Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili katika kata ya Hembeti, Kijiji cha Dihinda kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima nawafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.
Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.
Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akishuhudia madhara yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji kitongoji cha Dihinda uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na mama mjane aliyejeruhiwa na mbuzi wake kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima katika kitongoji cha Dihinda.Sehemu ya Mbuzi waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima wilayani Mvomero.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakiangalia madhara yaliyosababishwa na uhusiano mbaya kati ya wakulima na wafugaji eneo la kata ya Hembeti.Waziri wa Kilimo.Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa wakichanja mbuga za kijiji cha kigurukirwa wakati wa kukagua madhara yaliyotokana na uhusiano mbaya kati ya wakulima nawafugaji wilayani mvomero hii leo.
Picha na Sanga Festo Jr.
No comments:
Post a Comment