Monday, March 31, 2014

HEIFER INTERNATIONAL TANZANIA YAZINDUA MRADI MKUBWA WA KUENDELEZA SEKTA YA MAZIWA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mh Kaika Telele akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere Mwishoni mwa Wiki.
 Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini na wa kimataifa waliofika katika uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliodhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda, Mradi huo mkumbwa ulizinduliwa ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu wa East Africa Dairy Development (EADD), Mh Rakesh Kapoor akichangia mada kwenye uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza sekta ya Maziwa kwa Nchi za Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, jijini Dar Es Salaam. Mradi huo mkubwa kutoka Heifer International Tanzania umedhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda Foundation
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akifungua Pazia kuashiria Mradi huo wa Kuendeleza sekta ya maziwa umezinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo jijini Dar Es Salaam.
 Mjasiliamali wa Maziwa kutoka Mkoani Iringa, Bi Diana akitoa Ushuhuda wake kwa wageni waalikwa kuhusu mafanikio aliyoyapata akiwa kama mdau wa sekta ya maziwa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo ambae pia ni Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akimpongeza Mjasiliamali wa Waziwa kutoka Mkoani Iringa, Bi Diana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuendeleza Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na Wadau kutoka Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki wakifuatilia mada kwa makini wakati wa UZinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki
 Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Heifer International Tanzania na EADD pamoja na wadau wa Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya Kilolo mara baada ya kumalizika Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa Wiki.

WINDHOEK AMBAO NI WADHAMINI WAKUU WA SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 3 YA BONGO MOVIE WAFANYA KWELI KATIKA UKUMBI WA EAST 24 MWISHONI MWA WIKI

 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Mengele (Nyerere) akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa sherehe ya Kutimiza miaka 3 ya Klabu ya Bongo Movie, sherehe iliyofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Katika Jengo la Arcade Mikocheni, Mwishoni mwa Wiki
Warembo wakiwa wamebeba Chupa za Windhoek zinazosambazwa na kuuzwa na Kampuni ya Mabibo Beer ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa Sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya Klabu ya Bongo inayoongozwa na Steve Nyerere.
Mwenyekiti wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies, Bw Johnson Lukaza akipokea cheti cha kuthaminiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bongo Movie kama mmoja wa wamiliki wa kampuni ya usambazaji wa kazi za filamu nchini  iitwayo Proin Promotions Limited.
 Burudani pia zilikuwepo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila akiongea na waandishi wa habari wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa East 24 uliopo Mikocheni katika jengo la Arcade.
 First lady wa B Band inayoongozwa na Baba Zoro
 Wadau wakifuatilia burudani safi kutoka kwa wasanii mbalimbali waliopanda kwenye jukwaa
 Warembo wa Bongo Movie wakiingia ukumbi tayari kwa Kufurahia Miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie.
 Nuruel akiendelea kuimba kwa hisia katika sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki
 Mwenyekiti wa Bongo Movie akitoa maneno kwa wageni waalikwa pamoja na wasanii wa bongo movie na muziki nchini waliohudhuria sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa East 24.
 Keki ikikatwa kama ishara ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bongo Movie ikiwa imetimiza miaka 3
 Rich Rich akilishwa keki na Mwenyekiti
 Mwenyekiti wa Makampuni yaliyochini ya Proin Group of Companies, Bw Johnson Lukaza akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa sherehe ya kutimiza miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie.
 Bi Mwenda akifurahi kukabidhiwa cheti cha sifa ya kuwa msanii mkongwe
 Mtitu akipokea Cheti kutoka Kwa Mwenyekiti.
 Hawa ndio mabalozi wa Windhoek waliochaguliwa katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 3 ya bongo movie.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila ambae alikuwa mdhamini mkuu wa sherehe hiyo kupitia kampuni ya Mabibo Beer akitoa maneno mawili matatu mara baada ya mabalozi wa Bia ya Windhoek kuchaguliwa
 Amin Akishusha Burudani 
 Linex akiimba kwa hisia
 Shilole hakuwa nyuma na wimbo wake wa chuna buzi
Christa Bela akitoa vionjo safi kabisa katika sherehe hiyo.

Sunday, March 30, 2014

WANAFUNZI WA UDOM MWAKA WA MWISHO, WAAHIDI KUJIUNGA NA PPF

Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria semina hiyo Jumamosi Machi 29, 2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele.
Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, John Mwalisu, akitoa mada kwenye semina ya siku mbili, iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada.

WANAFUNZI wa mwaka wa mwisho wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wameridhishwa na mada mbalimbali zilizotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF, na wameahidi kujiunga kwa wingi na Mfuko huo, kwani wengi wao wanatarajia kujiajiri, hivyo itakuwa fursa nzuri kwao kuandaa maisha yao ya baadaye watakapostafu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti chuoni hapo jana mara baada ya semina iliyoandaliwa na PPF kwa wahitimu wa elimu ya juu, walisema awali walidhani kwamba Mfuko wa Pensheni wa PPF ni kwa ajili ya wafanyakazi walioajiriwa tu, lakini sasa wamefahamu kuwa milango iko wazi hata kwa wale ambao wamejiari ili mradi tu wawe na umri wa kuanzia 18.

Mmoja wa wanafunzi hao, Oneck Mwalongo, alisema kwa muda wote ambao amekuwa chuoni alikuwa  hajawahi kuona maofisa wa mifuko inayojihusisha na masuala ya hifadhi ya jamii wakifika kwa ajili ya kuwapa semina kuhusiana na fursa zinazotolewa, lakini PPF imekuwa ya kwanza kuwapa elimu hiyo.

"Lakini leo hii tunashukuru PPF wametufumbua macho kwani tulikuwa tunajua ili uwe mwanachama ni lazima uwe umeajiriwa, kwangu mimi nitajiunga na PPF kwa sababu kozi yangu ya sayansi ya kompyuta si lazima niajiriwe nitajiajiri mwenyewe," alisema Mwalongo.

Alisema mfumo wa uwekaji amana wa hiari ulioanzishwa na PPF utasaidia vijana wengi watakaokuwa wamejiajiri kujiwekea akiba.

Pia alisema amefurahishwa na mpango wa baadaye wa PPF wa kuanza kukopesha wanachama wake viwanja, kwani nyumba ndiyo jambo muhimu kwa maisha ya binadamu. 

Mwalongo, alisema wakati akiingia kwenye semina hiyo alikuwa hafahamu kama  maisha ya kesho huanza kuandaliwa leo, hivyo atakapoondoka chuoni hapo ataanza kujiwekea akiba ili asikumbane na msemo wa fainali uzeeni.

"Nilikuwa sifahamu kama maisha ya kesho yanaandaliwa leo wamenionesha njia sasa naanza kuandaa maisha ya uzeeni," alisema.

Kwa upande wake, Elizaberth Elibarick, alisema PPF ni mfuko wa kujiunga nao hasa kwa kuzingatia mfuko huo una mfumo wa uwekaji amana wa hiari na unatoa fao la elimu kwa watoto wa mwanachama anapofariki akiwa bado kazini.

Alisema si jambo la mchezo Mfuko kumsomesha mtoto au watoto wa wanachama ambao wamefariki kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita  na kizuri zaidi wanalipa mafao kwa wakati.

Naye Leonard Mgeja, alisema kupitia semina hiyo yeye na wanafunzi wenzake wameweza kufahamu vitu vya msingi ambavyo walikuwa hawafahamu kuhusiana na Mfuko wa PPF.

"Leo tumefahamu umuhimu wa maandalizi ya maisha ya baadaye tukiwa na umri mdogo ili kufanya mambo sahihi kabla ya kufikia uzeeni," alisema na kuongeza kwamba; 

"Hivi sasa ambapo tunakaribia kwenda makazini tunaenda na mwanzo mzuri kwani hatutegemei kuajiriwa tu, bali na kujiajiri hivyo tutajiunga na uchangiaji wa hiari kama hatutakuwa kwenye mfumo rasmi wa ajira."

Awali  Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko huo, Lulu Mengele, aliwaasa wanafunzi hao wa mwaka wa mwisho zaidi ya 500 waliohudhuria semina hiyo, kujiunga na PPF kupitia Mfumo wa asili wa Pensheni au ule wa uwekezaji amana pale ambapo wataamua kujiajiri wenyewe.

“Mfumo wa uwekezaji amana, unaandikisha watu kutoka sekta isiyo rasmi, kama wakulima, wafugaji, machinga na mama lishe”. Alifafanua.

Katika mada ya uwekezaji amana, Lulu alisisitiza umuhimu wa kuweka akiba kwani matayarisho ya maisha ya kesho yanaanza sasa.

Kwa upande wake Meneja wa Mfuko wa Pesnheni wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati,  inayojumuisha Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, John Mwalisu, alisema PPF imeandaa semina hiyo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho  wa chuo hicho kwa kuwa wao ndiyo wanaingia kwenye soko la ajira.

Alisema kutokana na wao kuwa na nguvu ya kuajiriwa au kujiajiri wameona ni vema kuwaelimisha namna nzuri ya kutunza akiba ili iwasaidie watakapokuwa fikia hatua ya kustaafu.

TASWIRA MBALI MBALI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI ZA CCM KATA YA MANDERA