Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City,
Allen Killango (kushoto), akimkabidhi msaada wa mabenchi, Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Palestina Sinza, Dk. Benedict Luoga yaliyotolewa na Benki ya CRDB tawi la Mlimani
City kwa ajili ya kupumzikia wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo. Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen
Killango (kulia), akimuonesha Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Palestina Sinza, Dk. Benedict Luoga, mabenchi yaliyotolewa
na benki ya CRDB tawi la Mlimani City kwa ajili ya kupumzikia wagonjwa wanaofika katika
hospitali hiyo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Dk. Benedict Luoga akiangalia mabenchi yaliyotolewa na Benki ya CRDB tawi la Mlimani City.
Sehemu ya msaada wa mabenchi yaliyotolewa na Benki ya CRDB.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Dk. Benedict Luoga (wa pili kushoto) akizungumza naMkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango .
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Dk. Benedict Luoga akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango mara baada ya kukabidhi msaada wa mabenchi ya kupumzikia.
Maofisa wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango.
Uongozi wa Hospitali ya Palistina Sinza ukiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki ya CRDB baada ya kukabidhi msaada wa mabenchi ya kupumzikia.
Na Francis Dande

BENKI ya CRDB tawi la Mlimani City, imekabidhi mabenchi kwa ya kuumzikia wagonjwa katika hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar es salaam ikiwa ni uendelezaji wa
mpango mkakati wa kusaidia huduma za jamii.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mabenchi sita ya kisasa, Mkurugenzi wa Tawi hilo, Allen
Killango, alisema CRDB hutenga asilimia moja ya faida yake ili kusaidia
maendeleo ya jamii katika afya, elimu na utunzaji wa mazingira.
Killango, alisema kwa mwaka 2013 CRDB imesaidia kuboresha
mazingira ya hospitali ya Mkoa Morogoro kwa kukarabati wodi ya watoto, kuweka
vitanda, mashuka, magodoro na vyandarua.
Alisema pia wameikarabati hospitali ya rufaa Mbeya,
wodi ya wazazi Bugando ikiwemo kufanya kampeni ya kuboresha mazingira ya
hospitali kwa kupanda miche ya miti.
“CRDB inaamini katika afya na siha kwa wateja wake, hakuna taifa
lolote duniani linaloendelea kama wananchi wake hawana afya njema au hawapati
huduma za hakika za matibabu,”alisema.
Naye Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Benedict
Luoga, alishukuru CRDB kwa masaada huo na kuzitaka taasisi nyingine kuwasaidia
kwani wana mapungufu ya mashuka, vitanda na magodoro.
“CRDB tunaishukuru sana maana ni benki inayorudisha
faida hivyo tumepokea kwa mikono miwili na tutayatunza mabenchi na kuhakikisha
yanatumiwa na watu wengi zaidi,”alisema.
Hadi sasa CRDB imeendelea kupanua mtandao wake kwa
kufungua zaidi ya ATM 350 zinazopokea kadi za visa, ikiwemo Mastercard, ChinaunionPay card.
No comments:
Post a Comment