PICHA NA HABARI NA JOHN NDITI
UONGOZI NA KAMATI YA SHULE YA MSINGI, MASANZE ILIYOPO KATIKA KIJIJI CHA SANGA SANGA , KATA YA MZUMBE, WILAYA MVOMEO, UMEPATIWA MDAASA WA MADAWATI 50 KATI YA 76 KUTOKA NMB MAKAO MAKUU KUTOKANA JUHUDI ZA MBUNGE WA JIMBO LA MVOMERO, AMOS MAKALLA, AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO,
HII NI BAADA YA KUUOMBA UONGOZI HUYO KUSAIDIA MADAWATI KATIKA SHULE KADHAA ZA MSINGI JIMBONI MWAKE.
MSAADA HUO UMETOLEWA BAADA YA ZIARA YA MBUNGE HIYO KUANDIKA BARUA YA KUIOMBA BENKI HIYO WAKATI ALIPOJIONEA MWENYEWE HALI MBAYA YA UHABA WA MADAWATI WAKATI WA ZIARA KATIKA VIJIJI KADHAA IKIKIWEMO CHA SANGA SANGA.
NA OKTOBA 25,MWAKA HUU NMB ILITIMIZA UTEKELEZAJI WA MAOMBI HAYO KWA MKUMKABIDHI MBUNGE HUYO MADAWATI 76.
KATI YA MADAWATI HAO , 50 WALIPEWA UONGOZI WA SHULE HIYO ILI KUPUNGUZA TATIZO SUGU LA UHABA WA MADAWATI NA YALIYOSALIA YAMEPANGIWA KUISAIDIA SHULE NYINGINE AMBAYO NAYO IMEKUBWA NA UHABA MKUBWA WA MADAWATI.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, ( kati kati ) akiwa ameketi kwenye dawati, na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki hiyo, Gabriel Ole Loibanguti (kushoto) na ( kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Shule ,Leochrista Bavon, ni baada ya makabidhiano ya madawati 50 kati ya 76 yaliyotolewa na NMB kufuatia maombi ya msaada wa Mbunge huyo ili kukabiliana na uhaba wa madawati kwenye baadhi ya shule za Msingi Jimboni humo, hafla iliyofanyika shuleni hapo, Oktoba 25, mwaka huu.
Kukata utepe
Wanafunzi
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, ( kushoto) akipeana mkono na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya NMB , Gabriel Ole Loibanguti , Oktoba 25, mwaka huu ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya msaada wa madawati 50 kwa shule ya Msingi Masanze,iliyopo Kijiji cha Sanga Sanga, Kata ya Mzumbe, kufuatia ombi la Mbunge huyo kwa Uongozi wa makao makuu ya Benki hiyo hivi karibuni (kati kati ) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ,Leochrista Bavon.
Furaha
Wanafunzi na mfadhili wao
Mwalimu akishukuru kwa msaada
Picha ya pamoja na walimu
No comments:
Post a Comment