Mabao ya Mtibwa Sugar la kwanza lilipatikana dakika ya 34 kwa shuti kali la mchezaji Mohamed Mkopi wa Mtibwa baada ya kipa Juma Kaseja kuutema mpira ulopigwa na mshambuliaji Vicent Barnabas .
Bao la pili lilifungwa katika dakika ya 88 na mchezaji Hussen Javu kwa shuti la mbali ndani ya eneo la hatari baada ya Kaseja kuingia kugugumizi cha kuupiga mpira wa karibu aliorudishiwa na Beki Ramadhan Chombo ,na badala aliuparaza na kufikia mfungaji aliyepiga shuti la juu na mpira kujaa wavuni na kuandika bao la 2 kwa Mtibwa Sukari.
Kufuatia uzembe huo , Kaseja alijifunika uso kwa jezi yake na mikono akijutia kosa hilo ambalo lilikuwa ni la pili , awali liligharimu kufungwa bao la kwanza.
Kaseja katika mchezo huo ilionekana kama alishinikizwa kucheza kwa vile jina lake halikuwemo kwenye orodha iliyowasilishwa kwa waandishi wa habari na lilikuwa jina la Wiebert Mweta , lakini ghafla kabla ya kuanza kwa mchezo yalifanyika mabadiriko ya kulifuta jina la Mweta na kuandikwa la Kaseja na yenye kuwa kipa wa akiba.
Hata hivyo baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mashabiki wa Simba walivamia benchi la ufundi na kumzonga Kocha Mkuu , Milovan Cirkovik , wakilalamika kupangwa kila mchezo kwa kipa Kaseja , wakidai uwezo wake umeshuka na kutaka mabadiriko , lakini Milovan alikabia kimya akiangaria taharuki ya mashabiki wa timu hiyo , hapakuwa na kiongozi yeyote aliyotoa ufafanuzi kuhusu mabadiriko ya ghafla ya kupanga Kaseja wakati hakuwemo kwenye orodha ya awali ya wachezaji.
Kina Ras Makunja wakimdhibiti mtu anayedhaniwa ni shabikiwa simba aliyerusha chupa ya maji na mawe kwa Mwamuzi Judith Gamba wa Arusha ( hayupo pichani) Nov 4, wakati wa mchezo na Mtibwa Sugar
Huzuni katika benchi la Wekundu wa Msimbazi baada ya jahazi lao kuzama kwa bao 2-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar
Kikosi cha Simba kilichovaana na Mtibwa Sugar
Kipa Juma Kaseja akifarijiwa na mmoja wa mashabiki wake mara baada ya mchezo kumalizika
Makamu Mwenyekiti wa Simba, ' Kaburu' kati kati akisalimiana na viongozi wa Mtibwa sukari akiwemo Jamal Bayser aliyekaa kushoto, kabla ya kuanza mchezo
Sehemu ya umati wa watu uwanja wa Jamhuri moro juzi pambano kati ya Simba na Mtibwa Sugar, Simba ililala bao 2-0
Kikosi cha Mtibwa Sugar, kilichopambana na Simba
Picha na John Nditi
No comments:
Post a Comment