Monday, September 30, 2013

SAGCOT CEO meets with the US journalists

Mr. Geoffrey Kirenga (center), CEO of the Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) gives a background about SAGCOT before answering questions from the United States journalists.   Also in the photo is Mr. Obey Assery-Nkya, Director from the Department of Coordination of Government Business in the Prime Minister's Office and Ms. Alexandra Frank (left), Project Manager (Tanzania) from the John Hopkins University.  The meeting was also attended by Mr. Frank Mhina (not in the photo), Foreign Service Officer from the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

Ms. Frank had coordinated a 15 member-journalists group which is funded by the Bill and Melinda Gates Foundation through John Hopkins International Reporting Project.  The journalists have been selected from a very competitive application process open to media organizations throughout the world.  The group is in the country from September 29, 2013 to October 9, 2013.  The chief mission of their trip is to learn more about Tanzania's agriculture, food security and nutrition initiatives. 
Mr. Kirenga continues his discussion with the US journalists.  Also in the photo are Mr. Assery-Nkya (right), Director of the Department of Coordination of Government Business in the Prime Minister's Office, Ms. Tulalumba Mloge (far right -3rd), Executive Assistant at SAGCOT Centre Ltd., and Mr. Frank Mhina (far right - 4th), Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 

During his discussion, Mr. Kirenga explained that SAGCOT is an inclusive, multi-stakeholder partnership to rapidly develop the region’s agricultural potential. SAGCOT was initiated at the World Economic Forum (WEF) Africa summit 2010 with the support of founding partners including farmers, agri-business, the Government of Tanzania and companies from across the private sector. 

SAGCOT’s objective is to foster inclusive, commercially successful agribusinesses that will benefit the region’s small-scale farmers, and in so doing, improve food security, reduce rural poverty and ensure environmental sustainability. The risk-sharing model of a public-private partnership (PPP) approach has been demonstrated to be successful in achieving these goals and SAGCOT marks the first PPP of such a scale in Tanzania’s agricultural history.
Mr. Assery-Nkya explains about scaling up nutrition and its coordinated mechanisms such as collaborative advocacy efforts between the civil society-led Partnership for Nutrition in Tanzania and the government are underway to raise awareness on the importance of nutrition and solicit action.  He further explained that the the country has established a High-Level Steering Committee for Nutrition, which is convened by the Prime Minister’s office and involves representatives from nine key ministries, development partners, UN agencies, civil society, faith-based organisations, academia and business. With the support and participation of this Committee as well as cross-sectoral technical expertise, the country finalized its National Nutrition Strategy and is now working to complete a corresponding costed implementation plan.
US journalists listening to the presentation.  Prior to their arrival in Tanzania, the group also had an opportunity to meet with H.E. Liberata Mulamula, Ambassador of the United Republic of Tanzania in the United States of America and Mexico. 

The meeting continues. 

The International Reporting Project (IRP) based at the Johns Hopkins University’s School of Advanced International Studies (SAIS) in Washington DC, has been conducting in-depth fact-finding visits to countries around the world since 2000.  More than 200 senior journalists have reported on these trips to South Africa, India, Turkey, Nigeria, Indonesia, Uganda, China, Liberia, Brazil, Kenya, Rwanda, Egypt, Lebanon, Syria, Saudi Arabia, Kazakhstan, Peru and Korea.

Mr. Kirenga listens to the presentation by the US journalists, who also plan to tour the the KINU Innovation Space in Dar es Salaam, the iAGRI Project at Sokoine University in Morogoro, the One Acre Fund in Iringa and the Oikos East Africa group in Arusha.
The purpose of the trip is two-fold: it is educational, part of the ongoing programs at the Johns Hopkins University School of Advanced International Studies, and it is also designed to enable the media representatives to report accurately about food security and agricultural topics.All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

MAALIM SEIF AWATAKA WAISLAM NCHINI KUUNGA NA KUSHIKAMANA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa wito kwa waislamu kuungana kutokana na mambo ya msingi yaliyomo katika dini hiyo na kuacha kutofautia kwa sababu ya madhehebu.

Amesema kuwa na madhehebu tofauti ni neema katika dini, hivyo hakuna sababu ya kugawanyika kutokana na tofauti ya madhehbu waliyonayo waislamu.

Maalim Seif ametoa nasaha hizo wakati akifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa iliyofanyika Mjini Sumbawanga, Mkoani Rukwa. Amesema ni jambo la kushangaza kuona waislamu wanakubaliana katika mambo ya msingi, lakini wanatofautiana na kulumbana kwa mambo madogo ambayo hayana athari ndani ya misingi na mihimili mikuu ya dini.

Amefahamisha kuwa iwapo waislamu wataungana na kuwa kitu kimoja, wataweza kuwashinda maadui wa Uislamu ambao siku zote wamekuwa wakishabikia migawanyiko ndani ya dini hiyo.

KWa upande mwengine amesema wakati waislamu wakijadili juu ya maadili ya dini yao, pia hawana budi kuhimizana katika kukabiliana na maadui wanaoathiri maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na janga la UKIMWI pamoja na matumizi ya dawa za kulevya. Amesema majanga hayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na kuporomoka kwa maadili, na kwamba wanaoathirika zaidi ni vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.

Ameongeza kuwa ni wajibu wa masheikh, walimu, wazazi na jamii kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kuelimishana juu ya majanga hayo, sambamba na kuachana na makatazo ya Mwenyezi Mungu yakiwemo pia vitendo vya zinaa.

Amesema, inaweza kueirejesha jamii katika maadili mema iwapo waislamu watakubali kufuata misingi thabiti na miongozo sahihi iliyomo katika uislamu.

Naye Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, amewahimiza waislamu waliohudhuria katika Ijtimai hiyo ya siku nne, kuitumia kivitendo elimu waliyoipata juu ya dini yao.

Amewahimiza waislamu hao kuwafikishia wengine elimu hiyo, ili nao waweze kuitekeleza dini ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa maamrisho yake na mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW).

Kwa upande wake, Amiri wa Jumuiya ya Fiysabilillahi Tabligh Markaz Mkoani Rukwa Sheikh Abdallah Abubakar amewashukuru wailamu pamoja na viongozi wa Mkoa huo, kwa mshikamano walioonyesha katika kufanikisha Ijtimai hiyo.

Mapema akisoma Risala ya Jumuiya hiyo Amir Ali amesema Jumuiya imepata mafanikio makubwa tangu kuasisiwa kwake na kupatiwa usajili mwaka 1992, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha waislamu katika kutekeleza maamrisho ya Munyezi Mungu na kuacha kabisa makatazo yake, iki kujijengea mustakbali mwema katika maisha ya akhera.

Viongozi mbali mbali wa dini na Serikali wameshiriki katika ufungaji wa Ijtimai hiyo akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe. Said Ali Mbarouk.

MKUTANO WA CCM CHWAKA UNGUJA

KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Unguja , ambapo alimwakilisha Ridhwan Kikwete .
VIONGOZI mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliohudhuria mkutano wa hadhara katika Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza mgeni Rasmi Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba (hayupo pichani) wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka.
WANACHAMA wapya 126 waliojiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo 61 walitoka chama cha CUF na 65 wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha uongozi wa fedha Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
MMOJA wa Wanachama 61 waliotoka Chama cha CUF Jimbo la Chwaka, Lailat Abdalla akielezea sababu za kutoka hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM) mbele ya Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka (CCM) Issa Haji Ussi (Gavu) akitoa salamu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya chuo cha uongozi wa fedha Chwaka, kulia mgeni rasmi katika mkutano huo, Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba.
KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba (kulia) akimkabidhi seti za jezi na mipira Katibu CCM Wadi ya Dunga, Maryam Kondo Mwadini kwa niaba ya timu za mpira wa miguu zilizopo katika wadi yake, makabidhiano hayo yalifanyika katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Chwaka Wilaya ya kati Unguja.(Picha na Haroub Hussein).

TIC yawahakikishia wawekezaji ushirikiano zaidi

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesisitiza kuwa kitaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanaotaka kuwekeza katika mikoa ya kanda ya kaskazini na maeneo mengine nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano la uwekezaji kanda ya kaskazini lililomalizika hivi karibuni mjini Tanga, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Bi. Juliet Kairuki alisema kuwa kituo chake kiko tayari kupokea wale wote walio tayari kuwekeza katika kanda hiyo. 

“Kwa wale ambao watakuwa tayari kuwekeza katika mikoa ya kanda ya kaskazini, milango ipo wazi kuandikisha miradi yao TIC,” alisema mjini Tanga hivi karibuni.

Akielezea kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika katika kanda hiyo alisema huo ni mwanzo wa juhudi kama hizo katika kutangaza vivutio vya uwekezaji katika kanda hiyo na maeneo mengine ya nchi.

Alitoa shukrani kwa mikoa ya kanda hiyo kwa kushirikiana katika kongamano hilo na kusema kuwa hiyo ni njia nzuri na yenye matokeo makubwa na mazuri kwa uchumi wao na wa nchi kwa ujumla.

Alisema kongamano hilo limetoa fursa nzuri kwa wawekezaji, wafanyabiashara na wajasiriamali kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizo katika mikoa ya kanda ya kaskazini na pia kuelezea ambavyo serikali inasaidia uanzishwaji wa miradi ya uwekezaji.

Alisema katika kipindi cha miaka 12 iliyopita, Tanzania imefanya vizuri katika eneo la uwekezaji ambapo uwekezaji mkubwa umefanywa kwenye sekta za kilimo, utalii, viwanda, mawasiliano, miundombinu na usafirishaji.

Alisema katika kipindi hicho, miradi ya uwekezaji imekuwa kutoka 178 hadi 869 mwaka 2012 huku uwekezaji uliofanywa na watanzania wenyewe ukiwa ni asilimia 53 ya miradi yote.

Alifafanua kuwa kuongezeka kwa miradi kumechangia kukua kwa mitaji kutoka dola za kimarekani 874 milioni hadi USD 12 bilioni. “Miradi hii imevutia ajira mpya zinazofikia 135,760 mwaka 2012,” alisema.

Mkuu wa wilaya ya Hanan’g, mkoa wa Manyara, Bi. Christina Mndeme alisema kongamano hilo limekuwa la manufaa makubwa kwa wilaya yake.

Alisema kutokana na kongamano hilo, tayari amefikia makubaliano na baadhi ya wawekezaji ambao wako tayari katika kujenga kiwanda cha kuongeza thamani mazao mbalimbali pamoja na mwekezaji mwingine, Manyara Cement, anayetaka kujenga kiwanda cha sementi.

“Makongamano kama haya ni muhimu sana, tuko tayari kufanya kazi na wawekezaji na TIC,” alisema.

Awali, akielezea umuhimu wa makongamano hayo ya uwekezaji, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema ni ya muhimu na kuwa yanatakiwa kuimarishwa zaidi.

Akitoa mfano alisema tayari matokeo mazuri yameshaonekana kutokana na kongamano la uwekezaji lililofanyika mwezi Oktoba mwaka 2012 katika kanda ya Nyanda ya Juu Kusini mkoani katavi.

“Sasa kuna ongezeko kubwa la vyumba vya hoteli vinavyofikia elfu moja kutokana na uwekezaji katika sekta ya utalii katika mkoa wa Katavi,” alisema.

Kongamano la uwekezaji kanda ya kaskazini lilihudhuriwa na wawekezaji zaidi ya 1,500 toka ndani na nje ya nchi pamoja na maafisa wengine toka sekta binafsi na umma, viongozi wa dini, mabalozi na wadau wengine wa maendeleo.

AZANIA BANK YACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE YA SEKONDARI NARUMU

Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi Hajira Mmambe akipeana mkono na mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Narumu,Deodatus Nyoni mara baada ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Bweni.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi Hajira Mmambe akipeana mkono na mkuu wa shule ya sekondari Narumu,Sister Joyce Mboya mara baada ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Bweni.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi Hajira Mmambe katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne waliohitimu katika shule ya sekondari Narumu iliyopo wilayani Hai.
Mkuu wa shule ya sekondari Narumu Sister Joyce Mboya akizungumza wkati wa mahafali ya 25 ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Narumu sekondari wakiingia kwa madaha uwanjani kutoa burudani ya nyimbo kwa wageni.
Dada mkuu anayemaliza muda wake katika shule ya sekondari Narumu Anna Geluas akisoma risala mbele ya mgeni rasimi(hayupo pichani)aliyemshikia kipaza sauti ni mhitimu mwenzake Happiness Mkama.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Narumu Deodatus Nyoni akizungumza wakati wa mahafali ya 25 ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 25 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Narumu Hajara Mmambe akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mgeni mwalikwa katika mahafali ya 25 ya shule ya sekondari Narumu Ibrahimu Shayo(Ibra Line) akizungumza jambo wakati wa mahafali hayo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule Deodatus Nyoni akimkabidhi zawadi mgeni rasmi katika mahafali hayo Hajira Mmambe kwa niaba ya Bodi .
Mgeni rasmi katoka mahafali hayo ambaye pia ni meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akikata keki katika sherehe hiyo.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi Hajira Mmambe katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne waliohitimu katika shule ya sekondari Narumu iliyopo wilayani Hai.

2013 Young Achievers Awards Nomination Open!


The Young Achievers Awards is an annual event where Young successful Ugandans are recognized and awarded for their excellence and initiative in the areas of business, science and technology, agriculture and outstanding talent and leadership among other sectors.  We’ve just extended the application deadline until 30th October , 2013 @ 8:00pm East Africa Time to allow more time for interested candidates to apply. To learn more, visit our website www.youngachievers.ug or see below. The deadline will not be extended again, so click here to apply now as soon as possible!

What are the categories?
  • Young Achievers Award for Leadership and Social Enterprise;This category recognizes individuals, organizations or group of young people with innovative solutions to society’s most pressing social challenges.  It includes consideration for profit and not for profit social enterprise ventures, youth leaders/Activists in the social and political realm
  • Young Achievers Award for Farming and Agro-Processing; Agriculture being the backbone of Uganda’s economy, this category recognizes and rewards outstanding individuals who are engaged in agricultural production and processing (Agro industry) creating as a livelihood for themselves and others and eventually feeding the nation.
  • Young Achievers Award for Scientific Innovation ;This category recognizes outstanding achievement in areas of information communication, technology and other scientific and engineering innovative activities facilitating positive change in society. These may include technology software solutions and others ranging from private PC sales, right through to development of corporate, mechanics, robotic inventions and creations, education software solutions, and communications networks.
  • Young Achievers Award for Business Entrepreneurship;This category recognizes outstanding individuals who are leading entrepreneurs of their generation. He or she may be involved in general business of merchandise and retail business, Export and Distribution networks, service sector, Media  & Advertising, Event management, and others but been able to succeed against all odds and proven to be exceptional among the rest.
  • Young   Achievers Awards Outstanding Performing Arts;This category recognizes outstanding talent of young people with exceptional achievement in areas of acting, music, and stand-up comedy, dancing, and any other performing arts.
  • Young Achievers Awards Outstanding Sports Personality; This category recognizes outstanding sports talented of young people with exceptional achievement in sports and been able to represent the country internationally with pride and brought glory to the nation. May be a team or individual.
  • Young Achiever –Media and Journalism:This category includes young journalists in print and electronic media who cover the news stories and shape the outlook to society through media. It is aimed at encouraging, promoting and recognizing excellence in African journalism as well as reinforcing the importance of the journalists’ role in Uganda’s development. E.g. Print, radio, TV, bloggers, reporters and media entrepreneurs.

