Saturday, April 19, 2014

BONANZA LA MICHEZO LA PPF LAFANA SANA

Mkufunzi wa mazoezi ya viungo, Taifa Liwewa (Kushoto), akiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa mazoezi ya viungo, kwenye bonanza la michezo lililoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika viwanja vya Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 19, 2014. Mgeni rasmi kqwenye tamasha hilo lililoshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo, kuvuta kamba na soka, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akikagua timu za soka za Mfuko huo, wakati wa Bonanza hilo.
Wafanyakazi wa PPF, wakiwa kwenye mazoezi ya kunyoosha mgongo.
Wafanyakazi wa PPF, wakiwa kwenye mazoezi ya kuimarisha misuli ya mikono.
Mkurugenzi wa Mifumo wa Mawasiliano ya Computer wa PPF, Robert Mtendamema (Aliyetazama camera), akiwa miongoni mwa wafanyakazi walioshiriki mwanzo mwisho kwenye mazoezi ya viungo pamoja namchezo wa soka.
Timu za soka za Mfuko wa Pensheni wa PPF, zikiwa katika picha yab pamoja kabla ya kuanza kwa pambano hilo.
Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Mfuko wa Pesnheni wa PPF, ikizidiwa nguvu na wenzao wanaume kwenye mchezo wa kuvuta kamba. Hata hivyo timu hiyo ilijitutumua kwani katika raundi ntatu, ilishinda kwa taaabu raundi moja.
Mchezaji wa soka wa timu ya PPF, kutoka idara ya Utawala, Johnson Aloyce (Kushoto), akichanja mbuga, wakati wa pambano la soka dhidi ya Idara ya kuzuia Majanga.
Meneja Uhusiano nna Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (Katikati), akiwa sambamba na wafganyakazi wenzake, wakati wa mazoezi ya viungo.
Mkurugenzi Mkuu, wa PPF, William Erio, akitoa nasaha zake kwa wafanyakazi walioshiriki tamasha hilo la michezo.

No comments: