Saturday, January 31, 2015

MEYA MANISPAA MOROGORO, WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe ( wa kwanza kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro , Said Amanzi , wakipita eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
Gari la Meya likiwa halitamaniki.
Wasamalia wakimuwahisha Hospital,Mmoja wa majeruhi mara baada ya kupata ajali eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .
Hili ndilo basi lililogongana na Gari ya Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ,(45) akiwa amelazwa wodi namba tano ya daraja la kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari yake SM 4151 ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam ,mbali na Meya huyo na watu wengine watatu ,Dereva Mwambala Ally (55), na waandishi wa habari , Anita Chali (30) pamoja na HUSSEIN Nuha (28) pia walijeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu. ( Picha na John Nditi).
Mwandishi wa habari,Anita Chali akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari waliyoipata,walipokuwa kwenye kazi na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akionesha eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kupimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.

Na John Nditi ,Morogoro

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro , Amir Nondo (45), dereva  na waandishi  wa habari wawili wamepata ajali   baada ya  gari walilokuwa wakisafiria kugongwa na basi la abiria lenye namba za usajili T 831 CEH, aina ya Scania mali ya kampuni ya Happy Africa na kujeruhiwa  sehemu mbalimbali za miili yao na kulazwa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu majira ya saa 9: 30 alasiri , eneo la Msamvu Mzambarauni darajani katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, ambapo basi hilo lilikuwa likotokea mkoani Njombe.

Majina ya watu hao wengine waliojeruhiwa na kulaza katika wodi za daraja la kwanza katika hospitali ya rufaa ya mkoa , ni dereva wa gari la Meya, Mwambala Ally (55) , na waandishi wa habari ambao ni wapigapicha vituo vya televisheni , Anitha Chali (30) pamoja na Hussein Nuha (28).

Mstahiki meya huyo  aliyekuwa kwenye gari ya Halmashauri ya Manispaa hiyo  yenye namba za usajili SM 4151, ikiendeshwa na Mwambala  ambamo pia walikuwemo waandishi wa habari hayo na alikuwa katika msafara wa ziara ya kikazi ya mkuu wa mkoa huo,Dk Rajab Rutengwe.

Meya Nondo akizungumzia  ajali hiyo, akiwa wodini akipatiwa matibabu  ,sambamba na majeruhi wengine alisema baada ya kufika eneo la Mizambarauni, Darajani, lilichomoka pembeni basi la abiria ililokuwa likitokea Njombe kuelekea  Dar es  salaam, na kuligonga kwa mbele gari alilokuwemo.

Mashuhuda wa ajali hiyo  waliwaambia waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio,  kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni basi la abiria mali ya kampuni ya Happy Africa, kuingilia msafara huo wa mkuu wa mkoa uliokuwa ukielea mjini baada ya kukagua shughuli za ujenzi wa vyumba vya maabara na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bigwa katika  Shule ya Sekondari Sumaye.

Mkuu wa mkoa kwa takribani wiki mbili amekuwa katika ziara katik halmashauri saba za mkoa huo kwa ajili ya kukagua shughuli za ujenzi na umaliziaji wa maabara tatu kwa kila shule ya skondari ya Kata na pia kutumia fursa hiyo kujitambulisha , kusikiliza kero na kuzipatia majawabu ya msingi.

Januari 29 na 30 mwaka huu ilikuwa ni zamu ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Shule ya sekondari Sumaye kilikuwa ni kituo chake cha mwisho katika ziara hiyo na baadaye kufanyika kwa majumuisho ya ziara hiyo Januari 31, mwaka huu mjini Morogoro.

Hata hivyo baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya mkoa , viongozi mbalimbali walifika kuwajulia hali  wakati wakiendelea kupatia matubabu na madaktari mbingwa wa hospitali hiyo, akiwemo Mganga mkuu wa mkoa , Godfrey Mtei.

Mstahiki Meya Nondo ameumia sehemu ya kichani na mkononi , wakati na mpiga picha Anita Chali, ameumia  kichwani, huku dereva pamoja na  Hussein wakiumia zaidi  kwenye paji la uso na kichwani huku Hussein akisaidiwa na mashine ya kupumulia (oxygen).

 Kufuatia tukio hilo Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa imesema itatoa taarifa ya ajali hiyo  jumamosi ya  Januari  31, mwaka huu.

Friday, January 30, 2015

NAPE AANZA AMSHA-AMSHA YA MIAKA 38 YA CCM MJINI SONGEA

 Wananchi wakiwa katika shamrashamra za kumpokea Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Ruvuma mjini Songea leo, alipowasli kwa ajili ya kuanzisha amsha amsha ya Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM ambayo inafanyika Jumapili hii, Kitaifa mjini Songea kwa kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
 Mratibu wa Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Emaanuel John Nchimbi akiwasili kwenye Ofisi hiyo ya CCM mkoa wa Ruvuma leo kumpokea Nape
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza wananchi kwenda katika maeneo mbalimbali kuzindua mashina ya Wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutano wa hadhara, baada ya kuwasili leo mjini Songea
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza wananchi kwenda katika maeneo mbalimbali kuzindua mashina ya Wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutano wa hadhara, baada ya kuwasili leo mjini Songea
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza wananchi kwenda katika maeneo mbalimbali kuzindua mashina ya Wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutano wa hadhara, baada ya kuwasili leo mjini Songea
 Vijana wakiwa wameacha shughuli zao kumshangilia Nape alipokuwa akipita mitaani mjini Songea wakati akienda kufungua mashina ya wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutnao wa hadhara
 Mwanamke akihanikiza kwa vigelegele kumshangilia Napa wakati wakipita kwenye moja ya mitaa maarufu ya mjini Songea wakati akienda kufungua matawi ya Wajasiriamali wa CCM na kuhutubia mkutano wa hadhara
 Kina Mama wakimshangilia Nape wakati akipita kwenye mita hiyo
 Nape akiwashukuru wananchi waliokuwa wakimshangilia wakati wakipita kwenye mitaa hiyo leo
 Baadhi ya viongozi wakimsubiri kumlaki Nape kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Songea mjini leo
 Nape akisalimiana na viongozi kwenye Ofisi hiyo ya CCM wilaya ya Songe mjini
 Nape akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM Songea mjini leo
 Nape akikata utepe kuzindiuashina la wakereketwa wajasiriamali wa CCM katika Stendi ya mjini Songea
 Nape akipandisha bendera ya CCM kuzindua tawi hilo la CCM kwenye Stendi ya mabasi mjni Songea
 Nape akimsalimia Mjumbe wa Shina namba 12, Margareth Mtivila,  Songea mjini
 Nape akipandisha bendera kuzindua shina la wakereketwa wajasiliamali wa CCM Liziboni mjini Songea
 Ofisi ya CCM iliyozaa shina hilo la wakereketwa ilizinduliwa na Paul Sozigwa
 Nape akimkabidhi kadi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Hadija Nyoni, baada ya kuzindua shina hilo. Jumla ya Vijana 89 walikabidhiwa kadi hizo
 Nape akizindua tawi la CCM Liziboni

 Nape akizindua Mradi wa Ujenzi wa mabanda ya Biashara Kata ya Lisiboni
 Nape akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kuzindua ujenzi wa mradi wa vibanda hivyo vya Biashara, Liziboni
 Nape akiingia kwenye jengo la Ofisi ya CCM tawi la Mji Mwema, wilaya ya Songea mjini
 Nape akipaka rangi kwenye Ofisi hiyo ya CCM tawi la Mjimwema
 Nape akiwa katika picha ya pamoja na vijana wajasiriamali wa mradi wa kufuga kuku Mjimwema
 Nape akifungua shina la Wajasiriamali wa CCM Mjini Mwema
 Nape akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Ruwiko
 Nape akitoa pole kwa familia ya askari wa Magereza, wakati wa maziko ya askari huyo katika kata ya Ruwilo, wilaya ya Songea  mjini
 Nape akitazama picha ya askari huyo ambaye amefariki kwa ajali
 Nape akiwapa pole ndugu wa Marehemu huyo
 Nape akizindua shina la Wakereketwa wa CCM, tawi la Chuo Kikuu cha St. Joseph Songea mjini
 Bibi Riziki Ngonyani (92) wa mjini akishangilia wakati wa uzinduzi wa shina hilo la St. Joseph
Nape akiagana na baadhi ya viongozi wa CCM shina la Chuo Kikuu cha St. Joseph mjini Songea. Picha na Bashir Nkoromo

ZIARA YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII KWA SOKO LA MAREKANI YAENDELEA LOS ANGELES

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi akiongea katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (kulia) akiwa pamoja na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.
Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki ziara maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi akiwasilisha mada inayohusu vivutio vya utalii nchini katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ndege ya Emirates Ndg. Akbar Hussein akiongea juu ya namna gani unaweza kufika Tanzania kwa kutumia usafiri wa Emirates.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ndege ya Ethiopian Airlines akiongea juu ya namna gani unaweza kufika Tanzania kwa kutumia usafiri wa Ethiopina Airline.
Baadhi ya washiriki wa hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani iliyofanyika katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi akiongea na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kwa soko la Marekani iliyofanyika katika Hoteli ya Four Seasons jijini Las Vegas.
Mwakilishi wa Ethiopian Airline (kati) akiongea katika hafla hiyo.Wengine pichani ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii (TTB) Bi. Devota Mdachi.