Wednesday, May 9, 2012

Dkt. Mwinyi ahahidi ushirikiano kwa wauguzi

DSC04377.JPG
Mh. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi aliyeshika kiti akitembelea mabanda ya maonyesho ya wauguzi.Kushoto kwakwe ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Joseph Kuzilwa.
DSC04391.JPG
Mh. Waziri pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wakisalimiana na Viongozi wa TANNA Muhimbili kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa CPL
DSC04395.JPG
Sehemu tu ya Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ndani ya ukumbi wa CPL wakisimama kumkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
DSC04408.JPG
Mh. Waziri akizungumza na Wauguzi kama wanavyomsikiliza katika picha inayofuata hapo chini
DSC04399.JPG

DSC04405.JPG
Mkurugenzi Mtendaji Wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akitoa neon la shukrani kwa Mh. Waziri
DSC04415.JPG
Mwenyekiti wa TANNA Tawi la Muhimbili Bw. Paul Magesa pamoja na Prof. Kuzilwa wakitoa zawadi ya pongezi kwa Mh. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi kuteuliwa kushika wadhifa huo
DSC04411.JPG
Muuguzi Teddy Kulwa akipokea nishati ya mchango alioutoa katika taaluma ya Uuguzi
DSC04410.JPG
Muuguzi Dkt. Scolastica Ndonde akipokea nishati ya mchango alioutoa katika taaluma ya Uuguzi
DSC04409.JPG
Bw. Lugina akipokea nishati kwa niaba ya Marehemu Mke wake Prof. Hellen Lugina katika kutambua mchango wake alioutoa kwenye taaluma ya uuguzi
DSC04413.JPG
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela akipokea zawadi ya TANNA kama ishara pongezi na shukrani kwa ushirikiano alioutoa kwa Wauguzi toka aliposhika wadhifa huo Novemba 2011.
DSC04416.JPG
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akipokea zawadi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kutoka kwa Mwenyekiti wa TANNA tawi la Muhimbili Bw. Magesa pamoja na Prof. Kuzilwa kama zawadi ya pongezi kuteuliwa kushika wadhifa huo.
DSC04419.JPG
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Sr. Agnes Mtawa akitoa neon la shukrani kwa Mgeni rasmi kukubali kufungua Kongamano la Wauguzi siku mbili baada ya kuingia Ofisini
DSC04420.JPG
Mh. Waziri akiwa katika picha ya pamoja: Kulia kwake ni: Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, akifuatiwa na Mganga Mkuu Mstaafu Dkt. Upunda.Kushoto kwake: Prof. Joseph Kuzilwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini akifuatiwa na Dkt. Marina Njelekela Mkrugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili
DSC04425.JPG
Mh. Waziri akiwa na baadhi ya Wauguzi waliotunukiwa nishati na baadhi ya Viongozi wa TANNA Muhimbili
DSC04428.JPG
 Mh. Waziri akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na Mkurungezi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela
DSC04430.JPG
Mh. Waziri akizungumza na Wanahabari

Siku mbili tu baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dkt.Hussein Mwinyi kuingia ofisini, amehahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa wauguzi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kiutendaji.

Hayo aliyasema leo wakati akizindua Kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wauguzi Tanzania Tawi la Muhimbili ambao wataungana na Wauguzi wote duniani kuadhimisha siku ya Wauguzi Duniani inayotarajiwa kufanyika Mei 12, 2012.

Dtk. Mwinyi alisema nafasi ya wauguzi katika sekta ya afya ina umuhimu wa pekee kwani muda mwingi wao ndio wanaokaa na wagonjwa hivyo kazi yao ni kubwa na wanastahili kupongezwa kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Aidha alisema ofisi yake itakuwa wazi na inakaribisha majadiliano na wauguzi katika kutafuta ufumbuzi kwa pamoja na mapema wa changamoto zinazowakabili wauguzi badala ya kusubiri mihadhara kama hii kusema changamoto zao.

Aliwashuruku Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jinsi walivyotoa huduma bila kuchoka katika kipindi cha migomo iliyojitokeza hivi karibuni. Aliwasifu na kuomba jamii itambue mchango wao mkubwa walioutoa katika kuhudumia wagonjwa.

Chama cha Wuguzi Tanzania (TANNA) Tawi la Muhimbili kimeandaa maonyesho ya huduma wanazotoa ambayo yanafanyika ndani ya Hospitali na kutoa huduma za kupima sukari, shinikizo la damu, maambukizi ya UKIMWI, usikivu, ushauri nasaha pamoja na kuhamasisha wananchi kujitolea damu. Maonyesho haya yanaendana sambamba na kongamano la kisayansi la wauguzi linalofanyika ndani ya Hospitali ambapo wadau na wauguzi toka Hospitali za nje ya Jiji la Dar Es Salaam wameshiriki.

Wakati huo huo TANNA Muhimbili imempa zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela kwa kutoa ushirikiano wa karibu sana kwa wauguzi katika kipindi cha miezi sita aliyoshika nafasi hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Sr. Agnes Mtawa alisema Mkt. Njelekela ameonyesha upendo na ushirikiano mkubwa kwa wauguzi na kila mara amekuwa akitoa muda wake mwingi kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

No comments: