Friday, November 30, 2018

Washiriki Master Tanzania kutambulishwa Forty Forty Tabata leo

WASHIRIKI wa Shindano la Master Tanzania 2018/19, wanatarajiwa kutambulishwa leo Forty Forty Club, iliyopo Tabata Bima, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mratibu wa shindano hilo, Michael Maurus, alisema kuwa utambulisho huo ni sehemu ya maandalizi ya shoo ‘bab kubwa’ ya mchujo itakayofanyika wikiendi ya pili ya mwezi huu katika ukumbi utakaotangazwa.

Alisema kuwa jumla ya washiriki 30 watakuwapo Forty Forty leo ambapo watapata nafasi ya kujitambulisha mbele ya wadau wa sanaa ya uanamitindo na burudani kwa ujumla.“Tunaushukuru uongozi wa Forty Forty kwa kutupa nafasi hii, wadau wa burudani waje kwa wingi kuwaona vijana wanatashati watakaoshiriki shindano letu ambalo fainali zake zitafanyika Februari mwakani kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam,” alisema Maurus.

Maurus alisema kabla ya fainali za shindano hilo, kutakuwa na hatua ya robo na nusu fainali ambapo lengo lao ni kuwa na washiriki wa awali 50.

“Lengo letu ni kuwa na washiriki 50 na kesho (leo) ni siku ya mwisho kwa vijana wanaopenda kushiriki mashindano hayo kujiandikisha, baada ya hapo watalazimika kulipia fomu. Hivyo kwa wanaopenda kushiriki, waje pale Forty Forty kuanzia saa 2:00 usiku wachukue fomu, wazijaze na kuzirejesha hapo hapo,” alisisitiza Maurus.

Juu ya zawadi za shindano hilo, Maurus alisema hadi sasa wamna uhakika wa mwaliko wa washindi watano kwa kwanza kwenda Marekani kutembelea maeneo mbalimbali maarufu ya Hollywood, yakiwamo yale yaliyochezewa sinema zilizowahi kutamba, ikiwamo ya Coming To America iliyochezwa na wakali kadhaa, akiwamo Eddie Murphy.

Maurus alisema kuwa pia kutakuwa na zawadi nyinginezo za fedha, huku akisisitiza wameomba wenyeji wao mabosi wa Hollywood kuongeza idadi ya waalikwa ili waweze kupeleka huko washiriki 10 na waandishi wa habari watakaoripoti zaidi shindano lao.

Shindano la Master Tanzania lilizinduliwa kwa mara ya kwanza Machi mwaka huu, likiratibiwa na Kampuni ya Kiafrika Zaidi chini ya Rais wake, Mtanzania Winny Casey anayefanya shughuli zake Marekani ambaye pia ni Balozi wa Hollywood hapa nchini.
Baadhi ya washiriki Master Tanzania 201819

Mojabet yatangaza kudhamini fainali za Bongo Star Search

KAMPUNI ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha kupitia mmoja ya michezo yake ya Boompesa leo imetangaza kudhamini fainali za Bongo Star Search (BSS) ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakutangaza kudhamini Bongo Star Search msimu wa 9, Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni ya Mojabet Diana Chacha alisema kuwa wameona ni muhimu kushirikiana na Bongo Star Search ili kuendelea kuimbua vipaji vipya vya muziki hapa nchini na pia kufanya vijana zaidi waweze kujiajiri kupitia muziki.

Sisi lengo ni kuwafanya Watanzania wengi waweze kujiajiri kupitia zawadi za fedha taslimu ambazo huwa tunawapa washindi wetu. Kwa maana hiyo tumeona ni muhimu kutanua wingu wetu na kuelekeza kwenye muziki kwani huko pia kuna vipaji vyingi lakini kutokana na kutopata nafasi ya kuonekana, tunaamini kuwa ushirikiano wetu na BSS utaweza kutanua wingu na kufikia Watanzania wengi na hasa kupitia vijana kupitia Boompesa, alisema Chacha.

Chacha aliongeza kuwa Boompesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea.

Mojabet ni kampuni ya michezo ya Bahati na sibu na Boompesa ni mmoja ya michezo yetu.Mojabet kupitia Boompesa ni wadhamini wakuu katika Bss season 9.na nusu fainali na fainali Boompesa imeandaa zawadi nono na sio kwa washiriki wa bss tu Bali hata kwa wachezaji wa mchezo huo kwa kupitia code ya Bss.kwani kuna TZS 50 milioni imeandaliwa kwa wachezaji.hivyo ni fursa kwa kila MTU kucheza zaidi ili kujiongezea nafasi take ya kushinda.

Kwa upande wake, Mratibu na Jaji Mkuu wa Bongo Star Search Rita Paulsen alisema kuwa fainali za mwaka huu zimekutakuwa tofauti na za miaka iliyopita kwani mshindi mbali na kujipatia fedha taslimu lakini pia ataweza kupata ajira kutoka kwa kampuni ya Mojabet

Mojabet kupitia Boompesa wamefanya fainali za mwaka huu ziwe za kipekee, alisema Rita huku akiongeza kuwa mshindi wa BSS msimu wa tisa atapata fedha taslimu milioni tano, vile vile atakuwa Balozi wa Boompesa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo atakuwa analipwa shilingi milioni mbili kwa mwezi.

Tumeingia mkataba wa mwaka na kampuni kubwa ya muziki ambayo itakuwa ikizalishalisha na kusambaza kazi za mshindi wa mwaka huu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Lengo ni kuhakikisha mshindi wetu anakuwa ni staa kweli, alisema Rita huku akitoa shukrani kwa kampuni ya Mojabet kupitia Boompesa kuweza kudhamini mashindano yam waka huu ambayo yamekuwa tofauti na ya miaka ya nyuma.

Vile Vile, Rita aliongeza kuwa wakati wa kilele cha fainali hizo kutachezeshwa mchezo wa Boompesa ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni hamsini.

Jaji Mkuu wa shindano ya Bongo Star Search (BSS) Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza zawadi na fainali za BSS msimu wa 9 ambapo mshindi atapata zawadi ya fedha taslimu TZS5M pamoja na mkataba wa mwaka mmoja kutoka kwa wadhamini wakuu ambao kampuni ya Mojabet inayojishughulisha na mchezo kupitia Boompesa. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Mojabet Diacha Chacha.

BILIONI 4 KULIPWA KILA SIKU KWA WAKULIMA WA KOROSHO-MHE HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima. (Picha Zote Na Mathias Canl, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari tarehe 29 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.






Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Serikali imetangaza kuongeza kasi ya malipo ya wakulima wa Korosho ili kufikia kiasi cha shilingi Bilioni nne (4) kila siku kwani kufanya hivyo zoezi la malipo kukamilika haraka.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 29 Novemba 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Bodi ya Korosho Mjini Mtwara ili kutoa tathmini ya hatua zilizofikiwa na serikali za ununuzi wa korosho za wakulima.

Amesema kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na kuongezwa kwa wataalamu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya malipo huku akisisitiza kuwa wataalamu wengine tayari wamekuwa na uzoefu wa namna ya kuhakiki na namna ya kulipa tangu kuanza kwa zoezi hilo.

Mhe Hasunga alisema kuwa mikoa inayolima korosho ni mingi nchini hivyo wakati tathmini sambamba na malipo zikiendelea timu ya wataalamu wengine itaundwa kwa ajili ya kuanza kufanya tathmini katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine inayolima korosho nchini.

Katika hatua nyingine amesema kuwa serikali imejipanga kuwatambua wakulima wote wa korosho nchini ili kurahisisha kuwahudumia na kuainisha tathimini mahususi ya wakulima hao nchini.Kuwafahamu wakulima hao itaisaidia serikali namna ya kushirikiana nao na kuwasaidia ili wakulima hao waweze kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.

Miongoni mwa changamoto ilizokutana nazo serikali katika zoezi la uhakiki ni pamoja na kutotolewa takwimu sahihi na Vyama vya msingi vya ushirika za wakulima wa korosho kwani takwimu hizo zinatofautiana na vyama vikuu vya ushirika.“Jambo hili la takwimu kwenda kinyume linatupa uhakika kwamba kuna taarifa zilikuwa zinapikwa ili kumnyonya mkulima lakini changamoto zingine ambazo zimetukumba ni pamoja na uchache wa maghala kwani yaliyopo hayatoshi” Alikaririwa Mhe Hasunga

“Kuna changamoto za mgomo wa wapakuaji na wapakiaji wa mizigo, nasi kama serikali tutakuwa na kikao hivi karibuni na wasafirishaji ili kuhakikisha kuwa wanalipwa fedha zao haraka iwezekanavyo baada ya kupitia mikataba yao kujiridhisha jinsi walivyokubaliana” Alisema

Tayari vyama 163 vya wakulima wa korosho vimekwisha hakikiwa mpaka kufikia jana jioni tarehe 28 Novemba 2018 kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na zao la korosho nchini.Katika vyama hivyo vilivyohakikiwa tayari malipo yamevifikia vyama 97 ambapo wakulima 22,269 wameshalipwa huku kiasi cha korosho ambazo zimekwishalipiwa ni kilo 6,712,681 huku jumla ya Bilioni 22,151,00,000.8 zikiwa zimekwishalipwa.

