Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akibusu petu ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza,Yuda Thadei Ruwaichi wakati alipowasili kwenye Kituo cha Utamaduni wa kabila la Wasukuma cha Bujora kilichopo Kisesa Mwanza ambako alizindua sherehe za utamaduni wa Wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo, Juni 2, 2013.
Baadhi ya watemi wa Kisukuma wakiingia kwenye Kituo cha Utamaduni wa kabila la Wasukuma cha Bujora kilichopo Kisesa Mwanza ambako sherehe za Utamaduni wa wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo zilifanyika Juni 2, 2013.
Baadhi ya washiriki wa sherehe za umtamaduni wa Wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia alipozindua sherehe hizo kwene uwanja wa Bujora Kisesa jijini , Mwanza juni 2, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea fimbo ya Kitemi kutoka kwa Antonia Mipamo maarufu kwa jina la Tonisiza ambaye pia ni Mtemi Chigoku Masa wa Simiu baada ya kutawazwa muwa Mtemi wa Wasukuma wakati alipozindua sherehe za Utamaduni wa Wasukuma katika uwanja wa Bujora, Kisese jijini Mwanza Juni 2, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na baadhi ya watemi wa kabila la Wasukuma waliomkabidhi zawadi mbalimbali kabla ya kuzindua sherehe za utamaduni wa kabila la Wasukumba kwenye uwanja wa Bujora, Kisesa jijini Mwanza Juni 2, 2013.
Baadhi ya wapiga ngoma wakionyesha ufundi wao katika sherehe za utamaduni wa Wasukuma zilizozinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa Bujora, Kisesa jijini Mwanza Juni 2, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Mwanza, Yuda Thadei Riwaichi (kulia) wakifurahia ngoma ya wasukuma katika Sherehe za Utamaduni wa Wasukuma kwenye uwanja wa Kisesa jijini Mwanza Juni 2, 2013. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye hivi karibuni alitawazwa kuwa Mtemi Kishosha wa Dutwa, Bariadi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
No comments:
Post a Comment