Askari
wa kikosi cha bendera kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) wakitoa heshima kwa mwendo wa haraka mbele ya Luteni Jenerali
Mstaafu Abdulrahman Shimbo (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kumuaga
zilizofanyika leo katika kambi ya jeshi hilo Mgulani jijini Dar es
Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa
zaidi ya miaka 41 na kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Askari
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakitoa heshima kwa mwendo wa pole
mbele ya Luteni Jenerali Mstaafu A Shimbo (hayupo pichani) wakati wa
sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni
Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41
kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Luteni
Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kushoto) akiangalia kwa furaha
funguo za gari aina ya Toyota landcruiser alilopewa zawadi na Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo alilitumikia kwa kipindi
cha zaidi ya miaka 41 huku Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali
Davis Mwamnyange akimuangalia. Sherehe za kumuaga zilizofanyika leo
katika kambi ya Jeshi hilo Mgulani jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meja
Generali Grace Mwakipunda.
Mkuu
wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange akimkabidhi hati
ya utumishi Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kushoto) wakati
wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.
Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya
miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Luteni
Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (aliyesimama kwenye gari)
akisindikizwa maafisa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) ikiwa ni kuhitimisha sherehe za kumuaga rasmi
zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu
Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika
nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Baadhi
ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
wakiangalia gwaride la sherehe za kumuaga Luteni Jenerali Mstaafu
Abdulrahman Shimbo (hayupo pichani) zilizofanyika leo katika kambi ya
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es
Salaam.
Luteni
Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo akikagua kikosi cha askari wa kike
kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa
sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.
Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya
miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Ndugu,
jamaa na marafiki wa Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (wan
ne mstari wa mbele kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.Wa katikati
mstari wa mbele ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis
Mwamnyange.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment