Wednesday, January 31, 2018

KATIBU MKUU WA MIFUGO KUKABIDHI RASMI TAARIFA YA CHAPA YA MIFUGO LEO KWA WAZIRI MPINA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na wafugaji kuhusu upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo(mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. 
Dereva wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.

Na John Mapepele-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.

“Wakuu Wote wa Idara,Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa ” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.

Aidha amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote katika muda wa nyongeza uliotolewa na Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.

Akizungumza katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga chapa mifugo ambayo inatoka nje ya nchi ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali.

Aidha, Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio raia wa Tanzania waliyoingia katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema awali  inakadiliwa kwamba 30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo toka nje ya nchi.

Ameutaka Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza ushirikiano na kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana aliongeza siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji chapa mifugo huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo kikamilifu na wengine wawili wakipewa onyo kali.

Alida kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo Halimashauri ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu. 

Siku kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma, kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa Desemba 31 Mwaka jana .

Aidha alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.

Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi

Na Teresia Mhagama, Katavi

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefanya ziara mkoani Katavi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mwaka 2017 ya kukamilisha ufungaji wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme katika wilaya ya Mpanda  na Mlele mkoani humo.

Dkt. Kalemani alitoa maagizo hayo baada ya mitambo iliyokuwepo  katika kituo cha Mpanda kuharibika na hivyo kupelekea mkoa huo kuwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme huku baadhi ya maeneo katika wilaya ya Mlele yakipata umeme kutoka nchini Zambia.

  Meneja Miradi kutoka TANESCO, Stephen Manda alimweleza Dkt Kalemani kuwa,  ufungaji wa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda umekamilika na sasa kituo kinazalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 huku matumizi ya wilaya ya Mpanda yakiwa ni megawati 2.3.

Manda alieleza kuwa, kukamilika kwa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda  kumewezesha vijiji 14 kusambaziwa umeme ikiwemo wilaya mpya ya Tanganyika ambayo imepata umeme kwa mara ya kwanza kutoka kuanzishwa kwake.

Akiwa katika wilaya ya Mlele, Dkt. Kalemani alielezwa kuwa, ufungaji wa mashine moja ya kuzalisha umeme yenye uwezo wa kilowati 476 umekamilika na kuwezesha baadhi ya wakazi wa Mlele hususan Makao Makuu ya wilaya hiyo (Inyonga) kupata umeme.

Baada ya kupata taarifa ya utekelezaji wa maagizo yake,  Dkt Kalemani aliwapongeza wataalam wa TANESCO waliosimamia na kutekeleza kazi hiyo ndani ya wakati uliopangwa.

Aidha, alitoa maagizo kwa TANESCO ya kuongeza mitambo mingine miwili ya uzalishaji umeme katika kituo cha Mpanda na mmoja katika kituo cha Inyonga wilayani Mlele ili kuweza kuwa na umeme wa kutosha utakaowezesha wanannchi kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uanzishaji wa Viwanda.

Kwa kuwa mitambo hiyo  inatumia mafuta kuzalisha umeme, Dkt Kalemani alisema kuwa, Serikali ipo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme kwa msongo wa kV 400 kutoka mkoani Mbeya- Sumbawanga-Katavi - Kigoma hadi Nyakanazi. Hivyo mkoa wa Katavi utapata umeme wa gridi ya Taifa na kuachana na mitambo ya mafuta ambayo inatumia gharama kubwa.

Akizungumza na wananchi wilayani Mlele, Dkt Kalemani aliwaasa kujitokeza kwa wingi ili kuunganishwa na huduma ya umeme na hivyo kujiletea maendeleo huku akitolea mfano wilaya ya Mlele ambayo matumizi yake ya umeme ni kW 71 ambayo ni sawa na asilimia 15 tu ya uwezo wa mtambo.

Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga alimshukuru Waziri wa Nishati kwa kutoa maagizo ya kufunga mashine nyingine tatu mpya za kufua katika  mkoa wa Katavi suala ambalo litapelekea mkoa huo kuwa na umeme wa uhakika.

Vilevile aliisisitiza Wizara kuharakisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa kilovolti 400 ambao kukamilika kwake kutafungua fursa za kiuchumi mkoani humo kutokana na kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika.