Aidha, mpaka kufikia jana jioni tarehe 29 Novemba 2018 serikali imekwisha hamisha kiasi cha Tani 9,347.2 kutoka kwenye maghala makuu.Pia Waziri Hasunga ameyataja matarajio ya serikali katika uzalishaji wa Korosho kuwa ni takribani Tani 245,495.8

SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.

Hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wachimbaji wadogo wadogo wajiunge katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe.Amewahamasisha wachimbaji hao watumie taasisi mbalimbali za kifedha na kukopa fedha na kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa lengo la kujiongozea tija.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati ya kumaliza tatizo la maji nchini kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani.

Waziri Mkuu amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wananchi katika maeneo yote wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.“Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo na wa wilaya ya Mbogwe wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao.”

Kuhusua suala la wanafunzi kukatishwa masomo kwa kupata ujauzito wilayani Mbogwe, Waziri Mkuu ameitaka jamii kukemea vitendo hivyo. Wanafunzi 54 wamepata ujauzito.Amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu wanafunzi 20 wa shule za msingi na 34 wa sekondari wameacha shule baada ya kupata ujauzito.

“Hali ni mbaya, Mbogwe inatia aibu kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto waliopewa ujauzito. Naagiza msiwaguse wanafunzi wa kike ni moto utawaunguza. Tukikukamata jela miaka 30.”Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema wilaya ya Mbogwe inafanya vizuri katika sekta ya madini, ambapo ina viwanda 27 vya kuchenjulia dhahabu.

Amesema katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wadogo wanawezeshwa kufanya shughuli zao vizuri, Serikali imetenga eneo la hekta 547.64 kwa ajili ya kuwagawia wachimbaji hao.Akizungumzia kuhusu leseni za uchimbaji mkoani Geita amesema kuna jumla ya leseni 971 za uchimbaji mdogo wa madini na kati yake zinazofanyakazi ni leseni 184 tu.

Waziri huyo amewataka wachimbaji wadogo wadogo waendelee na shughuli zao za uchimbaji kwenye maeneo yao waliyopangiwa na kwamba hakuna atakayewaondoa.

Awali, Waziri Mkuu alikagua na kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbogwe katika kijiji cha Kasosobe. Ujenzi huo utagharimu sh. bilioni 4.3. Pia alikagua mradi wa uboreshaji miundombinu na kuzindua maabara ya Kituo cha Afya Masumbwe.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, NOVEMBA 29, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. 
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. 
Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoingia kwenye Kiwanja cha Shule ya Misngi ya Masumbwe wilayani Mbogwe kuhutubia Mkutano wa Hadhara, Novemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI LUGOLA AWATAKA MAJAMBAZI WAJISALIMISHE PAMOJA NA SILAHA ZAO, POLISI HAWATALALA MPAKA JAMBAZI WA MWISHO AMETIWA MBARONI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka majambazi popote walipo nchini kujisalimisha pamoja na silaha zao wakati Polisi wakiendelea na msako mkali mpaka jambazi wa mwisho anatiwa mbaroni. Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara na litawasaka majambazi hao usiku na mchana popote walipo na litahakikisha nchi inaendelea kuwa salama na wananchi wema wakiendelea kufanya shughuli zao za maendeleo kwa kulijenga Taifa.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, leo, Lugola amesema usalama wa nchi hauchezewi na mtu yeyote na watu wasijaribu kutikisa kiberiti kwa kulichezea Jeshi la Polisi. Lugola amesititiza kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inaongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ujambazi hauna nafasi na pia amewataka majambazi hao wafanye kazi nyingine ya kuwaingizia kipato kwa njia halali.

