Monday, April 27, 2015

BANK OF AFRICA-TAZANIA, YAZINDUA UCHANGIAJI MATIBABU KWA WATOTO WALIOPINDA MIGUU

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah. (Picha na Francis Dande)
 Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya kupinda miguu katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa  huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo yakupida miguu. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akionyesha picha za watoto wenye matatizo ya kupinda miguu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa  huo.


NA FRANCIS DANDE


BANK OF AFRICA-TANZANIA, leo imezindua rasmi kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia Hospitali ya CCBRT katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kupinda miguu.

Msaada huu kwa Hospitali ya CCBRT utawezesha watoto kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kupata matibabu bure au kwa gharama nafuu ili kuwawezesha kutembea sawa sawa.

Ugonjwa wa kupinda miguu unaweza kuathiri mguu mmoja  au yote miwili. Miguu iliyopinda huonekana kuingia ndani hasa katika goti.

Bila kupatiwa  matibabu, wagonjwa wa aina hii mara nyingi hutembea kwa kutumia magoti au au pande wa pili wa nyayo zao, lakini wakipatiwa matibabu mapema wakati wa utotoni watoto hao huweza kutembea vema na hata kushiriki mchezo wa riadha.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA-TANZANIA, Owusu- Amoah, alisema benki yake itaendelea kuisaidia CCBRT kwa kila hali, ikiwamo hilo suala la matibabu  kwa watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu ili kuboresha maisha ya  Watanzania.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemann, alisema kuwa CCBRT imekusudia kuyabadili maisha ya Watanzania, lakini hawatafanikiwa kufikia lengo lao bila kupata msaada kutoka kwa washirika wakarimu kama BANK OF AFRICA-TANZANIA.

“Kwa kusaidia matibabu ya  ya ugonjwa wa kupinda miguu, BANK OF AFRICA-TANZANIA itasaidia kuzuia  ulemavu miongoni mwa mamia ya watoto, hivyo kuboresha nmaisha yao,” alisema Telemann.

Kampeni hiyo itahusisha wafanyakazi wa benki hiyo hapa nchini, wateja na wale wote wanaosambaza bidhaa mbalimbali kwao.Telemann aliongeza kuwa dhamira hii itasaidia  kuhakikisha  watoto wetu wanakuwa na maisha bora siku za baadaye na kuzifikia ndoto zao.

Vilevile kutasaidia  kujenga jamii iliyo imarika kiafya, yakiwamo maisha ya wenye ulemavu.

No comments: