Sisi ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza tunaosoma nchini Algeria kutoka Tanzania,tumeamua kutuma taarifaa hizi katika vyombo vya habari kuhusu bodi ya mikopo yaani kuhusu utumaji wa pesa kwetu sisi
YALIYOMO
· Ahadi za kutuma pesa
· Utumaji wa akaunti
· Maisha tunayoishi sasa
· Utumaji wa pesa usiokamilika
· Madeni
· Jitihada za viongozi
· Matatizo
Ø AHADI ZA KUTUMA PESA
Tarehe 8 /10/2011 tulipokuwa tunajiandaa na safari ya kuja nchini Algeria tulikabidhiwa asilimia 50 ya mkopo na kuhaidiwa kwamba tutamaliziwa asilimia 50 iliyobaka baada ya miezi sita mara baada ya kuwatumia akaunti zetu
Ø UTUMAJI WA AKAUNTI
Ufunguaji wa akaunti ulikamilika 4 /4/2012 na kutumwa katika wizara ya elimu na bodi ya mikopo.Tangu kutumwa kwa akaunti hizo tulitegemea kwamba pesa zingetumwa mara baada ya wiki mbili lakini mpaka sasa tarehe 4/6 /2012 pesa hazijatumwa na ni takribani miezi miwili
Ø MAISHA TUNAYOISHI
Kutokana na kutokuwa na pesa tunaishi maisha magumu mpaka tunalazimika kukopa kwa kaka zetu na watu wamataifa mengine kwa kiasi tofauti wengine ni euro 500 na kuendelea kuwaahidi kwamba tutawalipa mwezi wa tano mwanzoni na mpaka sasa bado hatujalipa madeni hayo na watu wanatishiwa kupelekwa polisi
Ø MADENI
Watu walilazimika kukopa pesa kwa sababu zifuatazo
v Gharama za chakula
v Gharama za usafiri
v Malazi
v Matibabu
v Stationary
v Mawasiliano
Na vitu vyote hivyo ni ghali sana katika nchi ya Ageria na tunaishi kwa mashaka kwa sababu ya kudaiwa madeni na hatuwezi kukopoa tena kwa sababu hatuaminiwi tena
Ø JITIHADA ZA VIONGOZI
Tangu kutumwa kwa akaunti hakukuwa na taarifa zozote viongozi wa chama cha wanafunzi wanaosoma Algeria (ATSA)Walifanya mawasiliano na viongozi wa bodi ya mikopo na kupewa taarifa zisizo rasmi mpaka mwezi wa tano, na baadae waliahidi kutuma pesa katikati ya mwezi wa tano lakini hazikuweza kutumwa mpaka tarehe 27/5/2012 ,ndipo tulipopata taarifa kwamba pesa zitatumwa tarehe 1 /6/2012 Lakini hazikutumwa mpaka leo hii
Ø MATATIZO
v Watu hatuna pesa na tulizokopa zimeisha
v Tunadaiwa na hatuwezi kukopa tena
v Tunaweza kupelekwa polisi kwa kutolipa madeni
v Kuna wagonjwa na hatuna pesa za kuwaudumia kwa matibabu
v Dada zetu wapo katika mazingira magumu kiasi kwamba wakati wowote wanaweza kufanya maamuzi na mambo tofauti na yaliyowaleta huku
v Tumefikia hatua mpaka ya kuuza mali zetu kwa bei ya HASARA.
v Tuna msongo mkubwa wa mawazo ambao umesababisha kutokuelewa masomo
UTUMAJI WA PESA USIOKAMILIKA.
· 8/10/2011, Bodi ya mikopo ilitupatia pesa kwa mafungu mafungu na kusababisha wengine kuja baada ya mwezi 1.Tuna wasiwasi ya kuwa jambo hili litajirudia tena kwani wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara.mfano 2011 Tumekuja makundi 3 pasipo sababu za msingi.
· Tunaomba uhakika ya kuwa wote tutatumiwa pesa haraka sana.Jumla tupo wanafunzi 56 wa mwaka wa kifaransa nchini ALGERIA.
MADHARA YATAKAYO TUPATA KAMA HATUTOPATA PESA MPAKA 8/6/2012
· TUTAKOSA CHAKULA.
· TUTAKOSA MALAZI.
· TUTAKOSA USAFIRI.
· TUTAKOSA VIFAA VYA KIMASOMO&MITIHANI.
· TUNAWEZA KUPELEKWA POLISI KWA SABABU TUNADAIWA PESA NYINGI NA MUDA TULIOAHIDI KULIPA MADENI HAYO UMESHAPITA ZAIDI YA MWEZI MMOJA.
· TUTAKOSA HUDUMA YA MAWASILIANO.
· HATUTOAMINIWA TENA KWA SABABU HESLB WAMESABABISHA TUVUNJIWE UAMINIFU.
· DADA ZETU KUFANYA KINYUME NA KILICHOWALETA ALGERIA ILI KUPATA PESA.
· WIZI WA MALI ZA WATU WATU ILI KUPATA PESA.
Hayo ni baadhi tuu.Je serekali ilituleta kwa ajili ya hayo?
MAPENDEKEZO YETU
· Vyoombo vya habari mtusaidie kuanzia sasa mpaka tutakapopata pesa zetu haraka sana.
· Vyombo vya habari mtusaidie jambo hili mpaka kufika mwisho.
· Hatuhitaji kudanganjwa na BODI YA MIKOPO kwa sababu kabla hatujaja WALITUNDANGANYA na mpaka sasa wanatudanganya.
· PESA tunataka tutumiwe watu wote 56 na asiwepo hata mmoja wetu atakayecheleweshewa.
· Tunaomba vyombo vya habari vitupatie taarifa za KWELI kila wakati ili tujue&tuwe na nguvu.
Nakala kwa:
Bodi ya mikopo Tanzania
Wizara ya elimu Tanzania
Ofisi ya waziri mkuu Tanzania
MAWASILIANO YETU
Olenjolaimocko@rocketmail.com, Tel +213551867346
khadijaiddi@ymail.com
2 comments:
poleni sana wadogo zetu ...pia napenda kuchukua nafasi hii kuwaweka wazi watanznia wenzagu kuwa wasomi wengi wanakosa uzalendo na nchi yao kutokana na vitu kama hivyo..watoto wapo ugenini kwa ajili ya masomo bodi bado mnaendekeza usanii mpaka kwenye masula nyeti ya elimu kama haya....JE TUTAFIKA JAMANI? bodi ya mikopi inabidi ivunje tu maana wengi hapo wapo kwa manufaa binafsi ya kuzungusha pesa wakati wasomi wanaumia ...
MDAU BELGIUM
Nimetokwa na machozi baada ya kusoma taarifa hii.mie binafsi nimesoma nchini Algeria na nimekutana sana na matatizo haya ya bodi ya mikopo kuchelewesha posho bila sababu maalum miaka yote 5 niliyosoma nchini Algeria.kila mwaka mchezo ni ule ule.mchezo wanaoufanya ni kuzungusha pesa za posho ya wanafunzi kwny Fixed Accounts ktk mabenki ili kupata riba huku wanafunzi wanaostahiki kupata posho wakipata tabu na kudharirika ugenini.kutokana na kucheleweshwa kwa posho mwanafunzi mmoja aitwae Felix alijiua mwaka 2009 baada ya kupatwa na msongo wa mawazo uliosababishwa na kutokuwa na pesa na kuwa na madeni ya kupindukia.Labda hawa "wabinafsi" wanataka kuona mambo yakiharibika zaidi ili warekebishe tabia zao.
POLENI SANA WADOGO ZANGU.DAWA YA HUU UFISADI IPO NJIANI NA MAMBO YATAKWENDA SAWA TU!
Post a Comment