“Msijaribu kukitikisa kiberiti, Serikali ipo macho muda wote, Jeshi lenu lipo imara, majambazi wanaofanya uvamizi, tutahakikisha tunawasaka popote walipo jambazi mmoja baada ya mwingine, hatutalala wala kupumzika hadi jeshi letu litakapomtia mbaroni jambazi wa mwisho,” alisema Lugola. Kutokana na msako huo, Lugola alisema majambazi hao wajisalimishe wenyewe pamoja na dhana zao kwenye kituo cha polisi wanachoona kipo jirani na wao, vinginevyo hawatasalimika na hawatabaki salama.

“Kama kuna ndugu zetu, watoto wetu, majirani zetu tuwaambie serikali hii ya magufuli nafasi hiyo ya kufanya ujambazi haipo, nimepata taarifa za uhalifu, wizi wa mifugo na uvamizi wa aina mbalimbali, tuone taarifa polisi ili tuweze kuwatia mbaroni majambazi hao kwa wale wote ambao mnahisi wanajihusisha na uhalifu, toeni ushirikiano bila woga ili meneo yetu yazidi kuwa na amani,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Lugola alisema ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake ambavyo anavisimamia wapo baadhi ya askari wachache ambao wanajihusiha na vitendo vya rushwa na alishatoa onyo mara nyingi, hivyo atakao wakamata hatawaonea huruma. 
 

“Kuna baadhi ya mazingira ambayo yanachangia rushwa zaidi ndani ya Jeshi la Polisi ikiwemo kutokutolewa kwa dhamana katika siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili, baada ya kuona kunamianya ya rushwa nikatangaza nchi nzima vituo vyote vya polisi vitoe dhamana saa 24 na siku 365 na robo, pia kutowekwa mahabusu watuhumiwa ambao wanamakosa madogo madogo,” alisema Lugola.

Lugola anaendelea na ziara jimboni kwake ya kuhamasisha wananchi kuanza maandalizi ya kilimo pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo huku wakiendelea kuheshimu sheria za nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akiwapelekea zawadi kikundi cha kwaya ya Kijiji cha Kasahunga, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, wakati waimbaji hjao walipokua wanampokea kwa kijijini hapo. Lugola katika hotuba yake kwa wananchi zaidi ya 100 waliohudhuria mkutano huo, aliwataka wananchi wa Mwibara washirikiane na polisi kuwafichua majambazi, na pia aliwataka majambazi wajisalimishe pamoja na silaha zao katika kituo chochote cha polisi nchini, kwa kuwa polisi usiku na mchana wanawasaka na watahakikisha wanamtia mbaroni jambazi wa mwisho.

NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia na kuchunguza thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati ya bandari ya Lindi ili kuweza kubaini kama gharama iliyotumika inaendana na ujenzi uliofanyika
 
Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi mkoani humo ambapo amebaini kuwa kasi ya utendaji kazi kwenye gati hilo hairidhishi na kuongeza kuwa kazi ni ya mwaka mmoja ila imechukua miaka mitatu hadi sasa na bado haijakamilika. “Naielekeza TAKUKURU waje wafuatilie thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati hili,” amesema Nditiye. 

Nditiye amesema kuwa kwa bahati mbaya miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inayotekelezwa nje ya bandari ya Dar es Salaam haitekelezwi ipasavyo, tufike mahala tuheshimu fedha za Serikali na za wananchi. “Kwa bahati mbaya TPA hamfiki eneo la mradi wakati wa kuandaa nyaraka na hata ujenzi wa miradi husika inavyoendelea hivyo tunaingia hasara,”amesema Nditiye .

Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara Twaha Msita wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo kwa Nditiye amesema kuwa Kampuni ya Comfix & Engineering Ltd ilipewa kazi na TPA ya kujenga gati hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Mei mwaka 2015 na kutakiwa kukamilika mwezi Mei mwaka 2016 kuendana na mkataba husika kwa gharama ya shilingi bilioni 3.1 ambapo baada ya muda ilionekana kazi zimeongeza na hivyo kuongezewa fedha hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 .

Nditiye amesema kuwa tayari mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 2.448 na kazi hiyo ilisimama kwa kipindi cha mwaka mzima mwaka 2017 na kuanza tena ambapo hadi sasa haijakamilika na imechukua kipindi cha miaka mitatu tofauti na mkataba wa awali ambapo ilitakiwa ijengwe kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Serikali hatuwezi kuvumilia jambo hili kwa kuwa tunawatesa wananchi kwa kukosa huduma na kutumia vibaya fedha za Serikali,” amesema Nditiye
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amesema kuwa bandari ya Lindi ni muhimu sana kwa uchumi wa watu wa Lindi kwa kuwa tuna korosho na kiwanda cha Jeshi cha kubangulia korosho. Amekiri kuwa kazi hairidhishi na kuna tatizo la kujaa kwa mchanga hivyo tuombe wahusika wakamilishe ili bandari hii iweze kutoa huduma kwa wananchi .

