Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuzindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini Kahama. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Felix Maagi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hizi ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya Mji Kahama mkoani Shinyanga. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015.
Waziri Lukuvi akitizama michoro ya mradi wa nyumba 50 utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.1 unaotekelezwa na NHC Wilayani Kahama.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikagua majengo ya nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi (kushoto)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe Lukuvi akiwasili kuweka jiwe la msingi zilizojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Mjini Kahama.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akielekea kwenye ya mfano ili kuikagua na kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini Kahama.
Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50 yaliyojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama.
Meza Kuu- Waziri Lukuvi akitazama kikundi cha ngoma wakati alizindua nyumba za gharama nafuu za NHC Mjini Kahama lengo likiwa la kupendezesha mandhari ya miji yetu, kupandisha hadhi ya maeneo lakini pia kuwapatia wananchi wa kipato cha chini nyumba bora na gharama nafuu
Kundi la sanaa la Makhirikhiri la Kahama wakitoa burudani
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Benson Mpesya akizungumza eneo la Bukondamoyo na kulipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga nyumba za kisasa na imara na kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika halmashauri za wilaya nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,, Bw. Felix Maagi akizungumza eneo la Bukondamoyo ambapo alisema halmashauri zitakazotoa ushirikiano na kuwa tayari kununua nyumba ndizo zitazojengewa nyumba na NHC. Bw. Felix Maagi, alisema pia kuwa mradi huo umetengeza ajira za moja kwa moja 290, ajira shirikishi 145 na makazi ya watu 300.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50 zilizojengwa na NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula Wilayani Kahama. Alizitaka Halmashauri za Wilaya kupima maeneo ya Miji na kuyagawa kwa wananchi kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuweka mipango miji vizuri.
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh. James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili fedha za watu watakaoishi hapo zisitoke nje ya eneo hilo.
Waziri William Vangimembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wealiohudhuria uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Mjini Kahama.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi akiondoka eneo la tukio akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh. James Daudi Lembeli mara baada ya kuzindua nyumba za gharama nafuu eneo la Bukondamoyo.
No comments:
Post a Comment