Friday, September 30, 2016

WIZARA YA AFYA YAUPONGEZA MKOA WA SINGIDA KWA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI..

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe (katikati) akizungumza na wagonjwa, kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki na kushoto ni Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya afya Dokta Magreth Mhando.
 Wagonjwa waliofanyiwa operesheni ya macho na madaktari bingwa wakizungumza na Mkuu wa Mkoa (hayupo).
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe (katikati) akizungumza na mgonjwa (hayupo pichani), kushoto kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki.
 Wagonjwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa alipowatembelea na kuona huduma za mkoba za kibingwa zikiendelea kutolewa, wagonjwa hao walikuwa wakisubiri kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akitembelea na kukagua huduma wanazopatiwa wagonjwa wa huduma za kibingwa katika hospitali ya Mt calorus Mtinko, kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki na kushoto ni Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya afya Dokta Magreth Mhando.
.Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akisikiliza maoni ya wagonjwa waliokuwa wakisubiri kupata huduma za kibingwa kushoto kwake ni  Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki na  anayefuata wa kwanza ni Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya afya Dokta Magreth Mhando.

Grace Singida.

Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imeishauri mikoa yote ya Tanzania bara kuiga mfano wa mkoa wa Singida wa kuanzisha huduma za kibingwa za mkoba kwa ngazi za wilaya ili kuwafikia watanzania wengi wenye uhitaji.

Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara hiyo Dokta Magreth Mhando ametoa ushauri huo katika hospitali ya Mtakatifu Calorus Mtinko Singida Vijijini alipotembelea kujionea awamu ya pili ya zoezi la huduma za kibingwa za Mkoba. Dokta Mhando amesema kumekuwa na huduma za kibingwa za mkoba ila hazikufanyika vizuri kama ambavyo mkoa wa Singida umekuwa ukifanya na kutoa pongezi za Wizara kwa Mkuu wa mkoa na Mganga mkuu wa mkoa kwa ubunifu huo.

Amesema huduma za kibingwa za mkoba zimekuwa zikiratibiwa na taasisi au hospital kubwa kama Muhimbili ambapo madaktari bingwa wamekuwa wakitoa huduma kwa ugonjwa fulani na kwa ngazi ya hospitali za Mkoa tofauti na zoezi linaloendelea Mkoani Singida la kutoa huduma za kibingwa kwa magonjwa mbalimbali.

Dokta Mhando ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa madaktari bingwa nchini wizara imetenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari na kuwashauri waajiri ambao ni makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari hao kwakwuwa wizara pekee haitaweza.

Amesema utaratibu ni kuwa na madaktri bingwa angalau watano kila Mkoa lakini mikoa mingi haina idadi hiyo huku akiongeza kuwa lengo la kutembelea zoezi hilo Singida nikujionea hali halisi na sio kusubiria taarifa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe mara baada ya kutembelea wodi zote na kuzungumza na wagonjwa waliopata huduma za kibingwa amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kuongeza muda wa kutoa huduma hiyo kutoka siku tano hadi nane kutokana na wingi wa wagonjwa waliojitokeza.

Mhandisi Mtigumwe amesema huduma hiyo inasaidia kutambua magonjwa na kuyatibu kabla hayajawa sugu lakini pia gharama zikiwa nafuu kutokana na kusogezwa kwa ngazi za halmashauri. Ameongeza kuwa lengo la ofisi yake ni kuhakikisha huduma za kibingwa za mkoba zinapelekwa kwa kila halmashauri na endapo zoezi likikamilika na kukiwa na uhitaji mkubwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudia zoezi hilo.

Mhandisi Mtigumwe amesema kuelekea Tanzania ya viwanda afya bora ni muhimu na wazalishaji wakubwa ni wananchi wa ngazi za chini hivyo huduma hiyo itasaidia kuimarisha afya ili waweze kuzalisha bidhaa kwa wingi na zenye ubora.

Amesema kwa wale wagonjwa watakaopewa rufaa kwenda nje ya Mkoa utaratibu utaangalia wa kuwapatia usafiri wa Mkoa ili kuwapeleka hasa wale wasiojiweza. Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki amesema kwa muda wa siku tano wagonjwa zaidi ya 800 wameonana na madaktari bingwa huku idadi ikitarajiwa kuongezeka kutokana nakuongezwa kwa siku za klutoa huduma.

Dokta Mwombeki amesema wagonjwa wengi wanaofika wanatoka maeneo mbalimbali hasa maeneo ya kijijini na wenye hali duni ya maisha hivyo zoezi hilo limesaidia wananchi hasa wwenye kipato cha chini. Amesema madaktari bingwa wanaotoa huduma za kibingwa za mkoba ni madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, watoto, macho, meno, magonjwa ya ndani na daktari bingwa wa upasuaji.

Wagonjwa waliopata huduma wameushukuru uongozi wa mkoa kwa kubuni utaratibu wa kuwafuata wagonjwa karibu ili kuwapatia huduma za kibingwa kwakuwa inawasaidia kupata matibabu mapema kabla magonjwa hayajawa sugu na kushauri huduma iwe endelevu angalau kila mwaka.

WAZIRI MKUU APOKEA MICHANGO YA SH. MILIONI 190.

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 220 jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 80 kutoka kwa Balozi wa Pakistan nchini, Amir Khan  (wapili kushoto ukiwa ni mchango  kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani  Kagera. 
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na  kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Tasisi ya Aga khan nchini, Amin Kurji (kulia) ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na wapili kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
 Baadhi ya watu walioshiki katika tukio la kukabidhi  jumla ya shilingi 190  ukiwa ni mchango wa   waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza baada ya kupokea mchngo huo kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. milioni 190 kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan.

Fedha hizo zimetolewa ili kusaidiia  wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.

Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo (Ijumaa, Septemba 30, 2016) kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri Mkuu aliwashukuru kwa michango hiyo na alitumia fursa hiyo kuwaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi zao.

“Ninawaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi kwa kuzileta ofisini kwangu au kutuma kupitia akaunti ya maafa iliyofunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz,” amesema.

Amesema watu walio mbali na benki watumie namba za simu zilizotolewa mahsusi kwa ajili ya kupokea michango ya maafa hayo ambazo ni 0768-196-669 (M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).

Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Balozi wa Pakistan, Mhe. Amir alisema wanaamini mchango huo wa sh. milioni 80 walioutoa utasaidia kuwapunguzia uchungu wananchi wa Kagera kutokana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China Mhe. Haodong alimweleza Waziri Mkuu kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari walishawapeleka madaktari na wataalamu wengine mkoani Kagera na leo walikuwa wanakamilisha ahadi yao ya kutoa mchango wa sh. milioni 60.
Naye Muwakilishi Mkazi wa Taasisi za Aga Khan nchini, Amin Kurji  alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 50.                               
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, SEPTEMBA  30, 2016.

RAIS WA SHIRIKA LA ENGENDER HEALTH LA MAREKANI AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR.

 Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiahidi mashirikiano ya karibu na Shirika la Engender Health wakati wa mazungumzo yake na Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Ulla Muller Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Rais wa Shirika la Engender Health la Marekani Ulla Muller ambae pia ni Mtendaji Mkuu (CEO) wa Shirika hilo akizungumza na Waziri wa Afya  Mahmoud Thabit Kombo alipomtembelea Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar, (kulia) ni Mkurugenzi Ufundi ambae ni Naibu mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania Feddy Mwanga. 
 Maafisa waliofuatana na Rais wa Shirika la Engender Health kutoka Ofisi ya Dar es salaam wakifuatilia mazungumzo ya viongozi hao yaliyofanyika Ofisi ya Waziri wa Afya Mnazimmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiagana na mgeni wake Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Engender Health Ulla Muller baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Mnazimmoja Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

SERIKALI KUFANYA MABORESHO KWA KUANDAA SERA YA UBORESHAJI WA VIWANDA VYA DAWA HAPA NCHINI.

 Rais wa Chama cha wafamasia Tanzania (PST) Ndg. Michael Kishiwa (aliyesimama)akitoa taarifa ya Chama kwa kifupi kwa  Mgeni Rasmi Mhe. Mrisho Gambo katika Kongamano la 49 la wafamasia Tanzania linalofanyika Jijini Arusha.
 Wanachama wa PST wakifuatilia ufunguzi wa Kongamano 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitoa hotuba katika ufunguzi wa kongamano la 49 la Chama cha  Wafamasia Tanzania.
Wajumbe wa kongamano wakiendelea kufuatilia Hotuba ya Ufunguzi  katika Kongamano la wafamasia linalofanyika katika Jiji la Arusha.

Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA
SERIKALI kufanya maboresho kwa kuandaa na kuhakikisha Sera ya Uboreshaji wa Viwanda vya Dawa vilivyopo nchini  kwa kuwawezesha na kuwajengea uwezo  wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha dawa na kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo kwa niaba ya Waziri  wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza katika Kongamano la  49 la Chama Cha Wafamasia Tanzania (PST),linalofanyika jijini hapa kwa siku mbili.

Akizungumza kwa niaba ya Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,alisema kuwa kutokana na umuhimu wa sekta hiyo ya dawa, Serikali inaangalia taaluma hiyo kwa macho mawili kwa lengo la kuiboresha ili iweze kutoa huduma bora.

"Wizara yangu inaangalia taaluma hii kwa macho mawili katika kuhakikisha kuwa sekta ya dawa inaboreka na inakua na hatimaye kuweza kukuza uchumi wetu, kwa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha zaidi ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia soko ndani ya nchi na kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi na hivyo kuwa na dawa bora, salama na zenye ufanisi"

"Endapo tutazalisha dawa zetu wenyewe hii itatupunguzia gharama zisizo za lazima kuagiza dawa nje ya nchi, sambamba na hili pia tunaboresha vyuo vya Wafamasia ili waweze kutoka wataalamu bora wa masuala haya ya madawa,”alisema Gambo.

Akizungumzia suala la wizi wa dawa katika hospitali za serikali,alisema kuwa Serikali haina mchezo na yoyote atakayokiuka maadili ya taaluma hiyo na kuwa watawachukulia hatua kali za kisheria ili wananchi wapate huduma bora za dawa.

"Mbali na changamoto ya upungufu wa dawa, wafanyakazi wasio waadilifu ambao wanatumia nafasi zao vibaya wanashirikiana na baadhi ya wafanyabiashara na kuuza  dawa, hili ni suala muhimu PST jadilianeni suala la maadili kwani hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa"alisema

Awali Rais wa PST, Michael Kishiwa, aliiomba Serikali kuongeza udahili wa wanafunzi wa famasia wakiwemo mafamasia wasaidizi ili kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa.

Alisema hivi sasa idadi ya watanzania ni kubwa, lakini wataalamu wa dawa Wafamasia ni 1,200, hali inayochangia kuwepo kwa watoa huduma hiyo wasio na sifa.

Alisema kutokana na kukosekana wanataaluma kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi yao kukiuka maadili na wengine kufanya kazi ya utoaji dawa pasipokuwa na uelewa nayo, hali ambayo hatari kwa afya za binadamu.

Kishiwa alisema kazi kubwa ya chama chao kuhakikisha inasimamia ubora wa utoaji huduma ya dawa na kusimamia maadili, ili wananchi wapate dawa sahihi na kuzitumia ipasavyo.

“Tunashirikiana na baraza la usajili la wafamasia katika kukemea vitendo hivyo vya ukiukwaji wa maadili na ndiyo maana tunaiomba serikali iongeze udahili na vyuo vinavyotoa taaluma hii"alisema
Naye Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabeth Shekalage alisema kwa sasa wananchi wengi wamechukulia huduma ya dawa ni biashara na kuwa baraza limejipanga kupambana na watu wanaofanya huduma hiyo ni biashara huku wakikiuka  maadili.

"Uchache wa wanataaluma unasababisha kika mtu aone hii ni biashara huria na yeyote anaweza kuifanya,kuna uhaba mkubwa wa fundi dawa sanifu,mafundi dawa wasaidizi,dawa ni sumu hivyo tunasimamia hili ili kuepusha madhara kwa watumiaji"alisema Elizabeth
Kongamano la Mwaka huu linaenda na kauli mbiu isemayo kuelezea ubora,usalama,ufanisi na upatikanaji wa huduma bora za kifamasia.

Airtel Tanzania na Puma Energy waunda ushirika.

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso  akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na PUMA utakaowawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma za PUMA kupitia Airtel Money TapTap.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso (kulia) na Meneja mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kusaini makubaliano  rasmi ya  ushirikiano mpya ambao unawawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa kutumia kadi ya “Airtel Money Tap Tap” katika vituo  vya mafuta vya PUMA nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bw. Sunil Colaso (kulia) na Meneja Mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti wakisaini mkataba wa  makubaliano  rasmi ya  ushirikiano mpya ambao unawawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa kutumia kadi ya “Airtel Money Tap Tap” kwenye vituo vyao vya mafuta vya PUMA nchini. Wakishuhudia (kushoto) Meneja Bidhaa wa Puma , Adam Sipe na Meneja Mauzo wa Airtel, Bi Bartleth Omari.
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bw. Sunil Colaso (kulia) na Meneja mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti wakibadilishana mikataba mara baada ya kusaini makubaliano  rasmi ya  ushirikiano mpya ambao unawawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa kutumia kadi ya “Airtel Money Tap Tap” katika vituo vya mafuta vya PUMA nchini kote. Wakishuhudia (kushoto) Meneja Bidhaa wa Puma , Adam Sipe na Meneja Mauzo wa Airtel, Bi Bartleth Omari

 Meneja kitengo cha Airtel Money, Asupya Naligingwa, akitoa maelezo jinsi ya kuweka na kulipa mafuta kupitia kadi ya Airtel Tap Tap  wakati wa uzinduzi wa ushirika mpya kati ya Airtel na PUMA utakaowezesha wateja kulipia bidhaa na huduma zote za PUMA energy kwa kadi maalumu iliyounganishwa na huduma ya Airtel Money ya Tap Tap.  Pichani ni mpiga picha mkuu wa jambo leo,  Richard Mwaikenda akiwekewa mafuta na muhudumu wa kituo cha PUMA oyesterbay  kupitia huduma ya Airtel Tap Tap wakati wa uzinduzi huo
 Meneja kitengo cha Airtel Money , Asupya Naligingwa akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso (kulia) na Meneja mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti  mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Airtel Tap Tap katika vituo vya puma.
 Meneja mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti   akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na PUMA utakaowawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma za PUMA kupitia Airtel Money TapTap

Puma Energy kupokea malipo ya huduma zote na mafuta kupitia Airtel Money Tap Tap.
Airtel Tanzania na Puma Energy Tanzania imezindua rasmi ushirikiano mpya ambao unawawezesha wateja kulipia bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa kutumia kadi ya “Airtel Money Tap Tap” kwenye vituo 46 nchini kote.

Ushirikiano huu sasa utawawezesha wateja wa Airtel na Puma Energy kulipia mafuta na bidhaa nyingine bila kutumia fedha taslimu bali watatumia kadi ya Airtel Tap Tap ambayo imeunganishwa na akaunti zao za Airtel Money.  Huduma hii ni salama na rahisi kutumia inapatikana katika vituo vyote vya Puma Energy nchi nzima,  Huduma ya Airtel Money Tap Tap inatekelezwa kwa awamu 2 ambapo awamu ya kwanza itahusu vituo vyote 20 vya Puma jijini Dar es Salaam na awamu ya pili ni kwa ajili ya vituo vya mikoani kuanzia mapema mwakani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso alisema “Sisi kama Airtel tunafuraha kuanzisha njia hii ya malipo tukishirikiana na kampuni ya Puma Energy Tanzania. Ushirika huu utaleta ushirikiano katika kutanua huduma zetu katika maeneo mengi zaidi na kutoa usalama na uhakika wa huduma bora zaidi kwa wateja wote wa Airtel na Puma Energy kwa masaa 24 na siku 7 za wiki

Tunaamini kuwa ushirika huu na Puma Energy utaongeza ufanisi na kubadilisha maisha ya jamii kuwa bora zaidi kwani wateja wetu wote wataweza kuzipata huduma muhimu kwa urahisi kupitia kadi zao za Tap Tap” aliongezea Colaso

Katika hotuba yake, Meneja mkuu wa Puma Energy, Philippe Corsaletti aliishukuru Airtel Tanzania kwa ushirika huo wa kibiashara na alieleza imani yake katika ushirika huo akisema kwamba itaongeza thamani ya biashara ya rejareja kwa kutoa fursa kwa watumiaji wa Airtel kutumia vituo vya Puma Energy kama sehemu ya kulipia ununuzi wa mafuta na vilainishi vya magari.

Alisema Puma Energy itaendelea kufanya kazi na Airtel na kuhakikisha inapanua upatikanaji wa huduma hii kwa vituo vyote vya mauzo vya  Puma nchini kote. Kufanikisha hili, Bwana Corsaletti aliitaka Airtel kupanua huduma ya Tap Tap katika mikoa mingine nchini.

Thursday, September 29, 2016

Waziri Mkuu MAJALIWA APOKEA MISAADA ZAIDI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni tano kutoka kwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi 18,681,000/= kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja kati ya mabati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Eric Shigongo Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Publishers  (kushoto)  ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisni kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 20 kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Trans Ocean Supplies Limited ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 20 kutoka kwa mtendaji wa kampuni ya Woolworths Tanzania ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 50 kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Pepsi ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Msaada wa viti vya walemavu

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 415,800,000/= kutoka  Chama cha  Waagizaji wakubwa  wa mafuta nchini  (TAUMA ) ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea michango mbalimbali kwa ajili yawaathirika wa  tetemeko la ardhi mkoani Kagera, ofisini kwake jijini Dar es salaam

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea michango mbalimbali kwa ajili yawaathirika wa  tetemeko la ardhi mkoani Kagera, ofisini kwake jijini Dar es salaam
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata picha ya kumbukumbu na wachangiaji  baada ya kupokea michango mbalimbali kwa ajili yawaathirika wa  tetemeko la ardhi mkoani Kagera, ofisini kwake jijini Dar es salaam

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 20 kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Trans Ocean Supplies Limited ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akishukuru baada ya kupokea  mchango wa shilingi 18,681,000/= kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipokea mchango wa shilingi milioni 50  kutoka kwa watendaji wa kampuni ya Pepsi  ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 29, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiCharles Mwijage.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji   wa Kampuni ya Bia Tanzania, Roberto Jarrin (kushoto), Group Corporate Affairs Director wa TBL, Georgia Mutagahywa (wapili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa TBL, Fabian Mwakatuma baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 100 ukiwa ni mchango wa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam