Thursday, March 31, 2016

SERIKALI YAPONGEZA JUHUDI ZA CHUO CHA AGA KHAN KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha kuwa itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi katika kuleta maendeleo kwenye nyanja mbalimbali hapa nchini huku ikipongeza juhudi zinazofanywa na Taasisi ya mtandao ya Aga Khan kwa jitihada zake kufundisha wataalam wa sekta ya Afya.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 31.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga katika ngazi ya digrii katika chuo cha Aga Khan, Jijini Dar es Salaam.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Chuo hicho Kikuu cha Aga Khan kwa kuanzisha shule hiyo wanaongeza idadi ya vyuo vitakavyokuwa vikizalisha kwa wingi wataalam watakaokuwa wakipta digrii kwani awali kulikuwa na upungufu mkubwa.

Jengo la Chuo hicho cha Uuguzi na Ukunga, limefanyiwa ukarabati pamoja na kupatiwa vifaa mbalimbali kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo waliwezesha kwa kugharamia ujenzi wa jengo hilo pamoja na vifaa vya kisasa vya kufundishia.

Kwa upande wake, mgeni rasmi mwakilishi wa Serikali ya Ujerumani, Waziri wa Uchumi na Maendeleo, Dk. Gerd Muller ambaye alibainisha kuwa, wanataka kuona watalaama wengi wa sekta ya afya wanapata elimu ilikuondokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili wanadamu na kuongeza kuwa, bila wataalam wa tiba, Jamii haitakuwa salama.

Aidha, katika tukio hilo,wageni na viongozi mbalimbali walipata kulitembelea jengo hilo pamoja na kushuhudia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea shuleni hapo.

Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
DSC_8632Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
DSC_8640 DSC_8641Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
DSC_8648Baadhi ya wanafunzi na watumishi wa Chuo hicho wakiwa katika tukio hilo
DSC_8653 DSC_8654Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akisisitiza jambo..
DSC_8670Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo..
DSC_8677 DSC_8693DSC_8735Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akitoa maelezo mafupi kabla ya kuzindua rasmi jengo hilo la shule ya wauguzi na wakunga katika chuo kikuu cha Agha Khan..
DSC_8712 DSC_8710Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba ya Serikali namna Wizara Afya itakavyonufaika na wataalam wa sekta ya Afya watakaopata elimu katika shule hiyo
DSC_8737Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akifungua rasmi jengo hilo
DSC_8746 DSC_8748DSC_8721Wageni mbalimbali wakifuatilia tukio hilo
DSC_8761Msimamizi wa shule hiyo ya Uuguzi na Ukunga akitoa maelezo machache kwa wageni mbalimbali..
DSC_8751Picha ya pamoja baada ya ufunguzi huo..
DSC_8766 DSC_8772Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akiangalia namna ya vifaa vya kisasa vya kufundishia jinsi viavyotumika wakati wa kutoa huduma Hospitalini
DSC_8788Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akijaaribu kupata vipimo kuashiria ufunguzi wa jengo hilo pamoja vifaa vya kisasa vilivyowezeshwa na Serikali ya Ujerumani. Kushoto kwake ni Dk. Kigwangalla akimwelezea jambo la kitaalam juu ya vipimo hivyo.
DSC_8805Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari namna Serikali itakavyonufaika kupitia shule hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDD AKARIBISHWA OFISINI KWAKE

 
 Watendaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakimpokea na kumkaribisha kuanza kazi Ofisini kwake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kuteuliwa tena na Rais wa Zanzibar kuendelea kushika wadhifa huo katika kipindi cha Pili cha Awamu ya Saba.
 Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Abdullah Ali Abdullah { Kitole } aliyeinama akinong’onezana kitu na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim kwenye hafla ya kupokea Balozi Seif kuanza rasmi majukumu yake Vuga Mjini Zanzibar.
  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim akimpongeza Balozi Seif kutokana na juhudi zake zilizopelekea watendaji wa ofisi yake kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano iliyopita.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwashukuru watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake baada ya kufanyakazi pamoja atika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Watendaji wa Taasisi za Umma Nchini wanapaswa kuwa makini katika kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha kwenye Taasisi zao ili kuipa nguvu Serikali kuu kuvuka vyema katika kipindi hichi cha mpito.

Alitahadharisha kwamba kipindi hichi hali ya fedha si nzuri kutokana  na mambo mengi yaliyofanywa katika kipindi kifupi kilichopita ikiwemo suala la uchaguzi Mkuu ambalo limelazimika kutumia fedha nyingi.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wawakilishi wa watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake walipompokea rasmi kuingia ofisini kwake na kuanza kazi mara baada ya kuteuliwa tena na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kushika wadhifa huo katika kipindi chengine cha miaka mitano ijayo.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuendesha Taasisi zake za Umma kwa kutumia fedha inazokusanya kupitia vianzio vyake mbali mbali chini ya usimamizi wa watendaji watakaoonyesha uadilifu kwenye usimamizi huo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea kuchukiwa kwake na baadhi ya watendaji wa Umma wenye tabia mbaya ya kuwekeana chuki katika utekelezaji wa majukumu yao yanayowakabili ya kila siku.

Balozi Seif alisema tabia hiyo potofu  inayolaaniwa hata katika imani  na Vitabu vya  Kidini ikiachiliwa kuendelea hatma yake inaweza kuzaa uadui utakaoleta hasara kubwa hapo baadae.

Aliwapongeza na kuwashukuru Viongozi pamoja na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake kwa kazi kubwa waliyoifanya iliyomuwezesha kutekeleza majuku yake ya ufanisi mkubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Balozi Seif aliwanasihi Viongozi na watendaji hao kuendelea kushirikiana na kushikamana kwa kufanya kazi kama ndugu wamoja ili kazi ya Utumishi waliokabidhiwa na Taifa ifikie malengo yaliyokusudiwa.

Alisema zipo kasoro, changamoto na hata mikwaruzano iliyojitokeza na kupelekea kukoseana baina ya baadhi ya watendaji na Viongozi hao akiwemo na yeye pia ndani ya kipindi kilichopita cha miaka mitano. Hivyo njia pekee ya kuzishinda changamoto na kasoro hizo ni kusameheana ili kufuta kasoro hizo.

Mapema Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim kwa niaba ya watendaji wa Ofisi hiyo amempongeza Balozi Seif kwa kuteuliwa tena kushika wadhifa huo. 

Nd. Ahmad alisema ndoto na dua za Viongozi na Watendaji wa Taasisi za Ofisi hiyo zimesibu kwa Mwenyezi Muungu aliyempa ilham Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kumteua tena Balozi Seif kuendelea kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Alisema ahadi waliobeba Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ni kushirikiana nae bega kwa bega kadri ya uwezo wao kiutendaji ili kufanikisha majukumu yao kwa upeo mkubwa zaidi.

 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
31/3/2016

Dk. Pallangyo awakaribisha wazawa kwenye uzalishaji wa umeme

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati Dk. Juliana Pallangyo (pichani) akifungua mkutano unaoshirikisha wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme.
 Sehemu ya watendaji na wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani).
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) na  Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Decklan Mhaiki (kushoto) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mwenyekiti wa kamati ya nchi za kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya  umeme, Josh Chifamba (hayupo pichani)
 Mwenyekiti wa kamati ya nchi za kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, Josh Chifamba (kulia) akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) aliyekuwa mgeni  rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (aliyekaa mbele katikati) akiwa  katika picha  ya  pamoja na sehemu ya  watendaji na wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, mara baada ya  ufunguzi wa mkutano huo.


Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk Jualiana  Pallangyo amewataka wawekezaji binafsi nchini kujitokeza kwa wingi na kuwekeza katika uzalishaji na uuzaji wa nishati ya umeme  nchini ili  iweze kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Dk. Pallangyo alisema hayo kwenye mkutano unaokutanisha wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme. Nchi hizo ni pamoja na  Bostwana, Msumbiji, Afrika ya Kusini, Lesotho, Namibia, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Swaziland, Zambia na Zimbabwe. Lengo la mkutano huo wa siku moja lilikuwa ni kujadili changamoto zinazozikumba nchi wanachama katika uzalishaji  na uuzaji  wa umeme ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu.

Aliongeza kuwa  wawekezaji binafsi wanaweza kuzalisha   umeme kupitia  vyanzo mbalimbali vya nishati ikiwa ni pamoja na maporomoko madogo ya maji, upepo, bayomasi na  jua kutokana na uwezo wao.

Akielezea fursa za uwekezaji nchini, Dk. Pallangyo alisema kuwa wawekezaji wanaweza kuwekeza  kupitia ujenzi wa miundombinu ya usambazaji  wa umeme, uendelezaji wa miradi ya umeme unaotokana na maporomoko madogo ya maji na  vyanzo  vingine  ikiwa ni pamoja na jotoardhi, upepo na uanzishwaji wa viwanda vidogo kwa ajili ya utengenezaji wa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme.

Dk. Pallangyo aliongeza kuwa ushiriki wa  sekta binafsi  katika sekta ya umeme umeongezeka kila mwaka na kusisitiza kuwa serikali bado inaendelea na mikakati ya kuwawezesha wawekezaji binafsi  katika  uzalishaji ya umeme nchini.

Aliongeza kuwa serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini  ikiwa ni pamoja na sera na sheria mbalimbali  zinazotumika kama mwongozo na kutaja kuwa ni pamoja na sheria ya umeme ya mwaka  2008, sera ya nishati ya mwaka 2003 ambayo inahamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika sekta ya umeme.

Alitaja sheria nyingine kuwa ni pamoja na ile ya Mamlaka ya Udhibiti  wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ya mwaka 2001, sheria ya  Wakala wa Nishaji  Vijijini (REA) ya mwaka 2005.

Akielezea mikakati ya serikali katika upatikanaji wa nishati ya  uhakika, Dk. Pallangyo alisema kuwa serikali imeweka mkakati wa  kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 75 ya wananchi wote hasa waishio  vijijini wanapata nishati ya umeme ambayo ni ya uhakika.

“Tunatarajia kuzalisha hadi   megawati 10,000 za umeme ambao utachochea ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia viwanda na hivyo nchi kutoka katika kundi la nchi masikini duniani na kuwa  katika kundi la nchi zenye kipato cha kati  duniani,” alisisitiza Dk. Pallangyo.

Akielezea hali ya upatikanaji wa umeme nchini, Dk. Pallangyo alisema kuwa umeme unaozalishwa ni megawati 1461.69 huku mahitaji halisi yakiwa ni megawati 1026.

Umoja wa  nchi zinazoshirikiana katika sekta ya umeme kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool; SAPP) ulianzishwa Agosti mwaka 1995 katika Mkutano wa  Umoja wa Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la  Sahara (SADC) ambapo walisaini makubaliano kwa ajili ya  kushirikiana katika uzalishaji na biashara ya  umeme wa pamoja.

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA INTANETI, AfPIF 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba akielezea matumizi ya intaneti yalivyo nchini na changamoto zinazowakabili watumiaji wa huduma hiyo. 

Mwaka 2016 unakuwa mwaka wa neema kwa Tanzania kupata fursa ya kuandaa Mkutano unaowakutanisha wadau wa intaneti (African Peering and Interconnection Forum), mkutano unaotaraji kufanyika Agosti 31 – Septemba 1, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi amesema mkutano huo unalengo wa kukutanisha wadau mbalimbali wa intaneti ili kutanua miondombinu ya intaneti katika bara la Afrika.

Amesema taasisi yake inapenda kuona huduma ya intaneti ikipatikana kwa urahisi kwa watumiaji wake Afrika na hivyo kupitia mkutano huo wataweza kutazama jinsi gani wanaweza kushirikiana na kubadilishana takwimu za watumiaji wa mitandao kwa bara zima la Afrika.

“Tunatambua kuwa watumiaji wa intaneti wanazidi kuongezeka na kupitia mkutano huu tutaweza kuangalia jinsi gani tunaboresha huduma ya intaneti iwe bora ili iweze kutumiwa na watu wengi zaidi,” amesema Mwangi.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba amesema mkutano huo una umuhimu kwa Watanzania kwa kupata fursa ya kujifunza na kubadilishana mawazo na watu kutoka mataifa mengine katika huduma ya intaneti.

Amesema kwa sasa Tanzania bado ina changamoto nyingi katika huduma ya intaneti na kupata nafasi hiyo ya kuandaa mkutano kutakuwa na faida kwa mashirika yanayotoa huduma ya intaneti ili kuwawezesha kutambua ni jinsi gani wataboresha huduma kwa wateja.

“Nchi yetu inawatumiaji wengi wa intaneti ila bado kuna changamoto nyingi ikiwepo usalama wa mtandao na serikali inafanya jitihada nyingi kumaliza changamoto hizo na kupitia mkutano huu tunaamini utasaidia zaidi Watanzania kupata kitu kipya katika huduma ya intaneti,” amesema Simba.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary amesema Watanzania wengi bado hawajafahamu umuhimu wa intaneti kutokana na kutokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu intaneti lakini kupitia mkutano huo ulioandaliwa na Internet Society wataweza kuapata elimu mpya kuhusu intaneti.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary.
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba (kushoto), Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary, Meneja Mradi wa Tanzania Internet Exchange (TIX), Frank Habicht na Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi wakizungumza jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mwenyekiti wa TISPA, Vinay Choudary akifungua mkutano huo.
Meneja Mwandamizi wa Maendeleo wa Taasisi ya Internet Society, Michuki Mwangi akizungumzia mkutano wa Intaneti, AfPIF utakaofanyika nchini, Agosti, 30 - Septemba, 1
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo.



Baadhi ya waandishi waliohudhuria mkutano huo.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

THE BEAT FESTIVAL @ SLIPWAY MSASANI DAR ES SALAAM THIS FRIDAY


FRIDAY 01. April - 21.00 - 02.00 
Venue: Paparazzi Club, Slipway - Msasani Bay, Dar es Salaam
Entrance: 10.000 TSH only
  SIKINDE – Dance orchestra / Tanzanian rumba

Formerly known as DDC Mlimani Park Orchestra, Sikinde is one of the greatest Tanzanian dance bands of all time. Although the group was first formed in 1978 they embody the sound of independence, which took place in Tanzania in 1961, since the founding members came from the pre independence groups Dar es Salaam Jazz Band and the workers union band Ottu Jazz Band. While many of the older orchestras in Tanzania have lost or replaced many of their founding members, Sikinde is perhaps the oldest orchestra who still have most their founding members in their group. Don't miss this opportunity to see one of Tanzanias greatest orchestras performing classic Tanzanian rumba lead by the charismatic lead singer Hassan Bichuka.
MOPOA JAZZ TRIO – Afro Jazz
This trio is lead by Jazz guitarist Emmanual Abraham Mopao who is steadily becoming one of the authorities on the Dar es Salaam Jazz scene. Towards the end of last year he released his first solo album and toured with his trio project as the opening act for the Mzungu Kichaa tour in Germany and Denmark. He is a self taught and hard working musician, inspired by African Jazz stars such as Jimmy Dludlu and Hugh Masekela as well as the American Jazz standard traditions. His performance is based on improvisation and is a rare treat for Dar es Salaam Jazz enthusiasts.
KIFIMBO – Afrofusion / Reggae
Kifimbo is a reggae-afrofusion artist from Dar es Salaam who is respected on the Tanzanian reggae scene for his high energy on stage. His up-tempo songs never seize to put his audience in a good mood. He is based in Bagamoyo where he does different farming activities when he isn’t doing music. He performed his first performance at THE BEAT last year and surprised us all with his high-energy performance. We look forward to welcoming him back to THE BEAT!
BLACK FIT – Reggae / Dancehall
Hussein Badru Hussein, whose artist name is Black Fit, started his musical career in 1995 while he was still a “street boy”. He gained experience through participating in Street festivals and managed to record his first album “Harakati za Mweusi” in 2014. In 2007, he participated in one of the biggest Festivals of that time, held at the “Makumbusho Village Museum, “YA KALE YANAPOKUTANA NA YA SASA FESTIVAL”, and won 3rd prize which boosted his name on the scene. In 2009 he won the first prize during the same festival. Flack Fit has been studying at Music Mayday with an EU scholarship, perfecting his skills in both performance and self management through their 2 year music program. 
ABOUT THE BEAT: The Beat is a monthly festival showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is powered by: Caravan Records, Paparazzi Bistro Club, Jameson, and Goethe Institut Tanzania. Info: CRTanzania@gmail.com web:www.facebook.com/TheBeatFestival

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAVUTIWA NA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBON



Barabara za kuingia na kutoka katika Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam zinavyoonekana, wakati Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo limekamilika kwa asilimia 99.9 na litaanza kutumika rasmi kuanzia Aprili 16.
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia) akibadilishana mawazo na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja ala Kigamboni, Karim Mataka wakati Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea dalaja hilo.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja ala Kigamboni, Karim Mataka wakati Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea dalaja hilo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni.


Meneja Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi, Karim Mataka akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu barabara zinazoingia katika daraja hilo, wakati walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wake jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi, Karim Mataka akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Ufafanuzi kwa Wabunge.
Meneja Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi, Karim Mataka akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu jijini Dar es Salaam jana, walipotembelea kuangalia ujenzi wa daraja hilo linalotarajiwa kuzinduliwa Aprili 16. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Norman Sigala na kulia ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula.
Muonekano wa barabara za kuingia katika daraja la Kigamboni.
Darala la Kigamboni linavyonekana baada ya kukamilika kwa asilimia 99.9.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Norman Sigala.
Wabunge wa Kamati hiyo wakipata ufafanuzi kutoka kwa Meneja Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi, Karim Mataka.