Monday, December 29, 2014

MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MKE WA JAJI ANTONY BAHATI

Mwalimu Laurentia Bahati enzi za uhai wake.
Kitabu cha kumbukumbu.
Waombolezaji wakiweka saini katika kitabu cha kumbukumbu.
Waombolezaji wakiweka saini katika kitabu cha kumbukumbu.
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kufundishwa na marehemu mwalimu Laurentia Bahati wakimfariji mtoto wa marehemu, Angela Bahati (kushoto).
Mwalimu Omari akimpa pole jaji mstaafu, Antony Bahati kwa kufiwa na mke wake.
Waombolezji wakipata chakula.
Wakati wa chakula.
Wakati wa chakula.
Wanafamilia  na waombolezaji wengine wakiwa nyumbani kwa marehemu, Oysterbay.
Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu.
Wanafamilia.
Wanafamilia.
Jaji Bahati (katikati) akiwa na watoto wake.
Picha ya marehemu.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi akitoa heshima za mwisho.
Baadhi ya wanafunzi waliofundishwa na mwalimu Laurentia Bahati enzi za uhai wake wakitoa heshima za mwisho.
Watoto wa marehemu wakitoa heshima za mwisho.
Mtoto wa marehemu, Angela Bahati akitoa heshima za mwisho.
Mtoto wa marehemu, Thomas akitoa heshima za mwisho.
Mtoto wa marehemu, Angela Bahati akiwa na mtoto wake, Antony.
Waombolezaji wakiwa kanisani.
Mwili wa marehemu ukiwasili makaburini.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (katikati) akiwa na waombolezaji wengine.
Jaji mstaafu, Antony, Bahati akiweka shada la maua katika kaburi la mke wake, Laurentia Bahati wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni.
Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Agustino Ramadhani akiweka shada la maua.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi akiweka shada la maua.
Jaji mstaafu Antony Bahati akiondoka makaburini baada ya mazishi ya mke wake, Laurentia Bahati 
Watoto wa marehemu wakiwa katika picha ya pamoja.
Jeneza likishushwa kaburini.
Jaji mstaafu, Antony Bahati akiweka udongo katika kaburi la mke wake, marehemu Laurentia Bahati 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akiweka shada la maua pamoja na mke wake.
Mtoto wa marehemu, Angela Bahati na mume wake wakiweka shada la maua.
Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva.
Wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja.
Wajukuu wa marehemu wakiweka mashada ya maua.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Charles Kitwanga (kulia) akiwa na baadhi ya walimu waliowahi kufanyakazi na marehemu enzi za uhai wake.
Waombolezaji wakiwa nyumbani.
Wanafamilia wakiwa Kanisani.
Jaji Mark Bomani (wa pili kushoto) akitoa heshima za mwisho.
Padri Kizito Ngogoti SAUT-Mwanza akibariki Kaburi la marehemu Laurentia Bahati ambaye alikuwa mke wa Jaji mstaafu, Antony Bahati wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva (kushoto) akimpa pole Jaji mstaafu, Antony Bahati wakati wa mazishi ya mke wake, Laurentia Bahati yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa wanafamilia, Abdul Njaidi akitoa utaratibu wakati wa ibada ya mazishi. 
Padri akiweka maji ya baraka katika jeneza la marehemu Laurentia Bahati.

Kampeni ya “Wait to Send” yaendelea Mkoa wa Pwani na Morogoro

Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (kulia) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini. Akisikiliza kwa makini ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto).
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (kushoto) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia).
Dereva wa basi liendalo Morogoro, John Peter, akisoma kauli mbiu ya usalama barabarani ya mwaka 2014 katika fulana kabla ya kukabidhiwa fulana hiyo na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) pamoja na stika yenye ujumbe unaohamasisha madereva kutokutumia simu zao za mkononi wakati wanaendesha magari ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika zoezi lililofanyika leo katika mikoa ya Pwani na Morogoro. Wakishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Abigail Ambweni (wa pili toka kulia) na Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (wa tatu toka kulia).
Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akisisitiza jambo kwa abiria wa basi liendalo Iringa wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Morogoro leo kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini,Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, PC Twaima Othman (kushoto) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Abdallah Omari (wa tatu toka kushoto) kwa kutumia kifaa maalum wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Pwani leo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” ya Vodacom Tanzania inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (wa pili toka kushoto).

Kampeni ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe,leo imeendelea katika Mkoa wa Pwani na Morogoro.

Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Vilevile polisi wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani ambako ni barabara kuu inayotumiwa na magari mengi yaingiayo na yatokayo jijini Dar es salaam walitoa elimu kwa abiria jinsi ya kutoa taarifa waonapo vitendo vya madereva wanaondesha magari kwa uzembe na kuhatarisha maisha yao ambapo walipatiwa namba maalumu za simu za kutoa taarifa za matukio hayo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Boniface Mbao amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa pwani ni wengi hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu .

Kwa upande wake,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani Herieth Koka, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunatoa rai kwa madereva wote kuzingatia kauli mbiu ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani isemayo”Maamuzi yako barabarani ni hatma yetu-Fikiri kwanza".

Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa usalama barabarani na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabani walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendeshwa vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.

Baadhi ya abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Pwani wamesema ni ya muhimu itasaidia kupunguza ajali nchini.”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi kikubwa”.Alisema Bi Khalfan mkazi wa Morogoro aliyekuwa safarini akitokea Dar es Salaam.