Saturday, June 14, 2014

WABUNGE DODOMA WAMFAGILIA FILIKUNJOMBE WASEMA AMEVUNJA REKODI KUPELEKA WAGENI WENGI BUNGENI

Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa nne  kushoto akiwa na wanahabari na viongozi wengine mjini Dodoma
Mbunge Filikunjombe mwenye suti na tai nyekundu katikati akiwa na wageni wake mjini Dodoma
Waziri mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na wageni wa mbuge Filikunjombe
Waziri mkuu Pinda akisalimiana na wajumbe  wa mbunge Deo Filikunjombe  waliotembelea  bunge juzi ,kulia ni mbunge Filikunjombe
Ujumbe kutoka kwa  mbunge Filikunjombe  ukiwa bungeni
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa na ugeni wa  mbunge Filikunjombe
Mbunge Filikunjombe kushoto akiteta  jambo na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa bunge
Mbunge   wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza na timu ya ujumbe wake mjini Dodoma
Waziri mkuu wa mstaafu Mhe Edward Lowassa  akizungumza na  wajumbe 92  kutoka  jimbo la Ludewa  ambao ni  wenyeviti kata na makatibu kata kutoka kata  zote 25  za  jimbo la  Ludewa 
WAZIRI  mkuu wa  zamani  Edward  Lowassa   na wabunge mbali mbali wamempongeza  mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali  za  kuwakomboa wana Ludewa .
Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli alitoa pongezi hizo mjini Dodoma juzi  nje ya ukumbi wa bunge wakati akisalimiana na viongozi wa CCM ngazi ya kata  zaidi ya 92 waliofika bungeni kushuhudia shughuli za bunge kwa mwaliko wa mbunge Filikunjombe.
" Wana Ludewa mna kila  sababu ya  kujivunia kwa  kuwa na mbunge mchapa kazi ninyi mnamwita Jembe ila  mimi namwona zaidi ya  jembe ni katapila na hamkokosea  kumchagua nawaombeni mtunzeni mbunge  wenu na epukeni na michepuko kwani ni mbunge makini na anayependa kuwatumikia"alisema Lowassa
 Mbunge  wa jimbo la mbinga Magharibi kepten John Komba  amempongeza mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe  kutokana na jitihada  mbali mbali anazoendelea  kuzifanya katika  kuwatumikia wana Ludewa.
Komba  ametoa  pongezi  hizo juzi wakati wa hafla fupi ya  kuwakaribisha wajumbe 92  kutoka  jimbo la Ludewa  ambao ni  wenyeviti kata na makatibu kata kutoka kata  zote 25  za  jimbo la  Ludewa na viongozi  wa  wilaya ambao  wapo katika  ziara  ya  siku nne mjini  Dodoma na Dar es Salaam .
Alisema  kuwa jembo kama  Filikunjombe katika historia ya  jimbo la Ludewa ni aliyepata  kuwa mbunge  wa jimbo hilo marehemu Holace Kolimba na baada ya hapo mbunge mchapakazi ni Filikunjombe .
“Nasema mmlea    Deo Filikunjombe ni mbunge atakayefanya makubwa  jimbo la Ludewa  kutokanana jitihada  zako  za kimaendeleo na kazi  kubwa anayoifanya ya  kuwatumikia  wananchi  wa  jimbo la Ludewa ….nataka  kuwaambieni  leo viongozi ambao mpo hapa Filikunjombe  kwangu  mimi amekuwa msaada mkubwa  sana”
Hata  hivyo alisema kuwa  jitihada kubwa  zimekuwa  zikifanywa na Filikunjombe pamoja na wabunge  wengine wa  mkoa  wa Ruvuma  ambao  wanazunguka ziwa nyasa kutokana na adha  kubwa ya  usafiri  ila kwa  sasa kero ya  usafiri ikiwemo  ile ya mlima kandamija
Pia  amewaonya  wana Ludewa  kuacha  kutafuta  mbunge kama ndugu  yao na badala  yake kumtafuta  mbunge  wa  ajili ya  kuwapelekea maendeleo kama ilivyo kwa  mbunge  huyo ambaye amekuwa ni mwabikaji mzuri kwa wananchi.
