Mwanachama akipata maelezo kutoka kwa
Afisa Masoko Bi Rehema Mkamba
Banda la Mfuko wa Pesheni wa LAPF
ambalo lipo kwenye jengo la Ofisi ya waziri Mkuu, uwanja wa Nanenane, Dodoma
Wanachama wakipata maelezo kuhusu
bidhaa zinatolewa na LAPF ambazo ni uwezo wa kujichangia katika mfumo wa hiari,
mkopo wa elimu, mkopo wa kujikimu, mkopo wa nyumba na fao la uzazi.
LAPF ni mfuko bora wa pensheni Tanzania pia umeshiriki Maonesho haya ya Nanenane
2015.LAPF ipo banda la ofisi za Waziri Mkuu TAMISEMI
Katika banda hilo, LAPF tunatoa huduma zote za hifadhi ya jamii,kuu
zikiwa ni;
Elimu kwa umma kuhusu hifadhi ya jamii Tanzania yaani tumetoka wapi, tupo
wapi na tunaenda wapi.
Tunaandikisha wanachama wapya wa hiari, wa kisheria na waajiri na kutoa
vitambulisho hapohapo kwenye banda la LAPF
Wanachama wanapata fursa ya kuona michango yao na ya mwajairi na kupata
nakala inayo onyesha michango yao
Tunajibu maswali ya wanachama, kupokea maoni ya wanachama na wananchi
wote kwa ujumla.
LAPF inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao kujifunza kuhusu hifadhi
ya jamii, kujiunga na kujionea huduma bora zilizo pelekea LAPF kuzawadia tuzo ya mfuko bora na
msimamizi na mdhibiti wa sekta ya
hifadhi ya jamii pia kupata tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa miaka mitano kwa
utunzaji bora wa mahesabu ya mfuko
Karibu sana banda la LAPF.
No comments:
Post a Comment