Mama Salma Kikwete akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar, Balozi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataifa Mhe. Amina Salum Ali na Mshauri wa Rais mambo ya Diplomasia Balozi Liberata Mulamula kabla ya kuhudhuria mkutano wa African First Ladies Roundtable jijini New York, Marekani, leo
Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Bibi Katalin Bogyay Balozi wa Hungary UNESCO na amebobea katika diplomasia ya utamaduni na mtetezi mkubwa wa masuala yahusuyo fursa sawa ya elimu kwa mtoto wa kike.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo
Mama Salma Kikwete akihudhuria mkutano huo
Baadhi ya washiriki
Mama Salma Kikwete akipokea vipeperushi katika mkutano huo
Mama Kikwete akisalimiana na baadhi ya washiriki
Picha ya pamoja
SIMU ZA MKONONI ZINAWEZA KUWAKOMBOA
WANAWAKE
KIUCHUMI - SALMA KIKWETE
Na Mwandishi Maalum
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete , amesema tekinolojia
ya mawasiliano ya simu za mkononi, kama ikitumiwa vema, inaweza kuwa chombo muhimu katika kuchagiza na kuwaletea maendeleo ya
haraka wanawake na wasichana hususani
wale wa vijijini.
Mama
Kikwete ameyasema hayo, wakati alipokuwa akitoa mchango wake katika
majadiliano ya kwanza na ya aina
yake. Majadiliano yaliyowaleta meza
moja, baadhi ya wake wa marais, wakurugenzi wa
makampuni,wahadhiri na wanadiplomasia, kujadiliana na kubadilishana mawazo
na mbinu zitakazoweza kuwahamasisha watoto wa kike kuchangamkia masomo
ya Sayansi, Tekinolojia, Uhadinsi na Hesabu
( STEM)
Majadiliano
hayo ambayo yalifunguliwa na Bi. Anitta
Kalinde, Waziri wa Masuala ya Jinsia
kutoka Malawi kwa niaba ya Rais wa Malawi.Yamefanyika siku ya jumatatu katika
ukumbi wa mikutano wa jengo la Credit Suisse, Jijini New York.
Aidha Majadiliano hayo , yalilenga pia kuwachagiza viongozi
hao kutumia nafasi walizo nazo, uelewa wao na uwezo walionao katika
kuwasaidia wanafunzi wa kike kung’amua mapema vipaji vyao na hivyo kupata fursa ya kuvitumia vipaji hivyo kufikia malengo, matarajio na
ndoto zao kuhusu maisha yao ya baadaye.
Kupitia teknolojia ya simu za mkononi, Mama Salma amebainisha kwamba kwa nchi za Afrika
ikiwao Tanzania, siyo tu kwamba ni
tekinolojia rahisi ya mawasiliano lakini inawawezesha wanawake, kubuni
na kuanzisha miradi ya kiuchumi kwa kuwa mawasiliano hayo yanawapa fursha ya
kupata habari na kubadilishana mawazo na makundi mbalimbali ya jamii.
“
Ninawashukuru kwa kunialika katika majadiliano haya, lakini kilichonifurahisha
zaidi ni mada yenyewe. Tunahitaji
kukusanya nguvu zetu, uwezo wetu na maarifa yetu kuwasaidia wanawake na
wasichana wa vijijini kunufaika na tekinolojia rahisi zilizopo kujiletea
maendeleo yao na kuondokana na umaskini”. Akasema Mama Salma
Na kuongeza, tekinolijia hiyo ya simu za mkononi ni mfano
mmoja tu lakini zipo teknolojia nyingi na rahisi ambazo kwazo zinaweza
kuwanufaisha wanawake na wasichana ikiwa
watapewa na kuwezeshwa kujifunza masomo
ya sayansi, hesabu, uhandisi na tekinolijia.
Na kwa sababu
hiyo, Mke wa Rais amesema, ili wanawake
na wasichana wanaweze kunufaika na teknolijia zilizopo kunahitajika ushirikiano na ubadilishanaji wa mawazo na
uzoefu wa namna bora ya kuwasaidia.
“Wito wangu kwetu sote tuliokusanyika hapa, ni huu, tujenge mitandao, tubadilishane uzoefu, na utaalamu wa kuwasaidia wanawake na watoto
wa kike na kwa upande mwingine kuwapa fursa wanawake na wasichana nao kutembeleana
na kujufunza baina yao”. Akasisitiza.
Aidha amesema kwa kutambua umuhimu wa wasichana kupata elimu, ikiwamo maarifa na ujuzi mbalimbali. Yeye
binafsi kupitia taasisi yake ya wanawake na Maendeleo ( WAMA) imekuwa mstari katika kuwasaidia watoto wa kike kufikia
malengo yao.
Akatumia nafasi hiyo,
kuwakaribisha wajumbe wenzie kutembelea Tanzania na kujionea jitihada
mbalimbali zinazofanywa na Serikali na
WAMA katika kusukuma mbele maendeleo ya
wanawake na watoto wa kike.
Katika maajadiliano hayo, baadhi ya washiriki
akiwamo Bibi Savanna Maziya
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi
la Makapuni ya Bunengi ( Bunengi Group of Companies), na mwanzilishi wa majadiliano
hayo, wameonyesha nia ya kuja
Tanzania kutambua maeneo ya ushirikiano
hususani katika eneo hilo la kuwasaidia na kuwawezesha watoto wa kike
kumudu masomo ya STEM.
Tayari Bibi
Savanna kupitia Kampuni yake ameanza
kuwasaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kumudu na kuyakabili
masomo ya sayansi katika baadhi ya shule
nchini Marekani, na tayari ameanza kuona mafaniko makubwa kwa
watoto hao kufanya vizuri
Aidha Dkt, Herta
von Stiegel, Mkurugenzi Mtendaji na
mwanzilishi wa Kampuni ya Ariya Capital
Group Limited yeyé, na ambaye tayari
kampuzi yake imeanza kuwekeza nchini Tanzania
katika uvunaji wa umeme wa upepo. Anasema kwa kadri hali ya mabadiliko
ya dunia yanavyoendelea, Afrika inabaki kuwa ndilo bara lenye
raslimali nyingi zikiwamo za ardhi, madini na nguvu kazi kubwa.
Akasema wakati
idadi ya watu ikipungua katika nchi zilizoendelea, idadi ya watu inaongezeka barani afrika
na kwa sababu hiyo akashauri
kwamba idadi ya watu inayoongezeka
barani afrika inapaswa kutumika si tu kama nguvu kazi, bali yenyewe iwezeshwe ili ichukue nafasi ya kuendesha
uchumi na maendeleo ya nchi zao.
Dkt. Stiegel
amesema huu ni wakati muafaka pia kwa makapuni ya kibiashara kutafuta fursa za
uwekezaji nchini Tanzania, nchi ambayo
ameitaka kama yenye vivutio vingi vya uwekezaji.
No comments:
Post a Comment