Monday, June 1, 2015

KAMPENI YA UELEWA KUHUSU TATIZO LA USONJI YAZINDULIWA JIJINI DAR

 Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kueneza uelewa kuhusu tatizo la usonji ‘Autism’ nchini Tanzania iliyondaliwa na Lotus Medical Clinic kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula na Daktari wa kufundisha kuongea, Nazreem Sumar.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam (katikati), akitoa utambulisho kwa meza kuu mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mtaalam wa Afya kutoka taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza, Kevin Baskerville, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula (wa pili kushoto), Daktari wa kufundisha kuongea wa Lotus, Nazreem Sumar (wa pili kulia) na Daktari Fathema Hasham.
Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam.
Mtaalam wa Afya kutoka taasisi ya Autism Education Trust ya Uingereza, Kevin Baskerville (kushoto) akipongezana na Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula,baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula (kushoto), akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Lotus Clinic, Dialla Kassam, baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari.
---
Kampenii dhidi ya ugonjwa wa usonji yazinduliwa • Familia nyingi Tanzania hazina ufahamu wa hali hii Na Mwandishi wetu
Kliniki ya Lotus kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zimeanzisha kampeni mpya inayolenga kuelimisha uma kuhusu ugonjwa wa usonji (autism), ambao watanzania wengi hawaufahamu.
Ugomjwa huu sasa unatishia familia nyingi kwani dalili zake huanza utotoni na zinaweza kuendelea hadi ukubwani.
Akizugumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia watu wenye Usonji Tanzania, Dk. Stella Rwezaula ambaye pia ni mtaalamu wa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia ana mtoto mwenye ugonjwa huo, aliishukuru Kliniki ya Lotus kwa
kuwa katika mstari wa mbele kuanzisha kampeni hiyo ili kuwaelimisha watanzania kuhusu ugonjwa huo.
“Ni vyema ugonjwa huu ukigundulika mapema na kutibiwa ili aliyeathirika aweze kupona na kuishi maisha ya kawaida hapo baadaye kulingana na athari aliyoipata. Mtoto kuanzia miaka 0-6 anaweza
kutibiwa vizuri na kusaidia kubadilisha maisha yake,” alisema.
Alisema watoto wenye hali hii wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni kurudia rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watuwengi wenye ugonjwa huu wananamna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.
“Mfano wa hali hii ni kwamba katikahali ya kawaida, mtoto wa mwaka mmoja hutabasamu au kuwa na furaha kila wakati, huiga mambo mbalimbali anayoona na kufuatilia vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye ugonjwa huu hafanyi vitu hivi,”alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kliniki ya Lotus, Dialla Kassam alisemamuelewa bado ni mdogo nchini Tanzania na watoto wengi huathiriwa na kuja kujukilana wakati hali imeshakuwa mbaya zaidi.
“Kukosa uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu na wazazi kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati kwamba watoto hawa wanahitaji uangalizi wa karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa
walimu na wenzao,” alisema.
Alisisitiza umuhimu wa kuwafundisha walimu na wazazi kuhusu watoto hawa wenye mahitaji maalumu ili waweze kuwasaidia kuishi na kukubalika katika jamii.
Alisema kliniki yake inahudumia watoto wenye mahitaji ya aina hii jijini Dar es Salaam na kuwa timu yake ina wataalamu mbalimbali wanaofanya kazi pamoja ili kutoa elimu kuhusu watoto wenye matatizo haya.
“Hii inafanyika kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo walimu na wazazi kupitia warsha,mafunzo mbalimbali, kutafuta wafanyakazi wa kujitolea na kutoa rasilimali kwa taasisi mbalimbali kama Shule ya Mbuyuni ya watu wenye ugonjwa huu,” alisema. 
Alisema kliniki mbalimbali kuhusu ugonjwa huo hufanyika katika Hospitall ya Taifa ya Muhimbili kila Alhamisi na kwamba Chama Cha Watu Wenye Usonji-Tanzania (NAPA-T) kimekuwa kikisaidia.

No comments: