Tuesday, June 30, 2015

BANDA LA NSSF LAWA GUMZO MAONYESHO YA KIMATAIFA YA 39 (SABASABA) VIWANYA VYA MWALIMU NYERERE DAR ES SALAAM

Mmoja wa wateja waliotembelea Banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba akihudumiwa na Meneja Kiongozi Masoko na Ushirikiano wa, Bi. Eunice Chiume (wa kwanza kulia mbele).  Mmoja wa wateja waliotembelea Banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba akihudumiwa na Meneja Kiongozi Masoko na Ushirikiano wa, Bi. Eunice Chiume (wa kwanza kulia mbele).Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakitoa huduma katika Banda lao kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba.  Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakiwa katika Banda lao kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tayari kwa kuwahudumia wateja wao.Baadhi ya wateja kwenye banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiangalia machapisho anuai ndani ya banda hilo. Baadhi ya wateja kwenye banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiangalia machapisho anuai ndani ya banda hiloBaadhi ya wateja kwenye banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiangalia vipeperushi anuai ndani ya banda la NSSF. Baadhi ya wateja kwenye banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiangalia vipeperushi anuai ndani ya banda la NSSF. 
------------------------------------------
WANACHAMA wote wa NSSF na wasio Wanachama Mnakaribishwa kujionea na kupata huduma mbalimbali zikiwemo, taarifa za jumla zinazohusu kujiandikisha uanachama, uwekezaji unaofanywa na Shirika, Maelezo kuhusu Bima ya afya itolewayo na NSSF,na kupata Kadi mpya. 
 Wageni wote wanaweza kujua kuhusu namna ya kuwasilisha maoni yao kupitia mfumo wetu mypa wa HaapyOrNot uliopo katika ofisi za Kinondoni, Ilala, Temeke na GDE- Waterfront Kwa kutumia mfumo huo mwanachama na asiye mwanachama anaweza kutuambia amefurahia huduma au Hapana pindi anapotembelea Ofisi za NSSF. 
 Pia wastaafu wote wanaofaidika na Pensheni za NSSF wataweza kupata pensheni kupitia mfumo mpya wa HIFADHI SMART ambapo mstaafu ataweza kupata fedha zake sehemu yoyote. 
 Vilevile wanachama na wasio wanachama mnakaribishwa ili muweze kujua kuhusu Huduma yetu mpya ya HIFADHI FASTA ambayo mwanachama sasa anaweza kulipa michango yake kupitia mtandao wa SELCOM wireless hivyo kumrahisishia yeye kuepuka usumbufu wa kutembea umbali mrefu ili aweze kuwasilisha michango yake.

TIMU YA WATU 21 YA KAMPUNI YA KUCHIMBA DHAHABU YA ACACIA WASHUKA KUTOKA MLIMA KILIMANJARO,WACHANGISHA MILIONI 800 KWA AJILI YA ELIMU TANZANIA.

Timu ya watu 21 ya wafanyakazi ,Ndugu na Marafiki wa Kampuni ya kuchimba dhahabu ya Acacia wakishuka kutoka mlima Kilimanjaro ambako walipanda kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia elimu.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu ya Acacia,Brad Gordon akiwa na Meneja wa Ustawi wa kampuni Asa Mwaipopo wakifurahia mara baada ya kushuka toka kaika kilele cha Uhuru ambako watu 19 kati ya 21 ndio walifanikiwa kufika kileleni.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia,Necta P Foya akishangilia wakati akishuka toka mlima Kilimanjaro.
Timu ya watu 21 iliyopanda Mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Kuchimba Dhabu ya Acacia wakiwa katika Uniform maalumu wakielekea lango la kutokea katika mlima la Mweka huku wakiimba nyimbo mbalimbali .
Mkuu wa wilaya ya Tarime ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika mapokezi ya timu ya watu 21 iliyopanda mlima Kilimanjaro,G;orious Luoga (wa tatu toka kushoto) akiimba na wapandaji hao.
Wapandaji wakiimba mara baada ya kufika katika lango la Mweka,hapa wakiongozwa nyimbo mbalimbali na mmoja wa asakari wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kiliamanjaro.
Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ,Brad Gordon akifurahia na wafanyakazi wa kampuni hiyo,Meneja wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma,Necta Foya na Fredrick Njoka .
Timu ya watu 21 waliopanda mlima Kilimanjaro,wakiwa katika picha ya Pamoja katika lango la Mweka mara baada ya kushuka toka Kilele cha Uhuru.
Baadhi ya washiriki wa zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime ,Glorious Luoga akiteta jambo na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia,Deo Mwanyika akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi kwa timu iliyoshiriki kupanda Mlima Kilimanjro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya shule za Msingi.
Mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorious Luoga akizungumza katika hafla hiyo.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Acacia ,Brad Gordon akikabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha Shilingi Milioni 8,000,000 kwa mkuu wa wilaya ya Tarime ,Glorious Luoga ,zilizochangwa kupitia mpango wa CanEducate kwa ajili ya kusaidia elimu Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorious Luoga akiwa amenyanyua juu  mfano wa Hundi.
Kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Charles Ngemba akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya timu ya watu 21 wakiwemo wafanyakazi ,Ndugu na marafiki wa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia.

Na Dixon Busagaga wa Globu 

ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

TANAPA MEDIA AWARDS 2014

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akimkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Sarakikya akiwa na mkewe kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerali Sarakikya pia  amepewa Kadi maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia yake, lakini katika hatua nyingine  atalipiwa gharama zote za kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi duniani  yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa  mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerali Mrisho Sarakikya  amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo  ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali  wamepewa tuzo hizo. Katika picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
Meneja  wa Mawasiliano TANAPA Bw. Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Fredy Sikagonamo mwandishi bora wa  habari za utalii vipindi vya redio katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Magessa Maggesa  mwandishi bora wa habari za utalii kwa vipindi vya Televisheni kutoka Stars TV katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jimmy Mengere kutoka Chanel Ten  Morogoro, mwandishi bora wa habari za utalii kwa habari za Utalii aliyeandika kuhusu wanyama wanavyouwawa kwa ajali katika mbuga ya Mikumi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Kasilda Mlimila Mwandishi bora wa habari za utalii za Televisheni kutoka Star TV Morogoro  kwa kuandika kukauka kwa mto Ruaha Mkuu , kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jackson Kalindimya Mwandishi bora wa habari za Utalii Magazeti  katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Humphrey Mganga  mwandishi bora wa habari za utalii katika magazeti katikati ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh Baraka Konisaga

 Mwenyekiti wa jopo la Majaji TANAPA MEDIA AWARDS,Dkt.Ayub Rioba.


 Katibu Mkuu wa  Maliasili na Utalii

















Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mh.Lazaro Nyarandu



Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati, Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya Gold Crest.



Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh.Baraka Konisaga

 Mwenyekiti wa jopo la Majaji TANAPA MEDIA AWARDS,Dkt.Ayub Rioba