Sunday, May 31, 2015

taswira kutoka kwenye mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mjini Abijah, Ivory coast

Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika,Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali akitetajambo na Mawaziri wa Fedha mbalimbali waliohudhuria mkutano huo Mjini Abijah-Ivory coast.
Baadhi ya Marais wa Afrika waliohudhuria mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mjini Abijah-Ivory coast.
Rais wa Benki wa Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka akiwa kwenye kikao na Magavana wa Afrika wakijadiliana changamoto mbalimbali za maendeleo zilizojitoketeza katika nchi za Afrika Mjini Abijah- Ivory coast.
Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali akisikiliza majadiliano kwenye kikao cha magava wa nchi za Afrika wakati wa kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo Mjini Abijah-Ivory.
Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicus B.Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa majadiliano pamoja na Mkurugenzi Mkuu Bw. Gabrriel Negatu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Abijah-Ivory coast.
Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji akitoa ufafanuzi kwa Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Ngosha Magonya akiwa pamoja na Afisa Mwandamizi Bw. John L. Sima Mjini Abijah-Ivory Coast.
Kamishina wa Fedha za Nje Bw. Ngosha Magonya akitoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali yanayohusu Benki ya Maendeleo ya Afrika katika miradi mbalimbali ya Tanzania Mjini Abijah- Ivory Coast. Aliyekushoto kwake ni Gavana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Servicus B.Likwelile ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali.
Kamisha wa Fedha za Nje wa Zanzibar Bi. Bihindi N.Khatibu akiwa kwenye mkutano siku ya kufunga kwa mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)Mjini Abidjan-Ivory Coast.
Rais Mpya wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akihutubia na kutoa shukrani kwa wajumbe kwa kuchanguliwa kuwa rais wa benki hiyo Mjini Abidjan-Ivory Coast.
Rais Mpya wa Benki wa Maendeleo ya Afrika(AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina akiwa pamoja na baadhi ya marais kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB) Mjini Abidjan-Ivory Coast.(Picha zote na Scola Malinga-Abidjan).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA MARIAN BAGAMOYO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, kwa pamoja wakikata utepe kuzindua Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, kwa pamoja wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian, baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo Mei 31, 2015 mjini Bagamoyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, baada ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo na baadhi ya viongozi na waumuini baada ya kuzindua rasmi Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkandarasi wa majengo ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian wakati akitembelea kujionea ramani ya Chuo hicho baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo mjini Bagamoyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya waumini wa Dini ya Kikristu, baada ya uzinduzi wa Chuo hicho uliofanyika leo chuoni hapo mjini Bagamoyo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo.

MWANAHABARI DEOGRATIAS MONGELA ALIVYO UKACHA UKAPERA

 Mwanahabari Deogratias Mongela wa Kampuni ya Global Publishers Ltd.
 Bibi Harusi, Elizabeth Sanga.
 Deogratias Mongela akiwa na mke wake Elizabeth Sanga wakati wa hafla ya ndoa yao iliyofanyika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana baada ya kufunga ndoa Katika Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mbezi Luis Dar es Salaam jana.
 Maharusi hao (katikati) wakiwa na wapambe wao kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Cobson Nzige na mke wake Subira Nzige (kulia), 'hakika wamependeza si mnawaona'.
 Bibi harusi Elizabeth Sanga akiteta na mpambe wake Subira Nzige.
 Mama mzazi wa Bwana harusi, Asia Kapori akiwahasa 
maharusi hao.
 Mjomba wa Bwana harusi, Karim Mtambo na pia 
akiwahasa maharusi hao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akimpongeza bwana harusi Deogratias Momgela baada ya kuoa. Wengine ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo (katikati), akijumuika na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mhariri, Amrani Kaima na Oscar Ndauka wa kampuni hiyo.
 Mama mzazi wa Deogratias, Asia Kapori akiwasalimia wageni mbalimbali kwenye sherehe hiyo.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Wageni waalikwa wakipata kinywaji kwenye hafla hiyo.
 Mwanahabari Kulwa Mwaibale wa kampuni hiyo akiteta jambo
 na Bwanaharusi.
 Maharusi hao wakiwa katika picha ya pamoja na 
wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Maharusi na wapambe wao wakiserebuka pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani), (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

STARTIMES KUANZA KUONYESHA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA U20

Na Dotto Mwaibale

WAPENZI  wa soka nchini sasa watafaidi kwa kutazama michuano ya kombe la dunia chini ya miaka 20 mwaka 2015 moja wa moja kwenye luninga zao kupitia ving’amuzi vya StarTimes pekee.

Michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi tarehe 30 mwezi Mei na kumalizika tarehe  20 mwezi Juni  mwaka huu moja kwa moja kutoka nchini New Zealand ambapo timu 24 za vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani yatachuana kuwania ubingwa.

Akizungumza baada ya kupata haki miliki kutoka kwa FIFA za kutangaza michuano hiyo maarufu duniani ambayo hubeba mastaa wa baadae kwa timu zao za taifa, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa wanafuraha kubwa kuonyesha michuano hiyo kwani soka ni mchezo unaopendwa zaidi duniani.

“Tunayofuraha kubwa kuwatangazia wateja wetu kuwa tumepata haki miliki kutoka FIFA za kuonyesha michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka 20 mwaka 2015 itakayofanyika nchini New Zealand. Soka ni mchezo unaopendwa zaidi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla na tunaamini tutawapatia wateja wetu burudani ya matangazo yenye ubora wa hali ya juu kupitia ving’amuzi vya StarTimes.” Alisema Bi. Hanif

“Itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi ya New Zealand kuwa wenyeji wa michuano hii ambayo inalenga kuyakusanya mataifa pamoja na kukuza umoja na amani. Wapenzi wa soka wataweza kujionea mechi 52 kutoka kwa timu 24 tofauti. Mchezo wa kwanza utapigwa tarehe 30 Mei ambapo utamkutanisha mwenyeji New Zealand na Ukraine, mechi itakayoonyeshwa moja kwa moja katika chaneli ya StarTimes Sports 2 inayopatikana katika ving’amuzi vyote vya dishi na antenna.” Aliongezea

“Ninachoweza kusema mwaka huu kwetu StarTimes ni wa bahati kubwa sana kwani tumeweza kufanya maboresho makubwa katika vipindi vyetu hususani vya michezo. Mbali na michuano hii pia kuna mingine mingi inakuja kwenye king’amuzi hiki hivyo wapendwa wateja wetu wakae mkao wa kula,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo nawaomba wateja wetu walipie na wale wasiojiunga wafanye hivyo sasa ili wasipitwe na uhondo huu.”


Katika michuano hiyo bara la Afrika linawakilishwa na timu za vijana wa chini ya miaka ishirini kutoka nchi za Senegali, Mali, Ghana na Nigeria. Huku barani ulaya ni Ureno, Ujerumani, Austria, Ukraine, Hungary na Serbia; kwa bara la Amerika ni Marekani, Mexico, Honduras, Panama, Colombia, Brazil, Ajentina na Urugwai; bara la Asia ni Qatar, Myanmar, Uzibekistani na Korea ya Kaskazini; na pia visiwa vya Fiji na New Zealand ambao ni wenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARADHI YA FISTULA YATUA WILAYA YA KIBONDO

Mkazi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Esther Batolomea akisoma kipeperushi chenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Wakazi wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwamba iliyopo Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma walijumwika na wakazi wa wilaya hiyo katika viwanja vya Community Centre wakimsiliza Meneja Biashara wa Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon wakati alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na maradhi ya Fistula. Wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea kufanyika katika mikoa mitatu nchini,Kampeni hiyo inaendeshwa na Hospitali ya CCRBT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Balozi wa maradhi ya Fistula nchini Msanii Mrisho Mpoto alimaarufu”Mjomba” akitoa elimu kwa wakazi wa Kibonda kuhusiana na maradhi ya fistula na kuwasihi wakina baba kuwaruhusu wake zao wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Alitoa elimu hiyo wakati wa kampeni inayoendeshwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na CCBRT ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea katika mikoa mitatu nchini. Inakadiriwa wastani wa wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wanapojifungua.

JAMBO LEO YAICHABANGA BODABODA FC TAMASHA LA BODABODA UKONGA

 Mlinda mlango Maganga Benjamin wa timu ya Bodaboda Wilaya ya Ilala, akiudaka mpira katikati ya wachezaji wa timu ya Jambo Leo 'Wagumu Stars' Zahoro Mlanzi (kushoto) na Ali Salum wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa. Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 Moja ya kizazaa langoni mwa Bodaboda FC iliyosababishwa na washambuliaji wa Jambo Leo
 Mshambuliaji wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, Ali Salum (katikati) akifunga bao la kwanza dhidi ya Bodaboda FC,wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
Slaa akiwasalimia wachezaji wa timu hizo mbili
 Wachezaji wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, wakifanya mazoezi ya kupasha mwili muda mfupi kabla ya kuvaana na timu ya Bodaboda FC ya Wilaya ya Ilala, wakati wa Tamasha la Bodaboda kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam leo. Katika mechi hiyo, Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 Kikosi cha timu ya Gazeti la Jambo Leo kilichopambana na Bodaboda FC
 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kulia), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, muda mfupi kabla ya timu hiyo kukipiga na timu ya Bodaboda FC ya Wilaya ya Ilala, wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam jana.Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.

 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda FC , muda mfupi kabla ya timu hiyo kukipiga na timu ya Gazeti la Jambo Leo, wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam
 Silaa akitoa mawaidha kwa timu hizo kabla ya mechi kuanza


 Mchezaji wa timu ya Jambo Leo,  Frank Balile (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Bodaboda, Sharif Mohamed