ya maeneo haya nashukuru baadhi ya marafiki wameitikia mwito wangu na wameweza kusaidia katika kichimba visima ambapo wananchi wangu wameaza kupata Maji safi na salama.”anasema Ulega

Anasema kuwa anawashukuru African Foundation Reflection Kwa kuonesha moyo wa kusaidia na juhudi hizo zote zimetokana na jitihada zake za kutaka kuona siku moja Mkuranga inakuwa ya kutolea mfano tofauti na ilivyo sasa. Aidha katika mpango huo wa maendeleo Kwa miaka mitano Kwa Serikali ameomba kujengewa barabara Kutoka Kisiju hadi Mkuranga Kwa kiwango cha lami kwani barabara hiyo ni muhimu Kwa wananchi wa wilaya hiyo lakini hata wale wanaotoka Mafia.

Pia anasema katika mpango mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano Kuhusu maendeleo ya miundombinu nchini na hapo aliangalia wilaya ya Mafia kwa sababu pale kuna bandari na watu wake pia ndiyo wazalishaji wakubwa wa korosho na samaki. Anasema kuwa pia kwenye kata yake ya mbezi kwaniaba ya wananchi wake wa Mkuranga wangeishauri Serikali kuwa eneo la viwanda ili wananchi wake wawe sehemu ya uzalishaji wake.

Aidha Ulega anazungumzia suala la kuondoa kero ya uhaba wa upatikani wa Maji katika jimbo hilo ambapo Serikali ingefanya bidii ya kutoa maji hayo kutoka katika mto rufiji kupitia kibiti hadi kufika Mkuranga na hatimaye Dar es Salaam.Anasema haiwezekani Kwa miaka nenda rudi tatizo la Maji halipatiwi ufumbuzi wakati Mkuranga inapitiwa kwa karibu na Mto Rufiji ambapo mikakati madhubuti ya kuleta Maji ikifanyika tatizo hilo litabaki kuwa historia katika eneo hilo.

Anasema tatizo la ajira Kwa vijana ni kubwa mno hivyo wanashukuru Serikali Kwa kutambua umuhimu wa kutilia mkazo uazishwaji na ufufuaji wa viwanda kwani eneo hilo ndilo linaweza kuwa.msaada Kwa vijana kuweza kupata ajira. “Mimi kama Mbunge wao kama nilivyosema awali nitaendelea kupambana na kufanya kila linalowezekana Kwa kuhakikisha Mkuranga inakuwa sehemu ya viwanda na naendelea kitoa rai Kwa wawekezaji kuchangamkia Ardhi yetu Kwa kujenga viwanda vingi ili vijana wangu wapate ajira.”anasema

Anaongeza kuwa mkuranga ilisahaulika mno pamoja kwamba ni miongoni mwa wilaya za siku nyingi lakini imekuwa nyuma kimaendeleo hivyo niwakati mwafaka wa kushirikiana Kwa pamoja Kwa ajili ya maendeleo. Anasema kuwa wananchi wake waendelee kumuombea Kwa Mungu na wazidi kudumisha Umoja na mshikamano ili Kwa pamoja wapambane Kwa lengo la kuona jimbo la mkuranga linakuwa la mfano.

Akizungumzia kilimo cha korosho anasema kuwa pamoja na zao hilo kuwa ndio zao linalotegemewa kuendesha maisha ya wananchi wake lakini bado kwasababu ya ukosefu wa kuwepo Kwa viwanda hususani vya ubanguaji kunafanya pasiwepo na tija sana wanayoipata wananchi wake katika kilimo hicho.Anasema kuwa kutokana na hali hiyo ana kazi kubwa ya kuendelea kuzungumza na watu mbalimbali ili kuleta ushawishi wa kukubali Kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda hivyo.

Pia akizungumzia Elimu anasema anatambua changamoto zilizopo katika eneo hilo hivyo amedhamiria Kwa dhati Kwa kushirikiana na Halmashauri wanaongeza hamasa Kwa wanafunzi ili waweze kufanya vema katika masomo yao na hatimaye kuweza kupata wataalamu wa baadae.

“Najua kuna Changamoto ya madawati na hili tunalishugulikia Kwa kushirikiana na kamati mbalimbali za Shule,wazazi,pamoja na walimu ili kuona namna ya kukabiliana na tatizo hilo na hata uchakavu wa majengo .”anasema Ulega. Anahitimisha Kwa kuwataka wananchi wa Mkuranga kila mmoja kujielekeza katika kuzalisha Mali huku wakienda na Kauli mbiu ya Rais Dkt.Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

No comments: