Kaimu
Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam jana, kwenye semina ya siku moja kuhusu magonjwa
yasiyoambukiza. Kulia ni Meneja Mradi Shirikisho la Vyama vya Magonjwa
Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA
Kaimu
Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kulia), akimuelekeza jambo Ofisa Habari wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura wakati wa semina
hiyo.
Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kushoto), akielekeza jambo kwenye semina hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MAISHA ya watu katika nchi zinazoendelea, yapo hatarini kutokana na asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza kusababisha vifo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa semina ya
magonjwa yasiyoambukiza iliyondaliwa mahususi kwaajili ya wanahabari
yenye lengo la kukamilisha mkakati pamoja na mpango kazi 2015/2020,
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Auson Rwehimbiza aliyataja magonjwa yasiyoambukiza ni moyo na
mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.
Alisema
magonjwa hayo yanazidi kuongezeka nchini hasa kwa jamii ya watu waishio
mjini na kuongeza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 80 kuwa na
magonjwa hayo kwa asilimia 1 hadi 3 na msukumo wa juu wa damu kwa
asilimia 5 hadi 10.
"Tathmini
ya mwaka 2012 iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50, inaonesha
viwango vya ugonjwa wa kisukari viliongezeka kwa asilimia 9, huku
asilimia 27 kwa msukumo wa juu wa damu," alisema Dk. Rwehimbiza.
Alisema
ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa utandawazi, ukuaji wa miji,
kutofanya mazoezi ya mwili, ulaji usiofaa, utumiaji wa tumbaku pamoja na
unywaji wa pombe kupita kiasi.
Aidha,
alisema Tanzania ilianza kujihususha na magonjwa yasiyokuambukiza
kuanzia mwaka 2009 hadi 2015, kwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi
ambao ulihusisha utekelezaji wa mpango wa taifa wa kisukari kwa
kushirikiana na chama cha wagonjwa wa kisukari nchini.
"Hadi
sasa utekelezaji wa mpango wa taifa wa kuanzisha kliniki za magonjwa
yasiyoambukiza umefikia asilimia 75 katika hospitali za mikoana wilaya
na vituo vya afya,". Nakuongeza kuwa asilimia 75 ya elimu zinazotolewa
na watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya
Afya.
Anaongeza
kuwa, shirika la afya duniani WHO, liliandaa mpango mkakati ambao
ulidhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa
hayo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza mapendekezo ya
hiari lengo ikiwa kufanikiwa kwa mkakati huo.
No comments:
Post a Comment