Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi mkoa wa Iringa Mariam Mwakingwe wa kwanza kulia mwenye suti akiwasikiliza wakufunzi kutoka benki ya wanawake Tanzania ambao wapo mjini Iringa kwa ajili ya kuwakopesha |
Mwakalebela katikati akiwa na wakufunzi wa mafunzo ya ujasiliamali wanaopaswa kupewa mikopo ya benki ya wanawake Tanzania |
Mwakalebela katikati akitoa maelekezo kwa wajasiliama mali wanaohitaji mikopo ya benki ya wanawake Tanzania |
baadhi ya wajasiliamali wenye ulemavu wanaoshiriki semina ya ujasiliama mali chini ya ufadhili wa kampuni ya VANNEDRICK (T) Ltd kwa ajili ya kukopeshwa fedha na Benki ya wanawake Tanzania (TBW) wakimsikiliza mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujasiliamali nchini ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela (katikati) wakati wa semina hiyo inayoendelea katika ukumbi wa maendeleo ya jamii mjini Iringa |
Na Francis Godwin Blog
MKURUGENZI mtendaji wa kampuni ya ujasiliamali nchini ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela amewataka wajasiliamali mjini Iringa kuepuka matapeli wanaotaka kuwatoza fedha ili kunufaika na mikopo ya benki ya wanawake Tanzania (TBW).
Pia Mwakalebela amepongeza jitihada za wanawake na wajasiliama mali mjini Iringa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo ya ujasiliama mali kabla ya kukopeshwa na benki hiyo hivi karibuni .
Akizungumza jana wakati wa mwendelezo wa semina hiyo kwa wajasiliama mali katika ukumbi wa maendeleo ya jamii Kitanzini mjini hapa ,Mwakalebela alisema kuwa amefurahishwa na idadi kubwa ya wanawake wapatao zaidi ya 400 ambao wamejitokea kutaka mikopo hiyo japo wapo baadhi ya watu wanaweza kutumia njia hiyo kwa ajili ya kujipatia fedha kijanja .
" Neema kama hizi zinapojitokeza wapo baadhi ya watu wasio na malengo mazuri ambao wamekuwa wakitaka kujinufaisha kwa kuwachangisha fedha wajasiliama mali hao ili kupata mikopo .....hivyo wanawake wote na wajasiliamali wanapaswa kuwa makini wasikubali kutoa pesa yoyote kwa ajili ya mikopo ya TBW "
Mwakalebela alisifu utaratibu wa benki hiyo ya wanawake Tanzania kuwa haumtaki mwomboji wa mkopo kuchangia fedha yoyote zaidi ya kufungua akaunti ya kikundi kwa kiasi cha Tsh 10,000 pekee kabla ya kukopeshwa mkopo husika.
Hata hivyo Mwakalebela kama mdhamini mkuu wa mafunzo hayo mkoani Iringa alisema kuwa amevutiwa zaidi na mwitikio mkubwa wa wajasiliama mali kujitokeza kushiriki mafunzo hayo tofauti na mikoa mingine ambayo benki hiyo imepata kupita na kuwawezesha wajasiliamali kama hao.
Alisema kwa upande wake amepata kuzunguka maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa hasa yale ya pembezoni na kuwahamasisha wajasiliamali kujitokeza kujiunga na vikundi ili kunufaika na mikopo hiyo kupitia benki hiyo ya wanawake Tanzania.
Pia alisema kuwa hadi sasa tayari ofisi ya TBW imefunguliwa katika jengo la benki ya Posta mjini Iringa ili kuwawezesha wananchi wenye shauku ya maendeleo kuweza kufika kujiunga na benki hiyo na kupewa mikopo.
Mwakalebela alisema kuwa kwa wale ambao walianza kupewa mafunzo mapema zaidi wataanza kupokea mikopo yao wakati wotote ndani ya mwezi huu .
No comments:
Post a Comment