Tuesday, January 31, 2017

SERIKALI YAELEZA UTEKELEZAJI WA MASUALA MBALIMBALI BUNGENI




Dodoma, Jumanne, Januari 31, 2017:  

Serikali leo imeainisha utekelezaji na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majibu ya Serikali kwa baadhi ya hoja ni kama ifuatavyo:

                          Ujenzi Nyumba za Walimu.

Akijibu hoja kuhusu ujenzi wa nyumba za walimu, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, ameliambia Bunge kuwa Serikali ilitenga kiasi cha Sh. Bilioni 13.9 katika Bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu wa Sekondari, na Shilingi bilioni 11.4 kwa nyumba za walimu wa Shule za Msingi.

Aidha, Waziri Jafo ameeleza kuwa tayari nyumba 146 za walimu zimeshajengwa nchini kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Pia amezungumzia Serikali kuanza kulipa madeni ya walimu.

                             Ujenzi wa Viwanda Nchini

Akijibu swali kuhusu uwekezaji wa viwanda nchini hususani mkoani Tabora ambako kuna kilimo cha Tumbaku na maeneo mengine yenye malighafi, Mhandisi Edwin Ngonyani kwa niaba ya Waziri wa Viwanda ameliambia Bunge kuwa tayari Serikali imeshafanya mazungumzo na wawekezaji kutoka Vietnam na kuzitaka Halmashauri zote nchini kuendelea kuitikia wito wa kutenga maeneo ya uwekezaji.

“Kituo cha uwekezaji Nchini (TIC) kimepewa maelekezo maalum kunadi fursa hii kwa wawekezaji katika sekta ya tumbaku na sigara hapa nchini,” alisema Mhandisi Ngonyani ambaye pia ni Naibu Waziri, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

                   Tupende Bidhaa Zetu.

Akijibu hoja kuhusu bidhaa nyingi za Kenya kuingia nchini, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba amesema moja ya changamoto inazozikumba bidhaa za Tanzania ni wananchi wake kupenda vya nje.

“Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali iliunda Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti na Kusimamia Uondoaji wa wa Vikwazo visivyo vya Kiforodha na kuhamasisha wafanyabiashara nchini kuzalisha bidhaa zenye ubora,” alisema.

                             Serikali yagharamia 100% umeme vijijini  

Serikali imesisitiza kuwa inagharamia ujenzi wa umeme vijijini kupitia Wakala wa Kusambaza Umeme Vijijini (REA) kwa asilimia 100. Akijibu maswali ya wabunge, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, alisema wananchi wanalazimika kuchangia Sh. 27,000 tu ambazo ni gharama za kodi ili waunganishiwe huduma hiyo wakati mradi ukiwa unaendelea.

“Lengo ni kuhamasisha na kuwawezesha wananchi wa vijijini wenye vipato vidogo kuweza kupata huduma za umeme kwa gharama nafuu,” alisema akisisitiza kuwa wale ambao huomba huduma hiyo baada ya wataalam wa REA kumaliza kazi yao ndio hulazimika kulipia umeme huo kwa Sh. 177,000 tu badala ya Sh. 320,960/- wanazotozwa wakazi wa mijini kwa umbali usiohitaji nguzo.  

                                 Bei ya maji kupungua

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge amesema Serikali itaendelea kupunguza gharama za maji nchini hasa vijijini kadiri gharama za umeme zitakavyoendelea kupungua hasa wakati huu nchi inapoingia katika uchumi wa gesi.

Aliongeza kuwa kwa upande wa vijijini miradi ya umeme wa jua na nishati nyingine za bei nafuu pia itasaidia kupunguza gharama za umeme na kusaidia wananchi kupata maji katika miradi mingi inayondelea sasa nchini.

                                   Madai ya Unyanyasaji Zanzibar

Serikali imewataka wananchi wote wanaodai kufanyiwa unyanyasaji na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutoa taarifa za matukio hayo polisi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema kwa kuwa hakuna  tarifa za kuripotiwa kwa matukio hayo katika kituo chochote cha Polisi, atachukua pia hatua za kutuma maafisa wake kufanya uchunguzi zaidi.















 



RC GAMBO:MAMBO GANI SERIKALI IYAPE KIPAUMBELE ILI KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII?



Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akiingia ukumbini tayari kwa kuanza rasmi kwa kongamano na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa maendeleo katika komgamano hilo.

Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa AICC Elishilia Kaaya akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo na yeye kama mwenyeji wa eneo hilo akiwakaribisha katika kituo hicho.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano ambalo aliwaahidi waandishi kuwa ataliiitisha kwaajili ya kujadili na kupata taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha pamoja na wadaumbalimbali.

Mwenyekiti wa Arusha press club (APC) Akizungumza na katika kongamano hilo.
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza katika kongamano hilo .
Wa kwanza kushoto ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,akiwa kwenye kongamano katika kituo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.
Wadau wa Utalii kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha .
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.
Wa kwanza kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Mussa Juma ,akifuatiwa na Omary Moyo wakiwa katika kongamano hilo.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog
Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha chanel ten Jamillah Omary akiwa na mkurugenzi mwenza wa Me Production ambaye pia ni mpiga picha wa kituo cha luninga cha ITV Anold Rweyemamu.Picha na Vero Ignatus Blog
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia,aliyeko kushoto kwake ni mwenyekiti wa ccm mkoa ndugu Laizer


Na.Vero Ignatus, Arusha.


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua Kongamana kutoa taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha ambapo kongamano hilo limewashirikisha wadau wa habari katika kuangalia na kutafakari na kupitia pamoja na kuangalia mpango mkakati wa maendeleo katika mkoa.

Gambo amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kutoa mrejesho kwa Watanzania kupitia waandishi kwa kipindi cha miezi sita ,na kuangalia mambo gani serikali ikiyapa kipaumbele itaondoa changamoto mbalimbali katika jamii kwa ujumla.

Aidha amesema kuwa utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia desemba 2016 umekuwa na mafanikio makubwa ,ambapo amesema kuwa hii ni kutokana na utamaduni wa kufanya na kutekeleza majukumu ya kazi kwa vitendo.

Amesema utekelezaji huo umechangia katika kuboreka kwa maeneo mbalimbali ya sekta muhimu katika kukuza uchumi katika mkoa hasa pato la mkoa na wananchi moja kwa moja.

“Katika kipindi hiki,miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kupewa kipaumbele cha kutosha hivyo kwa namna moja kutekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (MKUKUTA II)katika mkoa na taifa kwa ujumla”alisema Gambo.

Amesema kuwa Mkoa umesimamia utekelezwaji wa shughuli za serikali na kushuhudia mafanikio katika sekta za kilimo,afya,maji,barabara,mofugo,maliasili na nyinginezo kama takwimu zilivyowasilishwa .

Amesema kuwa serikali imejipanga kuhangaika na wale wote ambao wanachochea migogoro kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hatutawafumbia macho.

Kwa upande wamafanikio utekelezaji wa mkoa kuanzia mwaka 2005 mkoa ulikuwa na shilingi 723,809 milioni kwa mwaka huo mkoa ulikuwa wa (9) katika kuchangia patao la Taifa,ambapo pato la mkazi lilikadiriwa kuwa shilingi 506,902 kwa mwaka sawa na shilingi 1,389 kwa siku.

Kwa mwaka 2010 pato la mkoa wa Arusha lilikuwa shilingi 2,136,514milioni kwa kuchangia pato la taifa Arusha ilikuwa ya 7.mwaka huo pato la mkazi wa Arusha lilikuwa shilingi 1,283,361 kwa mwaka sawa na shilingi 3,516 kwa siku.

Hadi mwaka 2015 pato la mkoa linakadiriwa kuwa shilingi 4,271,447milioni.
kwa takwimu hizo pato la mkazi wa Arusha lilikuwashilingi 2,322,031 milioni kwa mwaka ni sawa na shilingi 6,361 kwa siku.

BOTI YA MIZIGO NA ABIRIA SITA YADAIWA KUPOTEA ZIWA TANGANYIKA,ILIKUWA IKITOKA KIGOMA KWENDA CONGO.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

BOTI ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya Kalemi, imepotea katika ziwa Tanganyika ikiwa na Watu sita pamoja na Shehena ya vitungu gunia 110, ngano mifuko180 ,Mafuta ya taa dumu 20 na kreti za soda 70  ambayo mpaka sasa haijulikani ilipo.

Akizungumza na Wanahabari Mkoani humo kamanda wa polisi  Mkoa wa Kigoma Fredinandi Mtui alisema Mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 16:30 jioni boti iliyotengenezwa  kwa mbao MV.Ngendo ya Buchuma, boti ya mizigo inayo milikiwa na  Mussa Hamisi Mkazi wa ujiji Kigoma Manispaa ,iliondoka  Katika Bandari ya Kibirizi ikiwa na shehena ya vitunguu, Ngano na watu sita kuelekea Congo ambayo mpaka sasa haijafika Congo na haijulikani ilipo.

Mtui alisema mpaka sasa boti hiyo haijulikani ilipo na hakuna chochote kilicho onekana kati ya mizigo wala abiria Waliokuwa wamepanda katika boti hilo, Askali wanamaji wakishirikiana na Chama cha Wamiliki wa maboti Wanaendelea na taratibu za kuitafuta boti hiyo inasemekana imepotelea maji ya Kongo.

Alisema kumekuwa na taarifa zilizo kuwa zikizungumzwa mitaani kwamba  kunamiili imeonekana, taarifa hizo sio za kweli hadi sasa hawajajua kama watu hao watakuwa hai au wamekufa maji, tumewasiliana na Watu waliopembezoni mwa ziwa Tanganyika hawajaona kitu chochote hadi sasa , aliwataka Wananchi kuwa na subira kuweza kutambua kama watakuwa salama au wamekufa.

"baada ya kupata taarifa kuhusu  Boti hiyo iliyokuwa ikielekea Congo kwamba haijafika kwa Muda ulio takiwa,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wamiliki wa Maboti walianza jitihada za kuitafuta boti hiyo maeneo ya mwambao mwa ziwa Tanganyika, na hatujapata taarifa yoyote ambapo ingekuwa imezama mizigo iliyo kuwemo katika boti hiyo ingekuwa imeanza kuelea, tumewasiliana na  Mikoa baadhi ambayo ziwa Tanganyika limepita pamoja na Nchi za Burundi na Congo kupitia ubalozi mdogo waweze kutujulisha endapo wataiona boti hiyo",alisema Mtui.

Nao Baadhi ya ndugu wa Wasafiri walio kuwemo katika Boti hiyo wameanza kutandika msiba kuwaombolezea Ndugu zao waliopotea katika Boti hiyo , Hamis Kakolwa ni mmoja kati ya abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Kalemii Congo.

Mgeni Kakolwa ni Mdogo Wa Hamis Kakolwa alisema Ndugu yao aliondoka siku ya tarehe 21 akielekea Kalemi kupeleka biashara zake, baada ya siku mbili kupita walifanya mawasiliano na watu wa Congo kujua kama boti waliokuwa wakisafiria ndugu yao imefika wakaambiwa haijafika ndipo walipoa anza kuwasiliana na Mmiliki wa boti hilo na kubaini kuwa boti hilo lilipotelea ziwani.

Kakolwa alisema baada ya familia yao kuona hakuna mafanikio ya kuipata boti hiyo kwa siku 7 kupita waliamua kuandaa msiba wa kjmuombolezea ndugu yao kwasababu hawana uhakika kama atapona au amekufa.

SIMUTV: HABARI NA YALIYOJIRI BUNGENI LEO January 31, 2017.

Je, ni lini serikali itaipatia  vifaa tiba hospitali ya wilaya ya Handeni ? Naibu waziri  TAMISEMI, Selemani Jafo anatoa ufafanuzi. https://youtu.be/qgDw0SmDCu4

Ni lini serikali itafanikiwa kumaliza ujenzi wa nyumba za walimu hasa vijijini? Swali kutoka kwake  mbunge Juliana Shonza. https://youtu.be/5keDsCfzmyQ

Je, ni lini serikali itapunguza tatizo la huduma za afya katika wilaya ya Simanjiro? Hapa naibu waziri TAMISEMI, Selemani Jafo anafafanua; https://youtu.be/Zod_cSdfxPc

Serikali ina fikiria nini kuhusu vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na vikosi vya SMZ visiwani Zanzibar kwa raia ? Haya hapa ni majibu ya serikali; https://youtu.be/wj5Xx5r85zY

Je, Serikali imeweka mkakati gani katika kukomesha suala la ubakaji kwa watoto wadogo? Swali kutoka kwa mbunge Lita Kabati. https://youtu.be/CJDSb8zCraY

Serikali ina mpango gani wa kupunguza bei ya maji kwa mkoa wa Shinyanga?  Swali kutoka wa mbunge Salome Makamba; https://youtu.be/soHfcEF3leI

Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha mto Ruaha unatiririsha maji katika bwawa la Mtera kwa mwaka mzima? Haya hapa ni majibu ya serikali. https://youtu.be/ZxumBb-4iro?t=1

Kwanini serikali isinunue miundombinu ya umeme kwa wananchi ili kuwasaidia kupata huduma ya umeme kiurahisi? Haya hapa majibu ya serikali; https://youtu.be/be7VvmLIsgw

Ni lini serikali itajenga kiwanda cha Tumbaku na kusindika asali mkoani Tabora?  Haya hapa ni majibu ya serikali. https://youtu.be/-MZQc1zhIbA?t=5

Fahamu kauli ya Spika wa Bunge Job Ndugai  kuhusu  nyumba nyumba zinazojengwa kwa ajili ya walimu, https://youtu.be/RKYcqc9hCLE 

NEWS

Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Iddi awataka wafanyakazi wa hospitali ya Abdallah Mzee kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi; https://youtu.be/kdJmSugxNBg

Serikali ya Magharibi A yakifunga kiwanda cha usindikizaji ngozi kwa kutiririsha maji machafu katika vyanzo vya maji safi na salama; https://youtu.be/0TmCHjiW0nU

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema umefika wakati wa kuwa na watumishi wenye uweledi katika halmashauri zote nchini; https://youtu.be/gdtXyIb-C-U

Walimu wameshauriwa kutoa ushirikiano kwa wazazi katika kuchunguza juu ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia; https://youtu.be/BKk_xdUL0wk

Rais Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa vikao vya nchi wanachama wa AU; https://youtu.be/tALQ7wK9beo

Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini anusurika kifo baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wilayani Kyela; https://youtu.be/4aCxFZKijJg

Viongozi wa taasisi mbalimbali mkoani Dodoma wametakiwa kuwashirikisha wananchi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo; https://youtu.be/He3bX2JsfeE

ANNA ABDALAH AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE WAWAFUNDE WASICHANA ILI WAWE VIONGOZI BORA WA BAADAYE

 Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 


Na Richard Mwaikenda

MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalla alisema kuwa  hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri. 

Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara  kukutana na wasichana  kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

"Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo 

nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama. 

Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia  Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo  atateuliwa miongoni mwao.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa  ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Wasichana Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda), katikati, na Andriambolamanana Vahatrimama wa Madagascar ambao wapo nchini kaitika programu ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili.wakiwa katika hafla hiyo.
 Wakipiga makofu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Anna Abdalah

 Anna Abdalah akihutubia katika hafla hiyo
 Mmoja wa wabia wa moja kati ya majengo ya TGGA, akisalimiana na Anna Abdalah
 Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shebe akitoa shukrani kwa wajumbe wapya wa bodi na wageni waalikwa kwa kuhudhuria uzinduzi huo.
 Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA pamoja na wanachama wa chama hicho.
 Sasa ni wakati wa msosi




 Wajumbe wa Bodi wakijadiliana jambo na watendaji wa TGGA
 Profesa Qooro akimuaga Zakia Meghji. Katikati ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
 Qooro akigana na Anna Abdalah. Kushoto ni Hangi
Mjumbe wa Bodi Grace Makenya akiaga

SSRA NA TRA ZAKOMBA TUZO ZA UMOJA WA AFRIKA (AU)

Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Freddy Maro, akizungumza wakati akimkaribisha Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi Kasiga.
Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga, akifurahia jambo pamoja na Ofisa Habari wa wizara hiyo, Freddy Maro, wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na TRA jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya Maofisa wa SSRA na TRA, wakiwa katika hafla ya kikabidhi tuzo hizo za Umoja wa Afrika (AU) kwa taasisi hizo.
Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi Kasiga, akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo za Umoja wa Afrika (AU) katika kipengele cha Ubunifu wa mradi wa kazidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na ushindi wa Jumla kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) jijini hivi karibuni.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Taasisi yake ilivyofanikiwa kupata tuzo ya Ubunifu wa mradi wa kazidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii, iliyotolewa na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Bi. Sarah Kibonde, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa tuzo hizo.
Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akielezea namna Mamlaka ya Mapato ilivyofanikiwa kupata tuzo katika kipengele cha Ubunifu wa mradi TANCIS, ambao umeunganisha mifumo midogomidogo ya Forodha na kupelekea kurahisisha utoaji wa huduma na kuongeza ukusanyaji wa mapato, tuzo iliyotolewa na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde (kulia) akiwa na Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.
Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi Kasiga, akifafanua mambo mbalimbali wakati wa kukabidhi tuzo hizo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde na katikati ni Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.


Meneja Mifumo ya Forodha toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bw. Tinkasimile Felix (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa mradi TANCIS, ambao umeunganisha mifumo midogomidogo ya Forodha toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.




Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde, akilifurahia kombe hilo la ushindi wa jumla.
Maofisa wa SSRA, David Nghambi (kushoto) na Ally Masaninga, wakiwa wamelishikilia kombe hilo.

RC SHIGELLA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA MKOANI TANGA,AVITAKA KUONGEZA UZALISHAJI

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Mjini Tanga cha (Unique Steel Mill ) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akiteta jambo na mmoja kati ya wamiliki wa kiwanda cha kuzalisha chuma cha (Unique  Steel Mill) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kulia ni Mhasibu wa kiwanda hicho,Sikander Husein Omari na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akimsikiliza kwa umakini Mhasibu wa kiwanda cha chuma cha Unique  Steel Mill Sikander Hussein Omari  wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akionyeshwa namna chuma zinavyozalishwa kwenye kiwanda cha Unique  Steel Mill) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akitazama namna chuma zinazozalishwa kwenye kiwanda cha chuma cha Unique Steel Mill  wakati wa  ziara yake ya kukagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga  Mhe. Martine Shigella  akitazama namna chuma akiwa amepanda kwenye chuma hizo kuona ubora wake  wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Unique Steel Mill wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Unique Steel Mill  wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akimuonyesha kitu mmoja wa viongozi wa kiwanda cha kuzalishia chuma cha Unique Steel Mill wakati wa  ziara yake ya kukagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili

Picha na habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.