Katika ziara hiyo,  Waziri Kalemani aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Dkt. Gidion Kaunda na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi ambao kwa nyakati tofauti waliwaasa wananchi kulinda miundombinu ya Umeme ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali za kusambaza umeme nchini.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa nne kulia) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja  Jenerali (Mst), Raphael Muhuga  (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Katavi kabla ya kuanza ziara ya kukagua  miradi ya kuzalisha umeme mkoani Katavi.
 Meneja  Miradi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Makao Makuu, Stephen Manda (kulia), akitoa maelezo kuhusu mitambo ya uzalishaji umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi. Anayesikiliza ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( katikati) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja  Jenerali (Mst), Raphael Muhuga  (wa kwanza kushoto).
 Mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi inayozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 kwa kutumia mafuta.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi wa Inyonge wilayani Mlele wakati alipofika wilayani humo kukagua mradi  wa uzalishaji umeme.
 Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt Alexander Kyaruzi akizungumza na wananchi wa  Inyonge wilayani Mlele wakati Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) alipofika wilayani hapo kukagua  mradi wa umeme. Wa kwanza kushoto ni  Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel  Kasanda.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gidion Kaunda akizungumza na wananchi wa  Inyonge wilayani Mlele wakati Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) alipofika wilayani hapo kukagua  mradi wa umeme. Wa kwanza kushoto ni  Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel  Kasanda.
Mtambo wa kuzalisha umeme katika kituo cha Inyonga, wilaya ya Mlele mkoani Katavi unaozalisha umeme wa kiasi cha kilowati 476 kwa kutumia mafuta.

MBUNGE KABATI ATOA MSAADA WA MIFUKO 25 YA SARUJI KATIKA KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA



Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.



Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano (25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa huduma bora ya neon la mungu.


Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.

“Mimi nimejitoa kuchangia shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa aliwaahidi kuwapa mifuko ishirini na tano ya saruji hivyo ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapa mifuko ya saruji yote aliyoiadi hivyo amefanikiwa kutekeleza na kuwaomba wananchi wananchi wengine kuchangia maendeleo ya kanisani.

“Alikuja diwani hapa kwa niaba yangu na kuahidi mifuko hiyo ambayo ni sawa na tani moja hivyo nimeamua kutimiza kuwa lengo langu nikiahidi kitu lazima nitimize malengo yangu ya kuitoa ahadi hiyo” alisema Kabati.

Aidha Kabati aliwata wananchi na viongozi mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa jamii na taasisi ambazo hazina uwezo wa kufikia mafanikio yanayotakiwa kwa ajili ya kutatua kero zinazorudisha nyuma maendeleo.

Kabati amesema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kumtegemea mungu ili kuweza kufanikisha malengo wanayotarajia.Katika hatua nyingine Kabati amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili wakapate elimu ambayo ndiyo itakuwa dira ya maisha yao ya baadae.

Kwa uoande wake mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero alisema kuwa walikuja viongozi wengi na kutoa ahadi nyingi lakini hakuna hata mmoja aliyetimiza ahadi yake zaidi ya mbunge Ritta Kabati.Nilialika wageni wengi wakala na kutoa ahadi nyingi kwa mbwembwe nyingi lakini kilichotokea hadi sana viongozi wote hakuna aliyetimiza malengo hayo hivyo nichukue furasa kushukuru" alisema Okero
Mchungaji Okero alimshukuru mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itatusaidia katika ujenzi wa kanisa letu

MENGI AIPA TWCC JENGO LAKE KUENDELEZA UJASIRIAMALI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD, amekipatia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania ( TWCC) jengo la maonyesho la IPP Ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali.

Jengo hilo pamoja na kuendeleza ujasiriamali litakuwa eneo la maonesho na kufunzia na Dk Mengi amesema amelitoa ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi. Maamuzi ya kutoa jengo hilo yalifuatana na ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa TWCC Jacqueline Maleko aliyetaka jengo hilo kupewa wanawake ili kuwaendeleza kiuchumi na kimafunzo.

 Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce-TWCC), Dk Mengi aliwataka wanawake kuwa macho na kutumia fursa zilizopo kujiwezesha kiuchumi. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mwakilishi wa TRA, Rose Mahendeke (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini TWCC, Bi. Noreen Mawalla (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chemba ya Wajasiriamali Wanawake nchini (TWCC), Bi. Jaqueline Mneney Maleko (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Aliwataka wanawake kuthubutu na kuwa wajasiri katika kuangalia na kuzitumia fursa zilizopo sasa nchini badala ya kuzipita bila kuziona. Aidha Dk Mengi aliwataka wanawake wajiamini na kujihakikishia kwamba wanaweza kujiletea maendeleo, wawe wanyenyekevu katika biashara zao, na wawe na ndoto kubwa ya maendeleo huku wakianza kidogo kidogo badala ya kusubiri mtaji mkubwa. 

Katrika mkutano huo Dk Mengi alitoa ushuhuda wa jinsi yeye alivyoanza biashara zake na kusema alitumia fursa alizoziona kutengeneza dawa ya kung’arisha viatu baada ya kuchukua mkaa Kariakoo na kuusaga na kuchanganya na mafuta. Alisema alitengeneza dawa iliyoitwa ‘Sunshine’ na alivuna mapesa.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.


Aidha alisema kwamba alianzia kutengeneza kalamu ndani ya sebule kabla hajaondoka na kutumia maeneo ya nje kutengeneza kalamu na kasha kuwa na kiwanda kikubwa. Alisema yeye alizaliwa katika umaskini akiishi katika nyumba ya msonge pamoja na wanyama na kuamua kuukataa umaskini. Alisema kilichomsaidia yeye ni kuwa na macho yanayoona Fursa na kuitumia vilivyo kwa kujiamini na kuthubutu. 

Alisema Mungu aliumba kila mtu kuwa namba Moja na ni vyema watu wote wakajiona kuwa namba moja na katika hilo kuthubutu huku wakihakikisha kwamba wanatumia vyema teknolojia iliyopo kwa kufanya matangazo ya biashara zao. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC, Bi. Noreen Mawalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania TWCC Jacqueline Meney Maleko (hayupo pichani) kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wanachama wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa TWCC uliofunguliwa jana jijini Dar es Salaam.

Aliwataka kutumia simu zao kuhakikisha kwamba wanauza na kuzitangaza bidhaa zao huku akiwataka wakue na kuacha kuogopa kuanzisha viwanda. Pia aliwataka kuwa wanyenyekevu katika biashara zao kwani ndio namna bora ya kuendeleza urafiki wa kibiashara kati yao na wadau wanaohitaji huduma au bidhaa zao. 

Alisisitiza utoaji wa bidhaa bora hata kama bidhaa hizo zimelenga kuwasaidia watu maskini na kuwataka kila senti wanayoipata katika biashara kuhakikisha inabaki hukohuko na isichanganywe na matumizi binafsi. Mapema akimkaribisha mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mwenyekiti TWCC, Jacquiline Maleko alipendekeza Chama chake kiwe na ushirikiano na uwakilishi mkubwa kwenye taasisi muhimu za biashara na kuyataka makampuni binafsi nchini yawe yananunua bidhaa za wanachama wao kabla ya kupendelea bidhaa za nje.  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dr. Reginald Mengi kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa TWCC unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Maleko pamoja na kumuomba Dk Mengi, kuipatia TWCC jengo lililopo Sabasaba pia aliitaka TPSF (sekta Binafsi) kuhakikisha kwamba inawazungumzia wanawake na kuwapa nafasi katika vikao vya maamuzi. Pia alifafanua kwamba chama hicho kinataka kushirikishwa katika baraza la biashara la kitaifa na mikoani kwa lengo la kutetea wanawake ambao asilimia 50 ya wafanyabiashara nchini ni wao. 

Maleko alisema chama hicho kilichoundwa mwaka 2005 na kwa sasa kikiwa na majukwaa 11 pote nchini, kimelenga kuunganisha nguvu za wanawake katika kuhakikisha wanashika uchumi kwa kutumia fursa zilizopo za nafasi mbalimbali za wanawake zilizowezeshwa kitaratibu, kama asilimia 5 ya mapato ya halamashauri kusaidia makundi maalumu na asilimia 30 ya zabuni ya manunuzi ya serikali kupewa makundi maalumu. Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Louis Accaro akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of commerce (TWCC) unaondelea katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es Salaam.

Alishauri asilimia hiyo tano kukopeshwa SACCOS yao wanawake ili waweze kukopa na kuendeshea biashara zao, akiamini kwamba fedha hizo zikifikishwa zitawatoa wanawake kiuchumi. Alisema kwa sasa wanawake wafanyabiashara wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya mila, desturi na taratibu za kisheria na hivyo wao ni kazi yao kuhakikisha kwamba sauti ya mwanamke inafika kila mahali ili mazingira ya biashara yaboreshwe. 

Maleko pia alisema kama serikali inaweza kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa kwanini na wao wasipewe ruzuku hiyo ili waweze kuinua uchumi wa taifa. Pia waliomba nafasi katika maeneo ya Taasisi ya viwanda vidogo SIDO kutumiwa na wanawake kuanzisha viwanda vya kusindika vyakula ambapo pia wanaweza kufundishwa na watalamuwa SIDO wakiwa palepale. Meneja mikopo ya wanawake na uwezeshaji wanawake wa benki ya CRDB nchini, Rehema Shambwe akitoa salamu za benki hiyo kwa wajumbe wa TWCC wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam.


Mkutano huo wa mwaka ulifadhiliwa na Mamlaka ya Kodi na Mapato TRA, uilikuwa na wageni wengi wakiwemo watu wa CRDB ambao wanampango wa kuanzisha kituo cha kusaidia wanawake katika masuala ya biashara na ujasiriamali na Trade Mark ambao tayari wanaushirikiano na TWCC. 

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga alisema Asasi yake ipo katika hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wenye thamani ya shilingi bilioni mbili na Chama hicho, baada wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650 kuhitimishwa. Mkataba huo wa mwanzo ulishughulika na mafunzo kwa wajasiriamali katika nyanza zote kuanzia uzalishaji na ufungashaji na matumizi ya hati mbalimbali zinazogusa ujasiriamali.  Mwakilishi wa TRA ambao ndio wamefanikisha kufanyika kwa mkutano huo, Bi. Rose Mahendeke aktioa salamu za TRA kwa wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga akitangaza kuhusiana na hatua za mwisho za kuingia mkataba mpya wa miaka 5 wa thamani ya shilingi bilioni mbili na TWCC, baada wa ule wa mwanzo wa shilingi milioni 650 kuhitimishwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania – Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko akishuhudia Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akiweka kwa maandishi kukabidhi jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wa TWCC kuendeleza ujasiriamali. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha juu na chini ni wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa BOT jijini Dar es Salaam.   Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC), Bi. Jacqueline Mneney Maleko (katikati) kibali cha jengo la maonyesho la IPP ltd lililopo ndani ya viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Biashara jijini Dar es salaam, ili liwasaidie wanachama wake kuendeleza ujasiriamali. Kulia Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Trade Mark East Africa Dr John Ulanga. Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akisalimiana na wajumbe wa TWCC walioshiriki ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD katika picha ya pamoja na wajumbe wa TWCC wanaoshiriki mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea katika ukumbi wa mikutano BOT jijini Dar es Saalaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF Dr Reginald Mengi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP LTD akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Bi. Noreen Mawalla.

NAMNA MAHABUSU,WAFUNGWA WANAVYOTUMIA SEHEMU ZA SIRI KUINGIA NA SIMU, SIGARA GEREZANI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

WAMETAFUTA mbinu mbadala! Ndivyo unavyoweza kuelezea kinachoendelea kwenye baadhi ya magereza yaliyopo nchini kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kwa ajili ya kuingia na simu za mkononi pamoja na sigara.

Sheria za magereza kuna baadhi ya vitu vimepigwa marufuku ikiwamo simu ya mkononi, dawa za kulevya, visu ,nondo na sigara lakini baadhi ya mahabusu na wafungwa wamekuwa wakiingia nazo kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mrakibu Msaidizi wa Magereza, makao makuu kitengo cha sheria Absalom Mokily ameiamba Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika leo alipokuwa kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria inayoendelea jijini Dar es Salaam kuwa kuna mbinu nyingi wanazozitumia mahabusu na wafungwa kuingia na vitu hivyo.

SEHEMU ZA SIRI ZINATUMIKAJE? IKO HIVI .

Akielezea zaidi kuhusu baadhi ya wafungwa na mahabusu kutumia sehemu zao za siri kuingia na vitu ambavyo vimepigwa marufuku , Mokiry amesema wenye tabia hiyo wamekuwa wakijaza mizigo kupitia njia  za haja kubwa na njia ya mkojo.

Amesema kuwa wanaoingia na vitu hivyo hata askari Magereza wanashindwa kubaini kutokana na utaalamu wanautumia kificha vitu hivyo vilivyopigwa marufuku kuingizwa magerezani.

"Unaweza kuwapekua na usione chochote, hivyo unapomruhusu aondoke, anachokifanya anakwenda chooni na kisha kutoa vitu alivyoficha kwenye  sehemu zake za siri,"ameeleza.

Mokily amesema kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Magereza namba 149 ya mwaka 2003 imezuia baadhi ya vitu kuingizwa magerezani.Ametaja baadhi ya vitu hivyo ni ni silaha, simu, visu, nondo, bangi, tumbaku na simu za mkononi."Ni marufuku kuingia na vitu,"amesema.

Amesema kuwa tabia hiyo si tu kwa baadhi ya wafungwa na mahabusu wa kiume tu bali hata wanawake nao wanatabia hiyo kwa kuchukua vitu hivyo na kuficha sehemu zao za siri.

"Wanawake wenye tabia ya kuficha vitu wanachokifanya ni kukimbilia chooni na kisha huvitoa na baada ya hapo utashangaa kuona wanawasiliana na watu walioko nje kwa kutumia simu ambazo wameingia nazo kwa mtindo huo,"amesema.

Amefafanua kuna watu magerezani wamekuwa wakiingia na kutoka , wengine wazoefu magerezani hasa mahabusu.Wanapokwenda mahakamani inakuwa ndio njia ya wao kupata vitu hivyo na kisha kuingia navyo magarezani.

WASHINDWA KUTHAMINI UTU WAO

Wakati huohuo, Mokiry anasema mfungwa anachukuliwa kama binadamu na kubwa zaidi askari magereza wanathamini sana utu wa watu wote lakini baadhi ya wafungwa na mahabusu wameshindwa kuthamini utu wao hasa wakiwa magerezani.

"Unapawakagua huoni chochote lakini ukienda chooni utagundua wameingia na pakiti za sigara na simu na vitu vingine ambavyo haviruhusiwi.Tunashindwa kuwapekua sana kwani unaweza kuambiwa unadhalilisha utu wa mtu lakini wenyewe wamekuwa wakwanza kutothamini utu wao,"amesema.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Mokiry ameongeza mahabusu au mfungwa atakayekamatwa akiwa na vitu hivyo huchukuliwa hatua za kisheria ikiwamo ya kupelekewa mahakamani na ikitokea kuna mtumishi asiye mwaminifu na anayekiuka kanuni huchukuliwa hatua na ikiwezekana anafukuzwa kazi ikibainika ni kweli amehusika kusaidia kuinga kwa vitu hivyo.

MIMBA GEREZANI

Kwa upande wa Mrakibu wa Magereza, Amina Kavirondo  alipoulizwa kuhusu baadhi ya wafungwa na mahabusu kupata mimba wakiwa magerezani, amejibu haijawahi kutokea mwanamke akapata ujauzito akiwa gerezani.

"Kinachotokea wapo baadhi ya mahabusu na wafungwa wanaoingia wakiwa na mimba gerezani na hivyo hujifungulia huko huko na kupata watoto,"amesema.

Amefafanua wafungwa na mahabusu wanawake wanaipongia gerezani wanapimwa afya ili kubaini hali zao na kama mjamzito ripoti hupelekwa Makao Makuu ya Magereza na usimamizi wake kuanzia mwanzo hadi mwisho.

"Mfungwa wa kike akibainia ni mjamzito humpokea na kumtunza  ili kuhakikisha anakuwa salama yeye na kiumbe kilicho tumboni mpaka pale atakapojifungua salama,"amesema Kavirondo.
Mrakibu wa Magereza Kitengo cha Sheria, Absalom Mokiry akifafanua mambo mbali mbali juu ya wafungwa na mahabusu waliopo mahakamani ikiwemo kuingiza simu na vitu vilivyokatazwa gerezani kwa kutumia njia zisizostahili.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO JANUARY 31,2018