Wednesday, September 30, 2015

UPENDELEO WA KISHERIA KWA NYUMBA YA MAKAZI KABLA YA KUNADISHWA.

KUSOMA  ZAIDI  links  goes  to  sheriayakub.blogspot.com
Na  Bashir  Yakub.
KISHERIA  haizuiwi  kuweka  rehani  nyumba  ya  makazi  kwa  ajili  ya  kupata  mkopo  kutoka  taasisi  yoyote  ya  fedha. Jambo la msingi  sana  ni  kuwa  watoa  mkopo   wajiridhishe   na  umiliki  wa  nyumba  hiyo  hasa  kwa  kuangalia ikiwa  ni  mali  ya  familia  au  hapana ili wachukue  hadhari  za  kisheria.

Nyumba  ya  makazi  ni  ipi.  Nyumba  ya  makazi  ni  ile  nyumba  ambayo  inatumiwa  na  binadamu  kuishi  lakini  zaidi  wanaoishi  mle  ndani  iwe  ni  familia  ya  mchukua  mkopo.  Yawezekana  nyumba  ikawa  ni  ya makazi kwa  watu  wengine  lakini  ni  ya  biashara  kwa  mchukua  mkopo. Kwa  mfano  nyumba  za  kupanga  ambapo  mwenye  nayo  anaishi  kwingine   na nyumba  iko  kwingine ikiwa  na  watu  wengine.

 Nyumba  ya  namna  hii  haitaingia  kwenye  nyumba  ya  makazi  kwa  tafsiri  hii.  Hata  hivyo  haitarajiwi  mchukua  mkopo  kuhamia  kwenye  nyumba  ambayo  sio  ya  makazi  kwa  makusudi  na kuifanya  ya  makazi  akilenga   kuhadaa  ili  kupata  upendeleo  wa  mahakama.  Akifanya  hili  atakuwa  amedanganya  na  ni  kosa  kama  tutakavyoona.

1.MAKOSA  YA  KISHERIA  KWA  MKOPAJI.
( a ) Sheria  ya  masuala  ya  rehani  ya  2008  inamtaka  mkopaji  kutofanya  udanganyifu  wa  aina  yoyote  kwa  taasisi inayotarajia  kumpa mkopo. Moja  ya  udanganyifu  ni  kama  ilivyoelezwa  hapo  juu  lakini  pia  upo  udanganyifu  mwingine  mwingi  ambao hufanywa  na  wakopaji. Kwa  mfano  kuweka  rehani  nyumba  moja  kwa  taasisi  tofauti,  kudanganya  nyumba  sio  ya  familia  wakati  ni  ya  familia  na  udanganyifu  mwingine  mwingi  ambao  hulenga  kumnufaisha  mkopaji.  

2. ADHABU  YA  KUTENDA KOSA  LA  UDANGANYIFU  KATIKA  KUCHUKUA MKOPO.
Kisheria  tendo  likishakuwa  kosa  ni  lazima  iwepo  adhabu  yake.  Vivyo  hivyo  mkopaji  kumdanganya  mkopeshaji  nalo  ni  tendo  ambalo  huadhibiwa. Sheria  inasema  kuwa  hatia  ya udanganyifu  wa mkopaji   inapotangazwa  basi  adhabu  yake  ni  kulipa  faini  ambayo  ina  thamani  ya  nusu ya  mkopo  aliokuwa  amechukua. Hii  ina  maana kuwa,  kama  alichukua  mkopo  wa  milioni  200  basi  faini  yake  ni  milioni 100  halikadhalika  kama  alichukua  milioni  kumi  basi  faini  yake  ni  milioni tano.
Ikiwa  hana  hizo  hela  basi  itatakiwa  kwenda  jela  kutumikia  kifungo  kisichopungua  miezi  kumi  na  mbili. Kifungo  kisichopungua  miezi  kumi  na  mbili  maana  yake kinaweza  kuzidi miezi  kumi  na  mbili kutegemea  na  ukubwa  wa tatizo  lenyewe.  Hivyo  wakopaji  wajihadhari  na  kutoa  taarifa  za  uongo  hasa  kudanganya  kuwa  mali  si  ya  familia  au  kutumia  mali  moja  kuchukulia  mkopo  sehemu  zaidi  ya  moja n.k.

