Sunday, August 26, 2018

WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2018 JITEGEMEE SEKONDARI MGULANI JKT WATAKIWA KUJIAJIRI

Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Felix Lyaviva amewashauri wanafunzi waliopo shuleni kujiandaa kujiajiri na siyo kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo yao.
Lyaviva ametoa rai hiyo leo alipokuwa akifunga mafunzo ya ukakamavu ya wanafunzi wa Kidato cha Tano 2018 wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee ya jijini Dar es Salaam.
Akiwahutubia wanafunzi hao mbele ya wazazi, walimu, maafisa wa jeshi wakiwemo wastaafu na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, Lyaviva alisema; "Nawapongeza sana kwa mafunzo ya ukakamavu mliyopewa, mmeonesha ni jinsi gani mlivyoiva lakini niwaombe muwe na ndoto za kujiajiri siyo kuajiriwa mara mtakapotoka hapa."

Mkuu huyo wa wilaya, amewaasa wanafunzi kutojihusisha na vitendo vya mapenzi, uvutaji wa madawa ya kulevya na sigara ambavyo vinaathari kubwa katika maisha.
"Nyie wanafunzi wa kike, nawaasa msikubali kurubuniwa na wenzetu wa kiume kwani athari zake ni kupewa mimba ambazo zitawaharibia maisha yenu huku wao wakiendelea na masomo," alisema Lyaviva.

Aliongeza kuwa, ni vyema wanapotongozwa wakatoa taarifa kwa walimu wa nidhamu ili vijana wenye tabia hiyo washughulikiwe na siyo kuwachekea.

Kuhusu suala la kujiajiri, aliwashauri wanafunzi wawaeleze wazazi wao nini wanapenda kufanya maishani mwao ili wazazi wawaunge mkono kwa kuwaandalia mazingira ya kutimiza ndoto zao hizo.

"Kama unapenda kumiliki shule ya awali, wape wazo lako wazazi wako ambao wanaweza kukuunga mkono kwa kukujengea darasa moja halafu hapo baadaye ukaendelea mwenyewe, msiwaze kabisa suala la kuajiriwa," alisema.

Aliongeza kuwa, hawawezi kutimiza ndoto zao kama hawatakuwa na hofu ya Mungu na kuzifuata amri zake kumi ambazo zipo kwenye vitabu vyote vitakatifu.

"Mkisoma kwa bidii huku mkiwa na hofu ya Mungu na kutimiza amri zake kumi, mtafanikiwa maishani mwenu, lakini mkienda kinyume mtakwama," alisema mkuu huyo wa wilaya.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Kanali Robert Kessy akimkaribisha Lyaviva aliyekuwa mgeni rasmi, alimshukuru kwa kukubali kufika kufunga mafunzo hayo.
Kessy alimfahamisha mkuu huyo dhumuni la mafunzo hayo kwa wanafunzi kwamba ni kuwaweka katika hali ya ukakamu, kuwa na nidhamu, afya nzuri na kuwa wazalendo kwa nchi yao.

"Mafunzo haya yalianza rasmi mwaka 1985 yalikuwa ya wiki mbili na yaliongozwa na makamanda wetu, lakini ilipofika mwaka 2003 ndipo wanafunzi walipoanza kujiongoza wenyewe kama unavyoona," alisema Kessy.

Gwaride hilo lililowahusisha wanafunzi wa kiume na wakike lilikuwa na vikosi nane pamoja na kikosi maalum cha ukakamavu 'komandoo' liliongozwa na Stanrey Emmanuel.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akiwasili kwenye uwanja lilipofanyika gwaride la wanafunzi. (kulia) ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Robert Kessy.
Kamanda mkuu wa gwaride,  Stanrey Emmanuel akikabidhiwa zawadi na Mkuu wa Wiyala ya Temeke, Felix Lyaviva kwa kuliongoza vizuri gwaride hilo.

 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
 Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakifuatilia gwaride hilo.
 Kikosi cha nne kikitoa heshima kwa mgeni rasmi kilipokuwa kikitembea kwa mwendo wa haraka.
 Gwaride la ukakamavu likipita mbele ya mgeni rasmi.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva akimkabidhi zawadi Julieth Peter aliyekuwa kamanda wa kikosi namba tatu kwa kuongoza vizuri kikosi chake.
 Mkuu wa shule ya Sekondari ya Jitegemee, Robert Kessy akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva aliyekuwa mgeni rasmi.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, akihutubia.
 Gwaride likiendelea.
Brass Band ya JKT ikiongoza Gwaride hilo.


Thursday, August 23, 2018

TANZANIA YAZINDUA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

Naibu Waziri wa Vijana na Kazi Mhe. Anthony Mavunde (MB), Katibu Mkuu (Sera na Uratibu), Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Maafa na Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Prof. Petteri Taalas wakionesha mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
----------------------------------------------------------
Tanzania kupitia programu ya Kidunia ya Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services - GFCS) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Maafa imefanikiwa kuandaa na kuzindua rasmi Mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia vijana na kazi mhe. Anthony Mavunde (MB) kwa niaba ya  mhe. Jenista Mhagama(MB) Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu alisema uzinduzi wa mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa nchini utasaidia kufahamu mahitaji sahihi kwa watumiaji wa taarifa za hali ya hewa na kuongeza uhitaji wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa. Aliongeza kwa kuwataka wananchi wazitumie huduma za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania hasa ukizingatia kuwa huduma hizo zimeboreshwa na usahihi wa utabiri umeongezeka hadi kufikia zaidi ya 80%
‘Nimeelezwa kuwa Mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa nchini unatoa fursa ya kipekee katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kujenga uwezo wa watoa huduma za hali ya hewa na watumiaji, aidha ushirikiano kati ya mtoa huduma za hali ya hewa na watumiaji utaongezeka. Vilevile, mfumo huu utasaidia kufahamu mahitaji sahihi kwa mtumiaji wa taarifa za hali ya hewa ambapo utasaidia kuongeza uhitaji wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa’ alisema mhe. Mavunde
Naye Katibu Mkuu (Sera na Uratibu), Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Maafa katika maneno yake ya utangulizi alisema Baraza lilichukua jukumu la kuandaa mfumo kutokana na ukweli kuwa huduma za hali ya hewa zina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya taifa na zinahitajika katika sekta nyingi hivyo utoaji na matumizi ya huduma za hali ya hewa ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi ya nchi yoyote, hasa katika hali ya sasa ya mabadiliko ya hali ya hewa. Vilevile aliipongeza TMA kwa kuboresha utabiri
Wakati wa uzinduzi huo, alishiriki pia Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Prof. Petteri Taalas ambaye pia alipata nafasi ya kuzungumza akiwa kama mratibu na msaidizi wa uboreshaji wa huduma za hali ya hewa kwa nchi wanachama wa WMO ikiwemo Tanzania. Prof. Taalas aliongezea kwa kusema kuwa WMO imeisaidia Tanzania (TMA) kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo GFCS inayotekeleza lengo la kuongezea uwezo kwa nchi za Afrika kama Tanzania kupitia TMA katika kuboresha na kutoa huduma za hali ya hewa hadi kuwafikia wananchi wa chini kabisa.
Kwa upande wake Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA katika maelezo yake aliwashukuru viongozi wote walioweza kuhudhuria uzinduzi huo sambamba na Katibu Mkuu wa WMO akitambua kwamba ushiriki wake unadhihirisha namna anavyothamini juhudi za serikali katika kuboresha na kuimarisha huduma za hali ya hewa nchini
Uzinduzi wa mfumo wa Taifa wa hali ya hewa ulifanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, mashirika ya umoja wa kimataifa, mashirika ya maendeleo, taasis zisizo za kiserikali, wanahabari na wadau mbalimbali wa huduma za hali ya hewa.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA UHUSIANO

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Hati za Kimila za Kumiliki Ardhi Kuwakomboa Wananchi Kiuchumi - DC Kilosa

 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akisisitiza kuhusu wananchi kutumia hati  za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo ikiwemo kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha wakati wa hafla ya kuwakabidhi wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa hati hizo zilizotolewa baada ya maeneo yao kurasimishwa kwa kupimwa
 Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akisisitiza umuhimu wa hati za kimila za kumiliki ardhi katika kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi wakati wa hafla ya kutolewa kwa hati hizo kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani kilosa ambapo Mpango huo kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya hiyo wamefanikisha upimaji wa ardhi katika Vijiji 37.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akimkabidhi mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Magubike hati kimila ya kumiliki ardhi.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\2b.JPG
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Magubike wakipatiwa Hati Miliki za Kimila na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Adam Mgoyi. Pichani ni Bw. Jackson Mgoma, akiwa katika furaha baada ya kuipata Hati hiyo.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\3a.JPG
DC Kilosa Mhe. Adam Mgoyi akiongea na wanachi wa Kijiji cha Magubike (hawapo pichani)katika tukio la kugawa Hati miliki, zoezi linaloendeshwa na MKURABITA kwa lengo la kuwaondolea wananchi umasikini na kuwawezesha kuendesha uchumi kutokana na mali walizo nazo wenyewe. Kulia kwa DC aliyekaa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilosa Bw. Yohana Kasitila.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\4.JPG
Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania  (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe, akisisitiza jambo mara baada ya Hati miliki kutolewa kwa Wananchi wa Kijiji cha Magubike waliorasimishiwa Ardhi.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\7b.JPG
Huu ndio muonekano wa Hati miliki ambayo kwayo inasaidia kupunguza migogoro ya Ardhi ndani ya Vijiji, inasaidia Mwananchi kumiliki Ardhi yake kisheria na inapandisha thamani ya Ardhi baada ya kurasimisha na kupatiwa hati hiyo.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\1a.JPGBaadhi ya wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa waliopatiwa Hati za haki Miliki wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi (Katikati waliokaa) na Viongozi wa wengine wa Wilaya hiyo na Viongozi wa MKURABITA. Hii ni  mara baada ya kukabidhiwa hati za kurasimisha Ardhi kwa lengo la kutambulika kisheria hivyo kusaidia kuondoa umasikini miongoni mwao.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\Magubike\8.JPG


Hongera wananchi Wilayani Kilosa kwa mwamko wa kurasimisha Ardhi yenu hivyo kuwa na ulinzi wa Ardhi hiyo, kuongeza thamani na kusaidia kupunguza migogoro mliyokuwa nayo kwa muda mrefu. Huo ndio muarobaini pekee.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi akisalimiana na viongozi wa Kijiji cha Magubike kabla ya kuanza kwa hafla ya kutoa hati za kimila kwa wananchi wa Kijiji hicho.

 Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka MKURABITA  Bw. Japhet Werema akisisitiza umuhimu wa mpango wa kurasimisha ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa wakati wa hafla ya kutoa hati za kimila za kumiliki ardhi kwa wananchi wa Kijiji hicho.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi walipata hati za kimila katika Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa pamoja na Watendaji wa Halmashuri na  wale wa MKURABITA.
 Mratibu wa Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akifurahia ngoma za asili pamoja na kikundi cha ngoma hizo katika Kijiji cha Magubike  Wilayani Kilosa wakati wa hafla ya kukabidhi hati kwa wananchi wa Kijiji hicho.
 Kikundi cha ngoma za asili cha Kijiji cha Magubike kikionesha umahiri wake katika kucheza ngoma hizo wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila za kumiliki ardhi kwa wananchi wa Kijiji hicho.

 Sehemu ya wananchi wakifuatilia hafla hiyo ya kutolewa kwa hati za kimila za kumiliki ardhi katika Kijiji cha Magubike Wilayani Kilosa.

Mratibu wa Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) Bi. Serapia Mgembe akiwasikiliza baadhi ya wananchi mara baada ya hafla ya kutoa hati za kimila za kumiliki ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Magubike- Kilosa)

Wednesday, August 22, 2018

SWALA NA BARAZA LA EID EL HAJJ ILIYOFANYIKA KIZIMKAZI MKOA WA KUSINI UNGUJA

 Sehemu ya wananchi waliohudhuria katika Swala ya Eid el Hajj wakisikiliza Khutba iliyosomwa na Sheikh Abdalla Issa Makame (hayupo pichani) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini,ambapo Viongozi wa Kitaifa walihudhuria katika  Swala hiyo iliyoswaliwa Kitaifa  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduzi Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatib Hassan  wakati alipowasili katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo kabla ya  Swala ya Eid  el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo waislamu mbali mbali  walihudhuria
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Mashekhe wakati alipowasili katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja kabla ya  Swala ya Eid  el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja ambapo waislamu mbali mbali katika Mkoa huo  walihudhuria
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali na Mashekhe wa Mkoa wa Kusini Unguja  katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa  iliyoswaliwa leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja,ambapo Swala hiyo imeongozwa na Sheikh  Suleiman Haji Ibrahim
 Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Kusini Unguja  wakiwa katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa  iliyoswaliwa leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,ambapo Sheikh  Suleiman Haji Ibrahim(hayupo pichani) aliongoza Swala hiyo,iliyohudhuriwa na Viongozi  wa Kitaifa akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
 Baadhi ya akinamama waliojumuika katika swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi Wilaya ya Kusini,Mkoa wa Kusini  Unguja
 Sheikh Abdalla Issa Makame (kulia) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini Unguja akisoma Khutba mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine pamoja na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo baada ya Swala ya Eid el Hajj,Kitaifa iliyoswaliwa katika uwanja wa Jamhuri Makunduchi
 Waislamu wakimsikiliza Sheikh Abdalla Issa Makame (hayupo pichani) kutoka Kijiji cha Paje Wilaya ya Kusini  akisoma Khutba ya Swala ya Eid el Hajj, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine pamoja na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja leo baada ya Swala hiyo iliyoswaliwa katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine na Waislamu mbali mbali waliohudhuria katika Swala ya Eid el Hajj wakiitikia dua iliyoombwa na Sheikh Abubakar Ali Mohamed (wa pili kuilia) baada ya Swala hiyo iliyoswaliwa Kitaifa katika Mkoa wa Kusini Unguja   leo  katika Uwanja wa Jamhuri Makunduchi, Wilaya ya Kusini
 Askari wa Kikosi cha Polisi FFU wakitoa salamu ya Hesma kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa  akipokea salamu hiyo ya heshma  katika  Sherehe  za Baraza la Eid el Hajj zilizofanyika leo  katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa  akipokea salamu ya heshma kwa gwaride maalum la kikosi cha Polisi FFU wakati wa Sherehe  za Baraza la Eid el Hajj zilizofanyika leo  katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa  akisalimiana na Wananchi na kuwatakia kheri na salama katika Sikukuu ya Eid el Hajj baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa  akisalimiana na Wananchi na kuwatakia kheri na salama katika Sikukuu ya Eid el Hajj baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa  akisalimiana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Wananchi na kuwatakia kheri na salama katika Sikukuu ya Eid el Hajj baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Baadhi ya Viongozi na Wananchi wakiwa  katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
 Viongozi wanawake wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa  akitoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mohamed Hassan Haji (kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiitikia dua iliyoobwa baada ya Hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein alipoitoa  katika sherehe za Baraza la EId El Hajj lililofanyika Leo katika ukumbi wa mikutano wa Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi Mkunguni,Mkoa wa Kusini Unguja

MAGAZETI LEO ALHAMISI AGOSTI 22, 2018