Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu John Mkwawa wakati akisoma taarifa wakati akifungua
mkutano wa siku moja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa unaohusu
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na
matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika
katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa NEC kuhusu uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya
Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika
ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Mkoa wa Iringa.
Mkurugenzi wa Idara ya habari na Elimu kwa Wapiga Kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ruth Mashama akizungumza kuhusu uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya
Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika
ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa
Na Denis Mlowe,Iringa
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetoa elimu kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa kuhusu kusambaza elimu juu ya mchakato
wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa wananchi juu ya
mfumo mpya utakaotumika kuandikisha wapiga kura wa mkoani hapa wa
teknelojia ya kibailojia(BVR).
Tume
inatarajia kufanya uboreshaji wa daftari la Kudumu wa Wapiga kura kwa
awamu ya kwanza hivi karibuni kwa kutumia Teknolojia mpya ya Biometric
Vote Regstration (BVR).
Hayo yamebainishwa juzi mjini hapa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu John Mkwawa wakati akifungua
mkutano wa siku moja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa unaohusu
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na
matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika
katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa.
Jaji Mkwawa alisema lengo ni kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa za kuwa wapiga kura waliofika umri wa miaka 18 na hawapo katika daftari la kudumu la kupiga kura,waliohama makazi yao ya awali walikojiandikisha na wanajitokeza kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema
mfumo huo mpya ni wa kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia
au tabia ya mwanadamu na kuhifadhi katika kanzi data kwa ajili ya
utambuzi na kutumia kitambulisho kipya cha kupiga kura.
“Mfumo
huu hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine, ingawa
tabia hizo za binadamu ziko nyingi, lakini kwa ajili ya kuandikisha
wapiga kura watachukuliwa alama za vidole vyote kumi vya mikono, picha na saini ndizo zitachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya wapiga kura” Alisema Jaji Mkwawa
Jaji Mkwawa alisema kupiga kura kwa Watanzania walio wengi sio lazima hivyo hawaoni thamani ya kupiga kura, hivyo Vyombo vya Habari vinawajibu mkubwa wa kuelimisha umma juu ya umuhimu
wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na ni tofauti
na nchi ya Shelisheli ambayo kujiandikisha na kupiga kura ni lazima.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya habari na Elimu kwa Wapiga Kura Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ruth Mashama akiwasilisha mada inayohusu
maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa
kutumia teknolojia ya Biometric Vote Registration (BVR) ameeleza kuwa
Tume inatarajia kuboresha Daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya
kwanza hivi karibuni na maandalizi yake tayari yamekamilika kwa sehemu
kubwa na baadhi ya vifaa vimeanza kuwasili nchini Tanzania.
Alisema matumizi ya mfumo mpya utatumika katika zoezi la uandikishaji pekee
tofauti na nchi nyingine zilizotumia mfumo hadi katika kupiga kura na
kugundua mafanikio yaliambatana na changamaoto mbalimbali za
kiteknolojia na kimfumo.
Mashama
alizitaja baadhi ya nchi za Kiafrika zilizokwisha tumia mfumo wa BVR
kuwa ni Nigeria 2007,Ghana 2009,Liberia2005,Guinea 2005,Mali 2005,
Uganda 2008,Kenya 2013,Zambia 2008, Afrika Kusini na Zanzibar 2009.
No comments:
Post a Comment