3.  UPENDELEO  KWENYE  NYUMBA  YA  MAKAZI
( a ) Sheria  inasema  kuwa   iwapo  itabainika  kuwa  nyumba   iliyowekwa  rehani  ni ya  makazi  na  mkopaji  analeta  zuio la  kutouzwa   nyumba  hiyo  basi  mahakama  ikijiridhisha  na  hilo  inaweza  kukubali  ombi  hilo.

Mahakama  itakubali  ombi  hilo  la  kuzuia  nyumba  kuuzwa  kwa  kuzingatia  kiwango  cha  hela  kilichosalia  yaani kile kiasi  ambacho   mkopaji  ameshindwa  kulipa. Mara  kadhaa  hutokea  kuwa  mkopaji  amelipa  kiasi  kikubwa  na  kusalia na  deni  la kiasi  kidogo  ambacho  kwa   akili  ya  kawaida  tu  na kutokana  na  mazingira  yaliyopo  akipewa  muda  mwingine  anao  uwezo  wa  kulipa  na  kumalizia  kabisa  deni. Ni  katika  mazingira  haya  zuio  la  kutouzwa  nyumba   ya  makazi  litakubaliwa.

( b ) Hili  litakwenda  sambamba  na  kuangalia  iwapo  wajibu  wa  mkopaji  uliowekwa  katika  mkataba  wa  mkopo unaweza  kuzungumzika. Ikiwa  mkopaji  alikuwa  mgonjwa  sana  na  ushahidi  upo  na  hivyo  alishindwa  kuendelea  na  biashara  na  hivyo  kutokurejesha, na sasa  ana  afya  njema  na  anaweza  kufanya  biashara  na  kurejesha, basi  wajibu  wake ikiwa  unaweza kurekebishika  kwa  namna  hiyo  au  namna  nyingine mahakama inaweza  kutoa  zuio  ili  kutoa  nafasi  nyingine  kwa  mkopaji.

( c ) Pia  ikiwa mahakama  itajiridhisha   kuwa  nyumba  husika  ina  thamani kubwa  kiasi  kwamba hata   mkopaji  akiongezewa  muda  mwingine  bado  akishindwa  kulipa  huko  mbeleni   nyumba  husika  ikiuzwa  mtoa  mkopo  hatakuwa  na  hasara  ataweza  kurejesha  hela  yake  yote pamoja  na  riba,  basi  zuio  la  kutouza  linaweza  kutolewa  kwa  kulizingatia  hilo.
Izingatiwe  kuwa  zuio  katika mazingira  haya  niliyoeleza   linawezekana  ikiwa nyumba  ilyowekwa rehani  ni  ya  makazi.
MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

MAENDELEO ENDELEVU 17 YA DUNIA YAZINDULIWA TANZANIA

IMG_3349
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.
SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.
Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.
Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
IMG_3303
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.
Akizungumza umuhimu wa malengo hayo, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia , serikali zimekutana na kukubaliana kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu. Malengo haya yatasaidia mataifa yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi, kupunguza matumizi na kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.Katika hilo watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”
Akizungumzia malengo hayo Bw. Paul Kessy amesema kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kwa malengo hayo.
Alisema kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa New York, Marekani kwa ajili ya kutia saini malengo hayo na hilo linaonesha ni kiasi gani serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau wengine kuufuta umaskini.
Pia alisema:“Wakati huu, masuala ya uimarishaji wa muundo wa utekelezaji na kuamsha upya ushirikiano wa kidunia katika maendeleo ni msingi mzuri”
Naye Kamishina wa mipango wa Zanzibar, Bw Ahmed Makame : “Nikiangalia malengo haya 17 ya SDGs, ninafuraha kuona kwamba Zanzibar imekuwa sehemu ya mchakato huu...”.
IMG_3392
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akipozi kwa picha na lengo na tisa kabla ya uzinduzi rasmi wa Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu.
Aidha alisema kwamba Tanzania imeanza vyema katika utekelezaji wa malengo hayo.
Alisema kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika malengo ya milenia, inaonekana namna bora ya kuuoanisha malengo ya kitaifa na ya dunia.
Ninafurahi kusema kwamba Zanzibar tuko katika mchakato wa kutengeneza mkakati wa maendeleo wa kitaifa na tumepanga kufikia malengo ya SDGs.
Akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo, Bi.Fionnuala Gilsenan, amesema taifa lake Ireland lipo tayari kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
“Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya. Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Project Everyone, Bi. Liz Lloyd alielezea umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania katika kusambaza ujumbe wa malengo ya dunia.
IMG_3397
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akipozi la lengo namba 3.
“Kama benki huwa tunazungumza na umuhimu wa kuendelea kuwapo. Huu si tu msemo bali ahadi tunayoishi nayo kila siku. Malengo ya Dunia yanatoa nafasi adhimu ya ushirikiano na taasisi kubwa duniani, kutekeleza malengo 17 kwa nia ya kufufua ushirikiano wa dunia kwa maendeleo endelevu.
Standard Chartered inajisikia furaha ya kuwa nchini Tanzania kwa miaka mingi na inatumaini kwamba kwa ushirikiano huu kila mtu anayeishi nchini hapa atafaidika na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”
Malengo ya Maendeleo Endelevu yalizinduliwa Septemba 25 wakati viongozi wa dunia walipokutana pamoja mjini New York. Malengo haya yataanza kutumika Januari 1,2016.
IMG_3226
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akipozi na lengo na 17.
IMG_3280
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya uzinduzi rasmi wa malengo hayo nchini Tanzania.
IMG_3390
Mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza (kushoto) sambamba na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama katika picha ya ukumbusho.
IMG_3789
Meza kuu katika halfa ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) nchini Tanzania, kutoka kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd.
IMG_3781
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3554
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akielezea ushiriki wa benki yake katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3580
Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy akizungumza kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3640
Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame akiwakilisha serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
IMG_3772
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo.
IMG_3754
Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka mashirika na balozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
IMG_3796
Baadhi ya wageni waalikwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakifuatilia maoni na maswali yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3829
Mmoja wa wawakilishi wa vijana akiuliza swali meza kuu.
IMG_3868
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akijibu moja ya swali lililoulizwa na kijana (hayupo pichani).
IMG_3857
Sehemu ya wadau wa Maendeleo, taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_3851
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali na majibu.
IMG_3900
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia), Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame ( wa pili kulia), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahaya (wa pili kushoto) kwa pamoja wakifunua pazia maaluma kuashiria uzinduzi rasmi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3912
Sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_3921
Shamra shamra za uzinduzi zikiendelea.
IMG_3950
Fataki zikisherehesha uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3975
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko na wadau mbalimbali wa maendeleo, waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na vibao vya malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3997
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha jamii kuhusiana na malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_4021
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_4029
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mwanahabari mkongwe Mama Eda Sanga walioshiriki kwenye uzinduzi huo.
IMG_4097
Bendera ya Umoja wa Mataifa, SDG's na bendera za nchi mbalimbali zikipepea kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
IMG_4078

WASIMAMIZI NA WARATIBU WA UCHAGUZI MIKOA YA IRINGA MBEYA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA UPENDELEO KWA WAGOMBEA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)
Na Kahema Emanuel,Mbeya

WITO umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.


Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo. 


Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia  vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.


Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.


Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.


Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura  ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni  sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.
Baadhi ya wakurugenzi na Maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.




Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Sanif Khalifan akitoa maelezo kwa washiriki wa semina ya mafunzo ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,Wasimamizi wa uchaguzi ,Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na Maafisa wa uchaguzi Halmashari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.Picha JAMIIMOJABLOG


Daniel Kalinga Afisa Uchaguzi akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku mbili ikihusisha waratibu wa uchaguzi,Maafisa Uchaguzi ,Maafisa wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi Halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa .



Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo.




NEC: HAKUNA WIZI NA UDANGANYIFU WA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi  wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akiteta jambo na Kamishna wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Vincent Msena wakati wa mkutano baina ya NEC na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu nchini uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Pwani Hussein Kibindu akisoma taarifa ya mada ya tathimini ya uchaguzi mkuu wa oktoba 25 mwaka huu wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Mwanza, Alfred Kapole akichangia mada wakati wa mkutano mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mkalimani wa lugha ya alama, Kudra Munishi akitoa ufafanuzi wa mada na hoja kwa watu wenye ulemavu wa kusikia wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA).

Na Ismail Ngayonga MAELEZO
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  imevitoa wasiwasi  vyama vya siasa  kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 Oktoba, mwaka huu.
AIdha NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.

Jaji Lubuva alisema hadi kufikia sasa, vyama vyote vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo vimefanyika kampeni za kistaarabu ingawa katika siku za hivi karibuni baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa kauli na matamshi yaliyovuka mipaka, ambapo NEC imevionya vyama kuacha mara moja tabia hiyo.

“Vipo baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao  wamekuwa wakitumia muda mwingi kutoa lugha zisizofaa baada ya kunadi sera ya vyama vyao, vyama hivyo tumekutana nao na kuwataka kuacha mara moja kampeni za aina hiyo” alisema Jaji Lubuva.

Jaji Lubuva alisema tarehe 27 Julai mwaka huu, vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu vilisaini maktaba wa maadili ya uchaguzi huo, hivyo ni wajibu wa vyama hivyo kuzingatia viapo walivyotoa katika maktaba huo.

Akifafanua zaidi Jaji Lubuva alisema iwapo chama chochote hakina hoja ya kuzungumza na  wananchi ni vyema kikawa kimya hadi siku ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba mwaka huu.
Aidha Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuingilia masuala ya utawala ya tume hiyo, kwani kwa kufanya hivyo vyama hivyo vitakuwa vikifanya kazi za tume hiyo na hivyo kuingilia masuala ya ndani ya kiutendaji ya taasisi hiyo.

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Lubuva alisema mahitaji yote ya msingi ya uchaguzi huo tayari yamepokelewa na NEC ikiwa karatasi, wino, na masanduku ya kura ambapo baadhi yake yameanza kusafirishwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kuhusu Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva alisema katika kipindi cha siku 10 zijazo kuanzia sasa Tume hiyo inatarajia kusambaza daftari la kudumu katika mikoa yote nchini na wananchi watatakiwa kuhakiki majina yao katika kipindi cha siku 8.

Tuesday, September 29, 2015

SIMU TV:HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mgombea uraisi kupitia Ukawa Edward Lowassa amaliza kampeni zake mkoani Tanga huku akiahidi kujenga bandari mkoani humohttps://youtu.be/_VvUDJlBU8Q

Tanzania yazindua malengo 17 ya dira ya maendeleo ya millennia ikiwemo kutokomeza umasikini na usawa wa kijinsia. https://youtu.be/b6z2XKKCmlQ

Mahakama ya Rufaa kanda ya Tabora yaanza kikao chake chini ya jopo la majaji 3 kutolea uamuzi jumla ya kesi 39. https://youtu.be/j3ZU2YaFEoM

Mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia Chadema aachiwa kwa dhamana baada ya kutiwa mbaroni kwa kuanzisha vuruguru kuzua Msafara wa Dkt.Magufulihttps://youtu.be/gA5Up8AHfFE

Kati ya usalama wilayani Masasi yakanusha taarifa za uzushi zilizo zagaa mitandaoni juu ya kukamatwa kwa makasha ya kura. https://youtu.be/zoNOTN-_hhE

Watu 1000 wadaiwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu na wengine 17 kupoteza maisha jijini Dar es salaamhttps://youtu.be/s-FyuxFhVEo

Ligi ya mabingwa barani ulaya inelendelea kutimua vumbi huku klabu ya Barcelona ikiingia uwanjani bila nyota wake tegemeo Lionel Messi. https://youtu.be/bzQI-mi7yfw

Klabu ya Azam Fc yatoa saa 72 kwa TFF kutoa hukumu dhidi ya madai ya uzalilishaji wa mchezaji wake John Bocco. https://youtu.be/klB-3XzaVtU

Tume ya taifa ya uchaguzi NEC,imetangaza kuwachukulia hatua wagombea na wapambe wao wanao tumia majukwaa kutoa lugha za matusi.https://youtu.be/rN83TTGWyNs

Magufuli amaliza ziara yake ya kampeni mkoani Iringa na kuanza ziara mkoani Dodoma huku akikemea siasa za kikabila. https://youtu.be/vGXVPG1N8Dw

Kiongozi wa mbio za mwenge taifa awahimiza wajasiriamali nchini kuongeza thamani ya bidhaa zao ili ziweze kupata soko ndani na nje ya nchihttps://youtu.be/fvFiLz9ELTk

Makamo wa Raisi Dr.Bilali aongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa morogoro wakiwemo viongozi wa serikali katika mazishi ya marehemu Celina Kombani.https://youtu.be/PuhNSCBpUNM

Tume ya taifa ya uchaguzi yalaani matumizi ya lugha za matusi katika kampeni zinazo endeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchinihttps://youtu.be/DRsTs6qEnM4

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yapinga hoja ya serikali ya mkataba inayopigiwa chapuo na vyama vya upinzani huku ikidai itavunja muungano.https://youtu.be/e8hSl06h_94

Tanzania yaungana na jumuiya ya kimaifa kuadhimisha siku ya afya ya moyo duniani kwa kutoa huduma ya upimaji moyo na magonjwa yasiyo ambukizwa.https://youtu.be/CRfxN9aG9A4

Wakazi wa Arusha wachukua tahadhari dhidi kipindupindu kwa kufanya usafi dhidi ya meneo yenye mikusanyiko ya watu kama sokoni. https://youtu.be/bd5GDcV5QF8

Serikali ya Ujerumani yaikabidhi majengo ya kufundishia wanafunzi wa utabibu wa jeshi la wananchi wa Tanzaniahttps://youtu.be/PXTCJPEKsrg

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NA KUTOA VIFAA TIBA KWA MANISPAA YA KONONDONI

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam na kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu katika Manispaa ya Kinondoni. (Picha na Francis Dande).
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika Dar es Salaam.
Baadhi ya Mameneja na Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipundupindu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay. (Picha na Francis Dande).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipundupindu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya na wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipundupindu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Aziz Msuya.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB
 Vifaa tiba vilivyokabidhiwa leo.


  Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imekabidhi dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 15 kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.

Msaada huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Injinia Mussa Natty aliyeishukuru benki hiyo na kukiri kwamba kipindupindu kipo katika manispaa yake.

Akizungumza baada ya kupokea dawa na vifaa tiba hivyo, injini Natty alisema mpaka sasa ugonjwa huo umepoteza maisha ya watu 17 katika manispaa hiyo huku wengine 1194 wameugua kipindupindu. 

“Kata zote 34 za manispaa ya Kinondoni zimeathirika na kipindupindu kilichoanzia Mwananyamala Agost 15 mwaka huu kata nyingine zenye ugonjwa huo ni Mburahati, Kigogo, Sinza, Mabibo, Magomeni, Kimara na Manzese.

"Mpaka sasa kambini kuna wagonjwa 25 nawashauri watanzania waache kusalimiana kwa kushikana mikono sababu ugonjwa huu unaendezwa kwa uchafu,” alisema injinia Natty.

Dk. Kimei alisema wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa kila mwaka na benki hiyo viongozi wa CRDB kutoa huduma kwenye matawi mbalimbali huku akieleza kwamba kaulimbiu ya mwaka huu ni Asanteni Sana.

“Wateja wetu ndio jambo la kila jema linalotokea kwetu… tunaitumia wiki hii kufungua milango na kusogea karibu zaidi na wateja ili kusikiliza maoni, mahitaji na ushauri wao, lengo ni kuwahudumia kwa ubora zaidi,” alisema Dk. Kimei.