Thursday, June 7, 2012

SAKATA LA WANAFUNZI WA ALGERIA NA BODI YA MIKOPO

Lile sakata la mkopo kati ya bodi ya mikopo na wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioko mjini Constantine nchini Algeria linaendelea kuchukua sura mpya huku mambo yakiwa kitendawili ni lini fedha hizo zitatumwa kwa wanafunzi hao.

Habari kutoka chanzo chetu kilichopo huko nchini Algeria zinasema kuwa wanafunzi hao waliamua kuunda kamati yao ya kushughulikia jambo hili baada ya kuona wanazungushwa na kupigwa kalenda na umoja wa wanafunzi uliopo huko uitwao ATSA.Kamati hiyo ilipewa majukumu ya kupiga simu kwa mkurugenzi mtendaji wa bodi ambaye hakupokea simu hata moja kati ya zile zaidi ya 5 zilizopigwa.

Wakati taarifa zilizopo sasa ni kwamba bodi ya mikopo ilipokea akaunti hizo mnamo tarehe 25/5/2012 lakini kabla ya hapo vijana hao walishatumiwa e-mail na uongozi huo wakitaarifiwa juu ya akaunti zao kupokelewa bodi ya mkopo.E-mail hiyo ambayo pia ilitumwa kwa wanafunzi wote walioko nchini huko. Chanzo chetu kilitufowadia e-mail hiyo na tukakopi baadhi ya maandishi ya e-mail hiyo ambayo inasadikiwa kutumwa na waziri mkuu wa chama hiko ambaye tusingependa kumtaja jina :
   
KWA WANAFUNZI WAPYA – CONSTANTINE
Uongozi unawajulisha kuwa tayari umeshatuma Akaunti zenu BODI ya mikopo tayari kwa kupatiwa nusu ya mkopo wenu iliyobaki. Bodi ya Mikopo bado hawajasema ni lini watatuma kiasi hicho kilichobaki,lakini wamekiri kupokea Akaunti hizo na sasa wanashughulikia suala hilo. Tutakapopata taarifa yeyote mpya basi
tutawafikishia,tunawaomba muwe na subira na uvumilivu.

Tunawatakia Kila la Heri na Masomo Mema

UONGOZI,ATSA


Lakini cha ajabu viongozi hao wakaendelea kuzungusha mambo huku wakitoa taarifa zinazopingana,huku wakisema bodi wamesema hivi mara wamesema hivyo huku siku zikikatika na hali za vijana hao zikizidi kuwa mbaya katika nchi hiyo ya ugenini.

Baada ya kuvumilia muda mrefu ndipo vijana hao walipoamua kuitana pamoja na kufanya kikao katika ukumbi wa chuo,na tumefanikiwa kupata video ya minutes za kikao hiko kutoka kwa chanzo chetu ambacho pia kilidai kuwa kuna mbinu za chinichini za kubadilisha report ya kikao ili viongozi wajisafishe wao wenyewe.Katika maamuzi yaliyofikiwa katika kikao hicho ni kuwapigia simu bodi wenyewe,kuteua kamati ya kushughulikia jambo hilo na kupeleka habari hizi katika mass media za Tanzania itakapobidi.

Lakini viongozi wa chama hicho cha ATSA ambacho chanzo chetu kilidai ingekuwa vizuri kama kingeitwa ATAMSA,walijaribu kuingilia kati na kulizuia jambo hilo na kujaribu kujifanya wako in control kwa jambo ambalo lilishawashinda na kubakia kudanganya.Chama hicho cha ATSA au ATAMSA ambacho kinaongozwa na Rais ambaye jina lake tunalo,kimeshutumiwa kuwa na elements za udini nyingi sana na ambapo waumini wa dini fulani ambayo tusingependa kuitaja wamekuwa wakichagua viongozi kwa kufata dini,unazi na ushabiki ambao mwisho wake umeweka madarakani viongozi wabaya ambao hawajui ni nini wakifanyacho,viongozi ambao wanapoulizwa maswali huishia kupaniki na kutumia jazba kuwajibu raia wao.Chanzo chetu pia kilidai kuwa katika kikao kimoja cha wanafunzi walioko katika mji huo wa Constantine,waziri mkuu wa chama hicho almanusra amwage machozi baada ya mmoja wa wanafunzi hao kuweka wazi kuwa kulikuwa na mpango wa chinichini wa kuwakopesha baadhi ya wanafunzi hao kufuatana na imani zao za kidini.

Pia kumekuwepo na taarifa za kwamba waumini wa dini hiyo wamekuwa na tabia ya kufanya vikao vyao vya kidini siku moja kabla ya uchaguzi mkuu ili kupanga matokeo na kuhujumu uchaguzi huo;pia wamekuwa na tabia ya kuingilia na kutoa vitisho pale kunapokuwa na mahusiano ya muumini wao na wa dini nyingine kinyume kabisa na tamaduni za Tanzania huru.Chanzo chetu hicho ambacho ni mmoja wa waumini wa dini hiyo wasiokubaliana na mambo yanayofanywa na wenzao kimedai kitaendelea kutujuza mambo nyeti kabisa na sisi tukiyaanika mpaka yatakapokoma.

Uongozi huo ambao pia unabeba lawama sawasawa na bodi ya mkopo kama si zote,kwa kuchelewesha mambo ya wanafunzi na kutumia uongo na siasa ili kujiokoa wenyewe pale wanapoona mambo yamezidi unga.Na ikumbukwe kwamba vijana hawa sio wa kulaumiwa kwa kufanya yote haya kwa kuwa katika kikao kilichofanyika mnamo tarehe 19/5/2012 huko mjini Constantine,waziri mkuu aliwapa ruhusa vijana kufanya jambo lolote wanaloweza ikiwa wataona hela zimechelewa kutumwa,jambo amabalo linaashiria kuwa uongozi umeshawashinda.

Pia imedhihirika kuwa hali ni mbaya sana kwa wanafunzi hao kiasi kwamba hata ikitokea mmoja wao akaumwa haijulikani atasaidiwaje,maana wamekopa sana na hela zimeisha na haijulikani wanaishije mpaka sasa,na sasa vyuo vingi viko mbioni kufungwa nchini humo na viza zao haziruhusu kufanya kazi sasa kabla hawajaanza kufanya mambo kinyume na yaliyowapeleka ni vizuri bodi ya mkopo ikalifikiria suala hili na kuwaharakishia pesa zao.

Na tuna imani huenda bodi ya mkopo ikawa wameshapata taarifa hizi,na wakae wakifahamu kuwa vijana wanachohitaji ni fedha na sio siasa zingine.Kwani kwa mujibu wa uongozi wao akaunti zilishafika bodi na kupokelewa mnamo tangu tarehe 15/4/2012 kwahiyo vijana wanaona wameshangojea muda wa kutosha tu.

Tutaendelea kuwajulisha mambo yote yanayoendelea kujiri huko nchini Algeria mpaka pale bodi watakapotuma hizo fedha,hatutaacha kitu,mambo yote tutayaweka wazi pale yatakapozidi hasa hili suala la udini na chanzo chetu kimeahidi kututumia majina zaidi ya magamba wa tabia hii chafu ambayo Baba Wa Taifa aliikemea akijua itakuja kuleta maovu.

1 comment:

DAVID KAFULILA said...

DU...!!!! aiseee..! poleni sana ndugu zangu na wadogo zangu kwa haya matatizo yanayowasibu.
Nawapongeza kwa kushikamana na kutatua hili tatizo linalowakumba hususani katika uongozi. Pia nasikitika sana kuona bodi ya mikopo inaleta usanii hata kwa wanafunzi mnaosoma nje.

Jitahidini mshirikiane na muishi kama ndugu bila kujali itikadi za dini kwani mwisho wa siku kumbukeni mnatuwakilisha watanzania wote na baadae mnaweza kuwa viongozi wakubwa, hivyo kwa mantiki hiyo nawaasa kushirikiana.