Katika hatua nyingine, Nditiye ametoa rai kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango kuwachukulia hatua watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wa Mkoa wa Lindi wanaosimamia Bandari ya Lindi kwa kuikosesha Serikali mapato kwa kuwasaidia wafanyabiashara kukwepa kodi na kuvusha biashara za magendo. “Wafanyakazi wa TRA waliopo bandari ya Lindi wameoza, Waziri wa Fedha na Mipango tafadhali safisha uozo huo kwa kuwa wamepitisha madumu ya mafuta 650 mwezi huu Novemba yaliyopakiwa Zanzibar na kushushwa Lindi yakiwa madumu 30 tu na kusema kuwa yako tupu,” amesema Nditiye. Pia, amefafanua kuwa alimuagiza Mkuu wa Wilaya awaite ila wamedharau na hawakufika kwenye kikao na ziara yake mkoani humo. 

Vile vile, amemuelekeza Mkuu wa Wilaya hiyo kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilayani humo kudhibiti bandari bubu zilizopo na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wasio waaminifu wanaokwepa kodi, hivyo kuikosesha Serikali mapato kwa kufanya biashara za magendo kwa kutumia bandari bubu na kushusha mizigo na bidhaa zao kwenye pori lililopo karibu na eneo la Uwanja wa Ndege wa Lindi ambapo unaweza kuhatarisha usalama wa uwanja huo
Nditiye pia amekagua uwanja wa ndege wa Mkoa wa Lindi na kuwaeleza kuwa uwanja huo umewekwa kwenye viwanja 11 na Serikali ambavyo vimepangwa kukarabatiwa na kuendelezwa na kiwanja hicho kimetengewa shilingi bilioni 2.95 na Serikali katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 za kuwezesha kuanza kwa ukarabati huo .

Vile vile, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Nyamisati iliyopo Kibiti mkoani Lindi inayowawezesha wananchi kusafiri kwenda Mafia ambapo ujenzi huo ni pamoja na majengo ya ofisi, sehemu ya kupumzika abiria na vyoo na kubaini kuwa ujenzi huo unaendelea vizuri ambapo unagharimu shilingi bilioni 14.4 ambao ni wa kipindi cha mwaka mmoja ambao ulionza mwezi Machi 2018 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2019. 


Meneja Mradi huo wa TPA, Mhandisi Erick Madinda amemueleza Nditiye kuwa mradi wa ujenzi huo unagharamiwa na TPA na tayari mkandarasi Alpha Logisitics Tanzania Ltd & Southern Engineering Company Ltd ameshalipwa shilingi bilioni 2.4 kati ya shilingi bilioni 14.4 ambazo ni gharama za ujenzi atakazotakiwa kulipwa mara kazi itakapokamilika.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara, Twaha Msita (hayupo pichani) kuhusu kutoridhishwa na ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hiyo mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa fulana ya bluu) akikagua ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi unaosuasua wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Nyamisati wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo Kibiti, Lindi. Meneja Mradi wa TPA Mhandisi Erick Madinda akitoa maelezo

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 30,2018














DKT. NDUGULILE ASIKITISHWA NA UTENDAJI KAZI SEKTA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII TANGA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Lushoto wakati wa ziara yake mkoani Tanga kufuatilia utekelezaji wa utoaji huduma katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mmoja wa mtoto anayeishi katika makao ya kululelea watoto yatima na wenye shida ya Irente yaliyopo Lushoto mkoani Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwa amembeba mmoja wa mtoto anayeishi katika makao ya kululelea watoto yatima na wenye shida ya Irente yaliyopo Lushoto mkoani Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesikitishwa na utendaji kazi usioridhisha katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii kwa mkoa wa Tanga kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao 

Ameyasema hayo leo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga alipofanya ziara ya kujionea shughuli zinazosimamiwa na Wizara yake katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii na kukuta baadhi ya maafisa wahusika wakiwemo Waganga Wakuu wa Wilaya na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Lushoto hawapo katika ziara yake.. 

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Lushoto amesema kuwa watendaji wa Wilaya hiyo hawako makini katika kutekeleza majukumu yao na hakuna usimamizi wa moja kwa moja katika kuhakikisha mambo yanaenda wilayani hapo. 

“Nimesikiliza taarifa sijaona masuala ya Maendeleo ya Jamii na pia Afisa Maendeleo ya Jamii hayupo hapa na nimetembeela na Wilaya nyingine Waganga Wakuu wa Wilaya hawakuwepo hii inaonesha hamko makini katika kazi yenu” alisisitiza Dkt. Ndugulile 

Dkt Ndugulile amesema usimamizi na uwajibikaji ni njia pekee itakayowezesha kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu katika Sekta zilizopo na hapo baadae itabidi kila awajibike katika ngazi yake ya uteuzi iwapo hatashindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo. 

Ametolea mfano katika taarifa ya Wilaya iliyosomwa kwake kuwa kuna baadhi ya vituo vya afya vilivyopokea hela ya ujenzi na ukatarabati wa vituo hivyo havijakamilika na vingine kutokuwa na milango ikiwa Wilaya ya Lushoto ni wazalishaji wa mbao na kusema kuwa taarifa aliyopokea imeegemea katika Sekta ya Afya na kusahau Sekta ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasimamia masuala muhimu ikiwemo mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni. 

Naibu Waziri Ndugulile ameupa uongozi wa Wilaya ya Lushoto mwezi mmoja kukamilisha kuweka milango katika majengo yote yaliyopo katika vituo vya Afya vilivyopokea fedha ya ujenzi na ukarabati jumla ya Shillingi Billioni 1.4. 

Aidha Dkt. Ndugulile ameagiza kufanyika kwa marekebisho kasoro ndogo ndogo za kitaalam katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma bora kwa wananchi wa Wilaya hiyo. 

Akitoa maombi kwa niaba ya wananchi wa Lushoto mbele ya Naibu Waziri Ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mhe. Shaban Shekilindi ameomba kupatiwa gari ya kubeba wagonjwa vifaa vya X Ray pamoja na kuogezewa watumishi ili kuendana na kasi ya utoaji wa huduma za afya katika Wilaya ya Lushoto. 

Naibu Waziri Ndugulile amemaliza ziara yake ya Kikazi ya Siku kadhaa katika Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga katika kufuatilia utendaji kazi katika Sekta ya Afya na Maendelo ya Jamii.

Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya Katika Utumishi wa Umma










Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma.Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma. 
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma. 
Sehemu ya washiriki wa wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma. 
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.kulia ni Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD).

Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Chadhamiria Kuwajengea Uwezo waajiriwa wapya Serikalini wa Kada ya Sheria ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt . Laurean Ndumbaro wakati akifungua Kongamano la Wadau lililolenga kupitia na kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa mawakili na wanasheria wa sekta ya umma, Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Mick Kiliba amesema kuwa lengo ni kuwajengeauwezo wanasheria hao ili waweze kujua mifumo ya uendeshaji wa shughuli za Serikali, Uongozi na Utumishi wa Umma.

“Lengo la kuwaandaa waajiriwa wapya wa Kada ya Sheria ni kujenga utumishi uliotukuka na bora katika Kada hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu”; Alisisitiza Kiriba.Akifafanua Bw. Kiliba amesema kuwa waraka namba (5) Tano wa mwaka 2011 wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, unaoelekeza kutolewa kwa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya katika Utumishi wa Umma.

Aliongeza kuwa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kimekasimiwa madaraka ya kuandaa na kutoa mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiriwa wote wa kada ya Sheria katika sekta ya Umma nchini.

Aidha, Kuzinduliwa kwa mtaala huo ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka Mitano wa Chuo cha IJA wa 2018/19-2022/23. Katika kuandaa mtaala huo, Chuo cha IJA kilishirikiana na Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya Umma kama vile Mahakama ya Tanzania ya Tanzania na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) amesema kuwa mafunzo kwa mawakili na wanasheria wa sekta ya Umma yamekuwa yakitolewa bila kuwepo kwa mtaala mahususi ambapo kwa sasa ni wakati muafaka kuwa na mtaala huo.Aliongeza kuwa kwa kuzingatia waraka namba 5 uliotolewa na Ofisi ya Rais; Utumishi na Utawala Bora kila Taasisi ya Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa waajiriwa wapya wa kada ya Sheria Serikalini wanapata mafunzo elekezi kupitia katika Chuo Uongozi wa Mahakama Lushoto.


Baadhi ya Mambo ya yanayoangaziwa katika mtaala huo ni pamoja na; kuwawezesha waajiriwa wapya kuelewa namna ya kuendesha shughuli za Serikali, Utumishi wa Umma, Sheria ya Utumishi wa Umma, Kanuni na taratibu, Namna ya kufanya mawasiliano ndani ya Utumishi wa Umma, kanuni na taratibu, namna ya kufanya mawasiliano ndani ya Utumishi wa Umma,pamoja na rasilimali watu.

MABULA AZITAKA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA NA MAJI PAMOJA NA UMEME KUFIKISHA HUDUMA KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

Bw.Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) akimuonyesha eneo Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula itakapojengwa ofisi za Wizara hiyo alipotembelea eneo hilo leo jijini Dodoma
Mafundi mbalimbali kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wapo kazini katika eneo la ujenzi wa ofisa za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akiangalia ramani ya ujenzi wa ofisi ya wizara yake katika ni Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) na kulia ni wa msimamizi mradi huo Hasani Bendera 
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akiwa na Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wakikagua maeneo ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia kwa umakini maelezo ya Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula (hayupo pichani) alipotembelea eneo zitakapojengwa ofisa za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto

Msimamizi mradi huo Bw.Hasani Bendera kutoka shirika la nyumba Tanzania (NHC) akionyesha eneo itakapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Ardhi nyumba maendeleo ya makazi Mhe.Angelina Mabula alipotembelea eneo hilo leo jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelea eneo zinapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto leo jijini Dodoma
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula,akimsisitizia jambo Kaimu meneja kutoka shirika la nyumba Tanzania (NHC) kutoka Dodoma kulia ni Frank Mambo,mbunifu majengo wa NHC 
Bango likionesha mji wa Serikali ambapo eneo hilo zitajengwa ofisi za wizara mbalimbali Ihumwa jijini Dodoma
Fundi kutoka NHC Yusuph Amir akizungumzia ujenzi wa ofisi ya wizara ya ardhi nyumba maendeleo ya makazi .PICHA NA ALEX SONNA WA FULLSHANGWEBLOG



Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imezitaka mamlaka zinazohusika na maji pamoja na umeme kufikisha huduma hizo mapema iwezekanavyo katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma ili kurahisisha ujenzi wa ofisi za Wizara kuanza.

Naibu waziri wa wizara hiyo Angelina Mabula ametoa maagizo hayo leo alipotembelea eneo zinapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto katika eneo hilo.

Mabula amesema kuwa kutokana na kasi walinayo Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) ambao ndio wanatekeleza ujenzi huo wanaweza kukwamishwa na changamoto ya maji .

“Shirika la Nyumba wako serius kweli na kazi hii maana walipewa kazi ya kujenga ofisi za Wizara tatu baada ya siku mbili tu wakaanza kufanyia kazi agizo hilo, ila changamoto inakuwa kwenye huduma ya maji na umeme ambazo hazipo katika eneo hili.

“Sasa ili kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi huu kwa wakati wa siki 30 ni lazima mamlaka husika wahakikishe wanafikisha huduma ya maji na umeme mapema iwezekanavyo, hasa maji ambayo ndio inahitajika katika hatua ya awali,” amesema Mabula.

Aidha Naibu amesema kuwa wakati wanasubiria huduma hiyo kufikishwa wataangalia namna ya kupata maji ya visima lengo ikiwa ni kukamilisha ujenzi huo kwa wakati huku akisema atatembelea tena eneo hilo baada ya wiki moja .

Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo kutoka NHC Hasani Bendera amesema kuw wanatarajia kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa bila kujali changamoto ambazo zitajitokeza.

“Tusiangalie changamoto, muda tuliopewa si tatizo kwetu kwani tumejipanga kuhakikisha kuwa tunafanya kazi hii kwa wakati, iwe usiku, mchana, kiangazi au mvua ikiwa inayesha, kazi Itafanyika na tutakamilisha kwa wakati,” amesema Bendera

Kuhusu gharama ya mradi huo Bendera amesema kuwa hadi siku ya jumapili Disemba 2, 2018 watapata jibu kamili kuwa mradi huo utagharimu kiasi gani cha fedha.

Naye fundi kutoka NHC Yusuph Amir amesema kuwa kazi ya kusafisha eneo hilo lenye ukubwa wa hekari zaidi ya 20 itafanyika kwa muda wa siku mbili huku akisema kupitia mradi huo Watanzania watapata ajira.

Katika eneo hili ambalo zitajengwa ofisi za Wizara hizo, tayari NHC wapo hatua ya kusafisha huku ujenzi ukitarajiwa kuanza rasmi jumatatu Disemba 3, 2018.

SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI



NAIBU Waziri wa Nishati wa tatu kutoks kushoto akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili
Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara hiyo kukagua miradi wanayoifadhili kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akiteta jambo na Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu

Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akisaini kitabu cha wageni kulia ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu
NAIBU Waziri wa Nishati wa nne kutoka kushoto Subira Mgalu akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kulia akiwa na Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakifurahia jambo wakati wakiwa eneo la Mradi
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup katika akiwa na Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu kulia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigellakushoto mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Tanga

Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wa pili kutoka kulia akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu wakitazama ngoma mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mkoani Tanga



SERIKALI ya Norway imefurahishwa na jitihada zilizofanywa na serikali nchini katika kusimamia fedha walizotoa mwaka 1995 kugharamia miradi ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vilivyopo hapa nchini.

Akizungumza leo baada ya kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili, Waziri wa Maendeleo nchini Norway Nicolai Astrup, alisema walitoa fedha hizo kwa serikali kutokana na uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo ikiwemo usimamizi mzuri uliofanywa na serikali ya awamu ya tano. Waziri huyo pia alisema kuwa serikali yake imeongeza mkataba wa kusaidia uwekaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijiji kutoka mwaka 2020-2021 baada ya kuridhika na usimamizi mzuri uliofanywa katika ukarabati wa vituo hivyo.

“Nipo hapa Pangani Falls, Norway na Tanzania wanahusiano muda mrefu, nimekuja kufuatilia matokeo ya msaada tuliotoa mwaka 1995, kwa vituo vya kuzalisha umeme ‘Hydro Power Plants’,” alisema. Baadaye akizungumza na wananchi wa mji wa Bagamoyo wilayani Korogwe Waziri huyo alisema kwamba nishati ya umeme ni muhimu katika maendeleo ya wananchi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kwamba serikali yao itanedelea kushirikiana na Tanzania kusaidia nishati hiyo.

Serikali ya Norway ilitoa kiasi fedha za Kimarekani dola milioni 126 awamu ya kwanza na kisha awamu ya pili ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vya New pangani Falls, Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Mtera ukarabati uliomalizika Aprili mwaka huu walitoa jumla ya shilingi bilioni 21.

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu alisifu juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Norway kuwekeza kwenye sekta ya nishati kwa nchi hatua ambayo imewezesha maeneo mengi kunufaika na huduma hiyo muhimu.
Licha ya kufanyia ukarabati lakini pia walishiriki katika ujenzi kwa kutoa zaidi ya asilimia 42 pamoja na Serikali ya Sweeden kwenye ujenzi wa kituo hicho hatua ambayo imesaidia kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Alisema serikali ya Norway ni wadau wakubwa kwenye utekelezaji wa umeme vijijini na mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa iliyopata fursa ya uwepo wa vijiji vinavyofadhiliwa na katika mradi wa umeme vijijini ujazilizi. “kwa kweli kama Naibu Waziri naishukuru sana Serikali ya Norway kwa jitihada kubwa wanazofanya kwa uwekezaji kwenye sekta ya nishati katika nchi yetu sio suala la kupeleka umeme vijijini pekee lakini wamekuwa wakiwekeza kwenye sekta za mafuta na gesi”Alisema Naibu Waziri Mgalu.

Aliongeza kuwa licha ya uwekezaji wao katika maeneo hayo lakini pia katika sekta ya nishati jadidifu kwa kuangalia maeneo yaliyopo mbali kuweza kuyawekea miundombninu ya umeme ambao umesaidia kuchochea kazi ya ukuaji wa maendeleo kwenye baadhi ya maeneo.

“Sisi tunaona katika hili wametupa fursa na wamehaidi kuendelea kushirikiana na serikali kwenye maeneo mbalimbali hasa ya vijijini kuhakikisha yanapata nishati ya umeme na wamefadhili mpaka 2021 kuona vijiji vinapata umeme”Alisema.