Balozi
wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mh Balozi Dr Diodorus Kamala akifanunua
kuhusu maendeleo katika nchi ya Tanzania wakati wa hafla hiyo ya
kusherehekea miaka 50 utaifa kati ya Tanzania na Uingereza.
Salam,
Siku
ya jumanne tarehe 25.9.12 Jumuiya ya Uingereza- Tanzania ( BRITAIN-
TANZANIA SOCIETY) iliandaa hafla fupi ya kusherekea miaka 50 ya Utaifa
kati ya Nchi ya Uingereza na Tanzania katika ukumbi wa The Royal
Commonwealth Club, London.
Wageni
mbalimbali pamoja na wanachama walijitokeza kwa wingi kuhudhuria hafla
hii fupi ilioandaliwa hususani kwa ajili ya kuchangia nchi ya Tanzania.
Mojawapo ya wageni waliohudhuria ni pamoja na balozi wetu Peter
Kallaghe pamoja na mkewe Mama balozi Joyce Kallaghe, Mwenyekiti wa
Britain- Tanzania Society William Fulton JP DL.
Mgeni
rasmi katika shughuli hii alikua ni Balozi wa Ubelgiji Mh Dr Diodorus
Kamala aliyetoa mada maalum kuhusu mafanikio, maendeleo na changamoto
katika nchi ya Tanzania na jumuiya nzima ya Afrika mashariki. Aidha Mh
Dr Kamala alifafanua jinsi uchumi wa Tanzania unavyokua kwa kasi
kutokana na takwimu kutoka Benki ya Dunia pia aliongelea kuhusu masuala
ya utalii, mioundo mbinu, hali ya amani na usalama ambazo zimepelekea
wawekezaji wengi kuwekeza katika nchi ya Tanzania.
Nchi
ya Uingereza ndio nchi pekee inayoongoza katika uwekezaji katika nchi
ya Tanzania Ikifuatiwa na India pamoja na Kenya
Pamoja na hayo Mh Dr Kamala aliwashukuru wana jumuiya wa Uingereza-
Tanzania kwa kuendelea kuisaidia Tanzania kwa hali na mali ili kupambana
na hali ya umaskini.
Baada
ya kutoa mada yake kulikuwa na kipindi kifupi cha maswali na majibu
kutoka kwa wanajumuiya pamoja na wadau waliohudhuria.
Nae mwenyekiti wa Computer 4 Afrika ndg Aseri katanga alitoa risala fupi
ya kumshukuru mgeni rasmi kwa kujitolea kwake kuja kujumuika na
wanajumuiya pamoja na hotuba yake nzuri kuhusu Tanzania.
Vile
vile halfa hii ilijumuisha uoneshwaji wa picha zilizochorwa na
wachoraji kutoka Tanzania ambazo zilinadiwa ili kuchangisha pesa za
kuwasaidia kuwainua wadau wa tasnia ya uchoraji Tanzania. Baadhi ya
wachoraji ambazo picha zao zilionyeshwa ni Mmadi Ausiy, Haji Chilonga,
Hassan Kadudu, Florian Ludovick Kaija, James Haule na Aggrey Mwasha.
Asanteni,
Urban Pulse Creative
Mkutano Ukiendelea.
Msanii Francia Chengula akiimba wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa Computer 4 Afrika (katikati) Aseri Katanga akifuatilia mada ya Mh Balozi Kamala.
Mwenyekiti wa Computer 4 Afrika Aseri Katanga akisoma risala fupi ya kumshukuru Mgeni Rasmi na wageni waalikwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uingereza- Tanzania William Fulton JP DL akiongea na Urban Pulse baada ya Mkutano.
wadau wakibadilishana mawazo pamoja.
Balozi Dr Kamala akiwa na Sir Andy Chande.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh Peter Kallaghe akiwa na Susan Mzee na Sheilamina
Mama Balozi Joyce Kallaghe katika picha ya Pamoja Nelly Sheilamina na Elly baada ya mkutano.
Mh Balozi Dr Diodorus Kamala (Kulia) Frank Eyembe na Aseri Katanga.
No comments:
Post a Comment