Makamu wa Balozi wa Brazil nchini Mhe. Ronaldo Vieira akiwakaribisha wageni katika Maonyesho ya Mchezo wa Kapoeira yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Utamaduni wa Russia.
Mhe. Ronaldo amesema kwa mara ya Kwanza mchezo wa Kapoeira ulizinduliwa nchini Tanzania Mwezi June mwaka jana na kwa jijini Dar es Salaam mafunzo ya mchezo huo yanafanyika katika kituo cha Fitness Centre Msasani jijini Dar es Salaam na kuwakaribisha Wakazi wote wa jijini kuhudhuria mafunzo ya Mchezo huo.
Kulia ni Balozi wa Russia nchini Mhe. Alexandr A. RANNIKH naye alikuwa ni miongoni mwa wapenzi wa mchezo huo.
Wadau wakifuatilia kwa umakini Historia ya mchezo huo kutoka kwa Mestra Janja.
Mwalimu wa Mchezo wa Kapoeira ambao ni utambulisho halali wa Utaifa wa Brazil Mestra Janja akizungumzia umuhimu na faida za mchezo huo kwa wageni waliohudhuria Onyesho la mchezo huo katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kapoelista Gabriel Limaverde ambaye alikuwa akitafsiri Ujumbe huo kwa Lugha ya Kingereza.
Makapoelista wakimsiliza Mwalimu wao.
Wadau wakifuatilia kwa umakini.
Wadau wakifuatilia
Msanii Karola Kinasha naye alikuwepo.
Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa.
Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa.
Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa.
Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa.
Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa.
Mchezo wa Kapoeira unavyochezwa.
Makamu wa Balozi wa Brazil nchini Mhe. Ronaldo Vieira katika picha ya pamoja na Mwalimu Janja pamoja na Makapoelista.
Afisa Ubalozi Lucy akiwa na rafiki.
1 comment:
Asanteni kwa wote waliohudhuria! Karibuni kujifunza kapoeira hapa Dar: tupelekee barua pepe kwa capoeiradar@gmail.com. Madarasa yapo mara mbili kwa wiki kule Msasani.
Linda Lönnqvist, mwalimu wa kapoeira
Post a Comment