“Mkimuacha  Deo  Filikunjombe  Ludewa  mmekosa mambo na mmekosa maendeleo  katika  jimbo  hilo hivyo  ni lazima  kuendelea  kumtunza  ili  azidi kuwatumikia zaidi”
Komba  alisema kuwa  wilaya ya  Ludewa mbali ya  kuwa na utajiri mkubwa madini ila  wabunge   wote  waliopita  walikuwa  wakizungumzia suala  hilo  bila kuonyesha  jitihada  ila toka ameingia  Filikunjombe  madini  hayo yameanza kushughulikiwa .
Alisema kuwa  kwa sasa  wananchi  wa Mwambao   kilio  chao  kikubwa ni meli na kuwa  tayari  wabunge  wote  wa Mwambao wameungana kuona wanapigania upatikanaji  wa  meli  hiyo ili  kutatua kero  ya  usafiri  ziwa Nyasa .
“Mwisho  nasema endeleeni kumpatia  ubunge Deo Filikunjombe msibadilishe wabunge kama gauni…wenzetu  wa kaskazini  wanatushinda katika  hilo mfano Msuya aliacha  ubunge  baada ya  kusema mwenyewe  sasa  basi baada ya kufikisha maendeleo makubwa ikiwa ni  pamoja na kufikisha umeme  hadi  chooni ….ila sisi baada ya kipindi kimoja tunasema aliyevivyo(amekula hivyo hivyo)”alionya Komba .
Huku  kwa upande  wake , Mbunge wa Mbinga Mashariki Gaudence CassianKayombo  alisema  kuwa mbali ya  wana Ludewa  kumuona mbunge  wao ni jembe  ila kwake na  wabunge  wengine na  kusini wamekuwa  wakimuona ni mkombozi  wa  maendeleo  mikoa ya  kusini.
Kayombo pia  amewaonya  wana Ludewa  kuachana na tabia ya  kubadili wabunge kama nguo na  kuwa  iwapo  mbunge  wao  asingekuwa mchapakazi  ni wazi harufu ya  upinzani  ingeanza  kujitokeza katika jimbo hilo ambalo limeendelea  kuwa ni tishio hata kwa  vyama  vya upinzani .
Kwani  alisema  jitihada za  wana Ludewa  kujaribu  kwa  sasa  zimefika  kikomo baada ya kumpata  mbunge  huyo ambae  ni mchapakazi mzuri na kuwa ni vema wana Ludewa  hawana haja ya  kuendekeza uchoyo .
“Kitu ambacho  kitaendelea  kuiweka CCM madarakani ni umoja na mshikamano na  bila  umoja na mshikamano  hakuna chama na hakuna mbunge ndani ya CCM”
Kwa  upande  wake  mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Mbeya Hilda Ngowi  mbali ya  kumpongeza  mbunge  Filikunjombe kwa  maendeleo bado  alisema  kuwa mbunge  huyo ameleta ngunzo kubwa  bungeni kwa  kuvunja  rekodi ya kukaribisha  wageni  wengi  zaidi  bungeni tukio ambalo ni la kwanza kwa mbunge kuleta  wabunge  wengi kiasi hicho bungeni.
 Huku mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akisema  kuwa anatamani sana kufika Ludewa ili kumuunga mkono mbunge Filikunjombe ambae amekuwa ni ngunzo katika bunge kwa  utendaji kazi na kutetea maslahi ya  wananchi wake na Taifa.
Mbunge  wa  jimbo la Mwibara  Kangi Lugola alisema  kuwa kamwe katika ubunge wake hatakuja kumsahau mbunge Filikunjombe na  kudai kuwa lazima  viongozi  wa kata na  wanachi wa  jimbo la Ludewa kuachana na michepuko kwa  kutazama huku na kule badala yake  kutulia njia kuu kwa maana ya  kuendelea  kufanya kazi na Filikunjombe.
Wakati  Filikunjombe akidai  kuwa  wito ambao  wajumbe hao  wameonyesha ni wito mzuri  zaidi na  kuwa hilo ni  deni  kwake  na malipo  yake ni  kuwafikishia maendeleo jimboni.
Kwani alisema  kuwa kamwe hatawaangusha  katika utendaji kazi  wake  na  kuwa ni lazima aendelee  kufanya kazi kwa  moyo  zaidi  ili kuwapa imani  wananchi 

No comments: