Saturday, April 30, 2016

MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA USAFI JIJI LA DAR LEO


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda (wa pili kushoto),akiwa sambamba na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa za Wilaya ya Kinondoni,Ilala pamoja na Temeke wakishiriki kwa pamoja kufagia ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Mh Paul Makonda kuzindua kampeni ya Usafi wa jiji la Dar Es Salaam,uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika mapema leo asubuhi Katika viwanja vya .Lidaz Club,Kinondoni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali serikali,dini na makundi mengine yakiwemo makundi ya michezo na waendesha boda boda.Mkuu wa Mkoa alizindua kampeni hiyo ya Usafi kwa kuwakabidhi Wenyeviti hao kila mmoja ufagio wa ajili ya kwenda kuwahamasisha wananchi wao katika mitaa yao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda akiwahutubia Wananchi mbalimbali mapema leo asubuhi katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar mara baada ya kumaliza kufanya usafi na hatimae kukusanyika kwenye viwanja hivyo,ambapo Mh.Paul Makonda alizindua kampeni ya Usafi kwa jiji la Dar.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke ndugu Bakari Makere,kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa Paul Makonda katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ya Usafi kwa jiji hilo.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Juma Mgendwa
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliokuwa yakijiri uwanjani hapo


Wananchi wakishangilia jambo


Wananchi weakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo

Yamoto Band wakitumbuiza jukwaani.
Wasanii wa muziki wa kizazi wa kundi la Yamoto Band wakitumbuiza jukwaani na wimbo wao wa kuwahamasisha wananchi suala la usafi katika jiji la Dar na kwingineko

Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Leaders Club,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo mara baada ya kumaliza kufanya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiongoza maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika matembezi maalum ya kampeni ya kuhamashisha usafi katika jiji hili #Dar es salaam Ya Makonda, Usijifanye Mstaarabu kuwa Mstaarabu. Matembezi hayo yalimeanzia katika Uwanja wa Karume, Ilala na kuishia katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa na Naseeb Abdul "Diamond  Platnumz " Simba  , Babu Tale,Ruge Mutahaba wa  Clouds Fm  na wengine wengi wakishiriki Kampeni ya  Usafi Leo  Dar ya Makonda

Sehemu ya wananchi wa Jiji la Dar es salaam wakishiriki Matembezi ya maalum ya kampeni ya kuhamashisha usafi, kuunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda aliyeongoza matembezi hayo. #Dar es salaam Ya Makonda, Usijifanye Mstaarabu kuwa Mstaarabu.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza siku ya Jumamosi ya wiki ni siku ya usafi kuanzia saa moja hadi saa tatu na ndipo shughuli zikingine zitaanza ikiwa ni lengo la kufanya jiji la Dar es Salaam kuwa kitovu cha usafi na wengine waanze kuiga mfano huo.

Makonda ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi wa jiji la Dar es Salaam uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa pamoja na wasanii waliojitolea kuhamasisha wananchi kufanya usafi kwa kutumia muziki, Makonda amesema kuwa haiwezekani kila siku watu wawe wanasifia nchi ya Rwanda kufanya usafi, sasa kazi hiyo itafanywa jijini Dar es Salaam na wenyewe wajifunze kwetu katika kupata mabadiliko ya usafi kwa muda mfupi.

Mkuu wa Mkoa amesema vyombo vya usafiri hususani Daladala zitaanza kufanya kazi saa tatu na biashara zote zitafunguliwa muda huo ili kuwapa watu wote kutumia muda wa asubuhi kufanya usafi katika maeneo yao.

Makonda ameagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dar es Salaam kufanya ukaguzi wa Daladala zote kuhakikisha vyombo hivyo vinakuwa na vifaa vya kuhifadhia taka (Dust Been) na wasiofanya hivyo hatua za kisheria kuchukuliwa.

Amesema kuwa kila mtu katika jiji la Dar es Salaam kufanya usafi bila kusimamiwa na watu watakaochafua mazingira kwa makusudi au kwa ustaarabu watachukuliwa hatua .Aidha ameagiza watumushi wote katika manispaa tatu kuhakikisha hawajihusishi na kampuni za kufanya usafi kutokana na kudorola kwa usafi wa jiji kwa kipindi kirefu ikiwa ni pamoja na kupitia zabuni zote za usafi na watu ambao watakuwa hawana vigezo vya kufanya usafi waondolewe.

Katika uzinduzi huo Makonda amezindua mashindano ya usafi kwa wenyeviti wa serikali za mitaa 50,kushindana katika usafi kwa vigezo katika mitaa iliyopangwa pamoja na isiyopangwa na mshindi atapata zawadi ya sh.milioni 50.

No comments: