Wednesday, February 28, 2018

KESI YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA INAYOMKABILI TIDO MHANDO MHANDO KUANZA KUSIKILIZWA MACHI 28

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

KESI  ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando kuanza kusikilizwa Machi 28, mwaka huu

Hatua hiyo inakuja baada ya mtuhumiwa huyo leo Februari 28, kusomewa maelezo ya awali (PH), Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa

Kabla ya kusomewa PH, Mhando alikumbushwa mashtaka yake yanayomkabili na Wakili wa Serikali Dismas Mganyizi.Katika maelezo hayo ya awali, Tido amekubali maelezo yake binafsi ya kwamba alikuwa Mkurugenzi  Mkuu wa TBC  mwaka 2006 hadi 2010 na kuwa alikuwa msimamizi katika shughuli za TBC lakini  siyo kwa shughuli zote.

Pia alikubali kutoa maelezo katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) lakini hakukiri na kuwa alifikishwa mahakamani Januari 26,mwaka 2018.Aidha Mhando alikana mashtaka yote yanayomkabili na ksi hiyo itaanza kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuketa mashahidi wao Machi 28,mwaka 2018.

Mhando anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.

Inadaiwa kuwa Juni 16,mwaka  2008 akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhando ambaye alikuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili, Mhando anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake Juni 20,mwaka 2008 aliposaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11,mwaka 2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai, Mhando alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Katika shtaka la nne, anadaiwa kuwa  Novemba 16, mwaka 2008 akiwa Dubai, Mhando alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Katika shtaka la mwisho,  anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16,mwaka 2008 akiwa UAE, Mhando aliisababishia TBCli hasara ya Sh.887,122,219.19.

WATANZANIA SASA WAFIKIA MILIONI 54.2, NUSU YA WATU WOTE NI WATOTO

*Serikali yapiga marufuku mashirika kutoa takwimu ambazo hazina uthibitisho wa ofisi ya Takwimu

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk. Philip Mpango amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao milioni 54.2 huku asilimia 50 wakiwa ni wa umri chini ya miaka 18.

Pia Dk.Mpango amewakumbusha wadau wote was ndani na nje ya nchi kuwa takwimu za idadi ya watu kwa nchi ya Tanzania ni hizo ambazo amezitangaza leo na si vinginevyo.
.
Hivyo amepiga marufuku kwa shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu wa Tanzania na kuchapisha matokeo hayo bila kushirikisha Ofisi ya Taiga ya Takwimu na atakayebainika kufanya hivyo watamchukulia hatua kali za kisheria.

Dk.Mpango amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazondua taarifa ya makisio ya idadi ya watu Tanzania amvapo amesema kwa makadirio yaliyotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Na kuzingatia viwango vya uzazi na vifo kwa takwimu za mwaka 2016, idadi ya watu Tanzania sasa ni milioni 52.6 ambapo Tanzania Bara ni watu milioni 52.6 na Tanzania Bara watu milioni 1.6 kwa mwaka 2018.Dk.Mpango amesema idadi hiyo inakadiriwa kufikia watu milioni 59.4 mwaka 2021 na ifikapo mwaka 2030 idadi ya watu itafikia milioni 77.5.

Amefafanua kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani watu wapatao milioni 1.6 hapa nchini.Dk.Mpango amesema ongezeko hill linatokana na idadi kubwa vya vizazi vipatavyo milioni 2.0 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo ni takribani 400,000 kwa mwaka.

"Utafiti wa mama na mtoto wa mwaka 2015/16 unaonesha kwamba mwanamke wa kitanzania atazaa watoto watano katika maisha yake yote ya uzazi .

" Hata hivyo kiwango cha uzazi kilipungua kutoka wastani wa watoto 7 mwaka 1978 had I wastani wa watoto watano mwaka 2016.Baadhi ya sababu za juu cha uzazi ni kiwango kikubwa cha vifo vya watoto,familia kupendelea kuwa na watoto wengi,umasikini,mila,imani za kidini na matumizi madogo ya uzazi wa Mpango,"amesema.

Ameongeza matokeo yake ni kuwa na idadi ya watu hapa nchini imeendelea kuongezeka na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya sita katika Bara la Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya Nigeria, Ethiopia, DRC na Misri.

Amesema kwa mtazamo wake wingi au au uchache wa idadi ya watu sio tatizo bali tatizo ni pale ambapo kasi ya ongezeko la idadi hiyo inazidi kasi ya ukuaji wa uchumi na hivyo kulifanya Taifa kushindwa kumudu ipasavyo mahitaji ya wananchi.

Dk.Mpango amesema kasi ya ongezeko la idadi ya watu pia inaleta changamoto ya idadi kubwa ya watoto na vijana ."Kwa mfano takwimu nilizozizindua leo zinaonesha asilimia 50 ya watu wote nchini ni watoto wenye umri chini ya miaka 18.

"Asilimia hii kubwa ya watoto katika nchi zinazoendelea inatokana na mabadiliko ya kidemografia kutoka viwango vya juu vya vifo lakini wakati huo viwango vya uzazi vibaki juu," amesema.

Ameongeza asilimia kubwa ya watoto ni changamoto kwa maendeleo ya nchi yoyote duniani kwa vile kundi hilo lina mahitaji ya kipekee ambayo lazima yatimizwe na Serikali na jamii kwa ujumla wake.Dk.Mpango amesema mojawapo ya changamoto hizo ni kiwango cha juu cha utegemezi kinachotokana na idadi kubwa ya watoto.

Amesema kwa mfano kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kiwango cha utegemezi kiumri ni asilimia 92 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 40 kwa nchi zinazoendelea.Hiyo ikiwa na maana kuwa kwa Tanzania kila watu 100 wenye umri wa miaka 15 hadi 64 wanategemewa na watu 92 wenye umri chini ya miaka 15 wenye umri zaidi ya miaka 65.

Dk.Mpango amesema ili kukabiliana na changamoto hizo za ongezeko la idadi ya watu ,Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwa pamoja na kutunga na kutekeleza sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992 na ilifanyiwa marekebisho mwaka 2006.

Amesema lengo la Sera hiyo ni kutoa ni kutoa miongozo ya kushughulikia masuala ya idadi ya watu.Kwa kutambua kuwa kuna mahusiano baina ya mwenendo wa idadi na ubora wa maisha ya wananchi kwa upande mmoja na ulinzi wa mazingira.

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MTWARA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa wakiwasalimia wananchi, wakati wakiwasili katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya bakora, kutoka kwa mzee Mohammed Abeid Liyanga, anaye wawakilisha wazee wa Newala, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala Mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Newala Mjini, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi mashine ya kubangulia korosho, Aziza Juma, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi mashine ya kubangulia korosho, Halima Maulid, katika viwanja vya michezo vya sabasaba vilivyopo Newala mjini, Februari 28, 2018. 

NDITIYE AITAKA TMA IJITANGAZE UMUHIMU WAKE KIUCHUMI NA KIJAMII

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akizungumza na Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Dkt. Hamza Kabelwa
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiy (hayupo pichani) akiangalia picha za usafiri wa anga na majini ambazo usafiri wake unategemea utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akipatiwa taarifa ya hali ya hewa kwa usafiri wa anga na Meneja wa Utabiri wa Hali ya Hewa Bwana Samwel Mbuya wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wakati alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiye (hayupo pichani) akiangalia picha ya ujenzi wa barabara ya mabasi ya mwendokasi ambapo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli unategemea utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiye (hayupo pichani) akiangalia picha ya rada ya hali ya hewa iliyopo kwenye vituo vya utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiye (hayupo pichani) akipatiwa maelezo na msomaji wa taarifa ya hali ya hewa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni Bi. Hellen Msemo kuhusu namna wanavyotoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania jijini Dar es Salaam



……………………


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kujitangaza umuhimu wake katika nyanja ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Mhandisi Nditiye ameyasema hayo alipotembelea makao makuu ya TMA na kuzungumza na bodi ya Mamlaka hiyo, menejimenti na wafanyakazi kwa lengo la kutambua majukumu yao na kufuatilia utekelezaji wake ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi.

Akizungumza na Bodi, menejimenti na wafanyakazi, Mhandisi Nditiye amewaeleza kuwa TMA ni chombo muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya taifa letu na wananchi kwa ujumla kwa kuwa sekta ya usafiri wa anga, majini, ujenzi wa majengo mbalimbali, miundombinu ya barabara na reli, afya, kilimo na mazingira vyote vinategemea taarifa za hali ya hewa kutoka kwenye Mamlaka hii. “Mtambue kuwa hakuna ndege inayoweza kutua wala kuruka bila kupata taarifa kutoka kwenu, vile vile mkandarasi anayejenga reli ya kisasa ya SGR nae anategemea taarifa zenu kwa kiasi kikubwa, hivyo mtambue ninyi ni muhimu na mjitangaze,” amesema Mhandisi Nditiye.

Amesisitiza kuwa ni vema mjitangaze ili wananchi na wadau mbalimbali wafahamu majukumu na umuhimu wa taasisi yenu kwa kuwa uchumi wa taifa hili unategemea taarifa zenu ambapo wananchi wengi wamezoea kusikia na kuwaona mkitoa taarifa za tahadhari za hali ya hewa zinazohusiana na majanga na matukio mengine yanayohusiana na utabiri wenu angali ninyi mna taarifa muhimu zaidi na tofauti na mtazamo wa wananchi walio wengi.

Amefafanua kuwa wananchi wanaziamini taarifa zenu za hali ya hewa kwa kuwa kwa kiasi kikubwa yale mnayotabiri na kuwaeleza ndiyo yanayotokea iwe ni mvua kubwa, upepo mkali au joto kali kama ilivyo sasa. “Nimetembea na kukagua mitambo, vifaa vya kisasa na namna wanavyofanya kazi na nimebaini kuwa taarifa zinazotolewa hapa zimekusanywa kutoka vituo mbali mbali vya hali ya hewa nchini ambapo hapa makao makuu wataalamu wanazichakata, kusambaza kwa wahusika na kuhifadhiwa, na zinaonesha kuwa ni taarifa za uhakika kwa kiwango cha asilimia 87.5 ambapo imeongezeka kutoka asilimia 82.1 kwa miaka mitatu iliyopita,” amesema Mhandisi Nditiye.

Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi wakati akiwasilisha taarifa yake kwa Mhandisi Nditiye amesema kuwa Mamlaka hii ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya taifa letu na wananchi kwa ujumla kwa kuwa utoaji wa taarifa na huduma za hali ya hewa nchini zimewezesha uokoaji wa maisha ya watu na mali zao; kuepuka au kupunguza athari na hasara zinazosababishwa na matukio ya hali ya hewa; kuongeza tija na mafanikio katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi; kuwa na miundombinu imara kama vile barabara, madaraja; kuongeza ufanisi katika sekta za usafiri na mawasiliano; kuchangia katika sekta za ujenzi na uendeshaji wa viwanda nchini na kukuza pato la taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Hamza Kabelwa amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa wahitaji wa taarifa za hali ya hewa kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali ambao wanahitaji kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kiuchumi na kijamii wamekuwa wengi na teknolojia ya utabiri wa hali ya hewa na utoaji wa taarifa zake umebadilika ambapo inatulazimu kuhuisha Sheria Na. 6 ya Hali ya Hewa ya Mwaka 1978 na kukamilisha Sera ya Taifa ya Hali ya Hewa ili ziweze kwenda na wakati pamoja na kuboresha chuo cha Hali ya Hewa Kigoma kwa kuwa ndio chuo pekee nchini kinachotoa elimu ya awali na ya kati ya hali ya hewa.

Ameongeza kuwa TMA imepatiwa cheti cha ubora wa utoaji huduma na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) kwa kutoa huduma kwa sekta ya anga nchini. Pia, inashirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa jangwa la Afrika (SADC), Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa kubadilishana taarifa za hali ya hewa, mabadiliko ya hali ya hewa yanayohitaji ushirikiano wa kimataifa, na kuendeleza na kutunza mtandao wa vituo vya uangazi wa hali ya hewa ili kukidhi makubaliano ya kimataifa ya kubadilishana taarifa hizo.

Dkt. Nyenzi amemshukuru Mhandisi Nditiye na kumueleza kuwa TMA inafarijika kusikia kuwa anafahamu kwa undani umuhimu wa utabiri wa hali ya hewa nchini, hivyo ni imani yake kuwa ataisamimia vema ili ifikie malengo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

NAIBU WAZIRI WA ARDHI ATEMBELEA MPAKA WA TANZANIA NA KENYA NAMANGA ARUSHA

 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akielekea kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa TRA aliyeko katika kituo cha Huduma za  Pamoja Mipakani (OSBC) Paul Kamkulu  kuhusu huduma zinazotolewa katika kituo hicho kilichopo eneo la Namanga mpaka wa Tanzania na Kenya.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi msaidizi Upimaji vijijini wa wizara Huruma Lugalla (wa pili kulia) wakati akikagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akitoa maelekezo kwa ujumbe alioambatana nao wakati wa  kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga wilaya ya Longido mkoa wa Arusha.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na ujumbe wake wakitembea eneo la ardhi huru kuelekea ilipo alama ya mpaka baina ya Tanzania na Kenya Namanga mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula  akiwa amemshika Ngamia aliyemkuta eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya wakati alipokuenda kukagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya.


WAFANYAKAZI JNIA,TAA WAMLILIA MAREHEMU SWAI

Marehemu Jerome Swai
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (kulia), akimpa pole Bi. Honoratha Emmilian aliyefiwa na mume wake marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Bomba (JNIA), alifariki tarehe 26 Februari, 2018 kwenye hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian, akitoa pole kwa Bi. Honoratha Emmilian ambaye ni mke wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa fundi bomba.
Waombolezaji kwenye msiba wa marehemu Jerome Swai (kushoto), wakipokea pole kutoka kwa Meneja Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Vedastus Fabian. Marehemu Swai alikuwa Fundi Bomba JNIA na alifariki tarehe 26 Februari 2018
Ndugu wa marehemu Jerome Swai wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (mwenye tai) alipofika kuwafariji, ambapo marehemu alikuwa Fundi Bomba JNIA.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), wakiwa kwenye msiba wa marehemu Jerome Swai aliyekuwa Fundi Bomba. Swai alifariki rarehe 26 Februari 2018 katika hospitali ya Amana.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Juluius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka aliyeinama (kushoto) akiteta jambo na baadhi ya wafanyakazi wa JNIA waliofika kwenye msiba wa aliyekuwa fundi Bomba, Bw. Jerome Swai.


WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wamesikitishwa na kifo cha Bw. Jerome Swai (58) aliyekuwa fundi bomba mahiri kilichotokea  tarehe 26 , 2018 kwenye hospitali ya Amana baada ya kuugua kwa muda Mfupi.

Wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti walisema marehemu Swai alikuwa hakubali kushindwa kwa kuhakikisha anatatua tatizo linalohusiana na mabomba ya maji kwa wakati wote anapokuwa kazini.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Bi. Hanna Kibopile alisema marehemu ameacha pengo kubwa kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.
Naye meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, Bw. Daimon Mwakyosa alisema marehemu alikuwa akifanyakazi kwa bidii na hakukubali kushindwa.

“Marehemu alikuwa akiijua vyema kazi yake na hakukubali kushindwa nakumbuka wakati nikiwa JNIA na tukiwa tumepangwa shift (zamu) moja hakuna kilichoshindikana kwake kuhusu fani yake aliijua vyema kazi yake,” alisema Bw. Mwakosya.

Bi. Fatma Matimba, Kaimu Meneja Utawala JNIA, alisema marehemu Swai alikuwa mchapakazi, ambapo mwaka jana alichaguliwa kuwa mfanyakazi hodari. Pia aliwahi kupewa cheti cha ufanyakazi hodari mwaka 2001 kinachotolewa TUGHE.

Marehemu Swai alizaliwa mwaka 1960 wilaya ya Rombo, na kupata elimu katika shule ya msingi Kilesi mwaka 1976, na baadaye kujiunga na Chuo cha Ufundi cha Makalema akisomea fani ya ufundi bomba daraja la tatu, na baadaye kujiendeleza katika Chuo cha Ufundi cha Chang’ombe mwaka 1988 na VETA mwaka 2007.

Marehemu aliajiriwa na TAA mwaka 1984 akiwa kama fundi bomba daraja la tatu na baadaye alijiendeleza na kufanikiwa kusoma hadi kufikia daraja la kwanza. Marehemu ameacha mjane Bi. Honoratha Emmilian ambaye naye ni mfanyakazi wa TAA katika Idara ya Utawala akiwa kama mhudumu.

Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahala pema peponi.

TANZANIA YADHAMIRIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE NCHINI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi
Wadau wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.


SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 huku lengo likiwa ni kuondoa tatizo hilo nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.

“Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani na kuimarisha afya ya wanawake Tanzania na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Ocean Road Saratani ya Mlango wa kizazi zinazoongoza nchini kwa Asilimia 36 huku ikifuatia na saratani ya matiti, huku jumla ya wagonjwa wa Saratani nchini katika kila wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti.

Aidhe, Serikali imepanga kuanza na wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri wa chini, huku ikitegemea kuchanja zaidi ya wasichana 610,000 katika jitihada za kutokomeza kabisa tatizo hili la Saratani ya mlango wa kizazi nchini,

Mhe Ummy alisisitiza kuwa Chanjo hii itatolewa katika vituo vyote vya Afya nchini vya Serikali, vya watu binafsi na vikundi mkoba bure, na kuwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha mabinti zao wanapata chanjo hii ili kujikinga na ugonjwa huo.

Nae Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dafrossa Lyimo aliendelea kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza juu ya umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya duniani na mamlaka ya chakula na viodozi nchini (TFDA).

SERIKALI YAOMBWA KUENDELEA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA WANAWAKE NCHINI

 Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu, akihutubia wakati akifungua akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP Mtandao, Vicensia Shule akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akihutubia.
 Profesa Bernadeta Killian akitoa mada kuhusu hali halisi ya wanawake na uongozi hapa nchini.
 Spika wa Bunge Mstaafu Mama Anna Makinda na Naibu Waziri wa Walemavu (Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) – Stella Ikupa wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye kongamano hilo.
 Kongamano likiendelea.
 Taswira ya ukumbi kwenye kongamano hilo.


Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya akizungumza na wanahabari

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga bajeti kubwa katika bajeti zake kwa ajili ya kumuendeleza mwanamke wa Tanzania.

Ombi hilo limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu wakati akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 jijini Dar es Salaam jana.

"Tunaomba bajeti ya serikali ibadilike kwa kuangalia ajenda ya jinsia ukizingatia changamoto mbalimbali walizonazo wanawake" alisema Dk.Nagu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo.Dk. Nagu aliwataka wanawake wote kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuzijua changamoto walizonazo na kuzitatua kwa msaada wa viongozi wanawake wastaafu.

Aliongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa na ndio wazalishaji wakubwa wa mali lakini kwa namna moja hama nyingine wamekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya mali zinazotokana na uzalishaji wao kutumiwa na wanaume wao.

Katika hatua nyingine Dk.Nagu aliomba wake wa maraisi wawe mbele kuwaendeleza wanawake wenzao kama ilivyokuwa kwa Mama Anna Mkapa kupitia taasisi yake ya Wote Sawa na Mama Salma Kikwete kupitia WAMA.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema wameamua kuandaa kongamano hilo kama sehemu ya kutoa fursa kwa wanawake na wadau wengine kutafakari wapi wamefanikiwa, wapi bado kama kunachangamoto na kupanga mikakati ya kuimarisha ushiriki wa wanawake katika ngazi zote za maamuzi pamoja na uongozi.

Alisema kongamano hilo pia litatoa fursa ya kutafakari suala la ushauri, ulezi au ukungwi katika kuimarisha uongozi.Alisema tafiti zinaonesha kuwa nchi za Afrika zinapoteza takribani dola za kimarekani 105 milioni kwa mwaka kwa kutowaingiza wanawake katika uchumi, pia takwimu zinaonesha kuwa wanawake ni zaidi ya asilimia 70 ya wakulima wadogo ambao ndio wanalisha nchi yetu.

Alisema wanawake walioko katika sekta isiyo rasmi ni asilimia 51.1. ambapo wanaume ni 48.9 na kuwa ni asilimia 20 tu ya wanawake ndio wanamiliki ardhi.Katika kongamano hilo walihudhuria viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wengine ambapo kauli mbiu ilikuwa ni "kusherehekea na kutambua Mchango wa Uongozi wa Wanawake Jukwaani na Nyuma ya Pazia".



Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya amewata wanawake kuwa na moyo wa kuthubutu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanauwezo wa kuongoza.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO FEBRUARY 28,2018