Who becomes Young Achiever? 
We are looking for 7 outstanding youth below the age of 35 years from Uganda with incredibly inspiring stories, who are committed to developing innovative and creative solutions to ending poverty and who have been running a social impact project for more than one year on a full-time/part-time basis. Nominees can be working in any sector (non-profit, for-profit, government), on any issue, and can be either entrepreneurs or intrapreneurs.

 How can I get involved?
If you think you have what it takes to become a Young Achiever, nominate now ! But if you know someone else who might be interested, please encourage them to apply by forwarding them this email or nominate them yourself. And if you’d like to learn more, please visit our website, or reply directly to this email.

Young Achievers Awards
Team!

Sunday, September 29, 2013

HARAMBEE KUCHANGIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KUSINI UNGUJA YAFANA

Baadhi ya Wananchi na wanachama Chama cha Mapinduzi walioalikwa katika hafla ya Harambee ya kukichangia Chama Mkoa wa Kusini Unguja iliyofanyika  katika Hoteli ya Karafuu,Michamvi Wialaya ya Kat
 Viongozi wa Chama na Wananchi mbali mbali walioalikwa katika Uchangiaji wa Fedha kwa CCM Mkoa wa Kusini Unguja,wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika  katika Hoteli ya Karafuu,Michamvi Wilaya ya Kati
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza Daramsi,akiimba wimbo usemao “Mpewa hapokonyeki” wakati kikundi cha Culture Musicul Club kilipocharaza ala zake katika hafla ya Harambee ya kuchangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja huko Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akimkabidhi Fedha Tasilim Shilingi za Kitanzania Milioni Moja katibu wa Kikundi cha Culture Muzical Club Said Mwinychande,wakati wa hafla ya Harambee ya kuchangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja huko Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akimkabidhi Cheti maalum Kamanda wa UVCCM (M) Misungwi,John Buyamba, akiwa ni miongoni mwa Wanachama na Viongozi waliokichangia chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja katika hafla ya Harambee iliyofanyika  Michamvi Karafuu Hotel Wilaya ya Kati
Mbunge wa Jimbo la Muyuni  Mahadhi Juma,(kulia)akionesha Cheti alichokabidhiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(katikati)kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe,kwa mchango wake alioutoa kwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini katika hafla ya Harambee iliyofanyika Karafuu Hotel Michamvi,Wilaya ya Kati (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM

Zanzibar,akimakabidhi Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Mkoa wa Kusini Unguja Jafar Sanya,cheti kwa kukichangia chama cha Mapinduzi katika hafla iliyofanyika huko Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akipokea fedha tasilim shingi za Kitanzania Milioni Moja kutoka kwa Mohamed Naushad,wakati wa Hafla ya kukichangia Chama cha mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja,huko katika Hoteli ya Karafuu Michamvi Wilaya ya Kati
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni  Salmin Awadh,alipokuwa akitoa kauli ya kuchangia Shilingi Milioni Moja wakati wa Hafla ya kukichangia Chama cha mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja,huko katika Hoteli ya Karafuu Michamvi Wilaya ya Kati
Kamanda wa UVCCM (M) Misungwi John Buyamba,akionesha picha baada ya kuinuua kwa Shilingi Milioni Moja fedha za Kitanzania katika hafla ya kuchangia Chama cha Mpainduzi Mkoa wa Kusini Unguja,iliyofannyika jana Karafuu Hotel Michamvi Wilaya ya Kati,(kulia) Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai Mwiny
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya Harambee ya kukichangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja,huko Karafuu Hotel Michamvi Wi laya ya Kati Katika hotuba yake aliwashukuru Viongozi na wananchi kwa kuonesha moyo wao wa kujitolea katika chama
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(katikati) akimkabidhi Cheti maalum Mwakilishi wa  Jimbo la Uzini Mohamed Raza Daramsi,  akiwa ni miongoni mwa Wanachama na Viongozi waliokichangia chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja katika hafla ya Harambee iliyofanyika Michamvi Karafuu Hotel Wilaya ya Kati,(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Kati Mhe. Vuai Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Culture musical Club, baada ya kumalizika kwa hafla ya Harambee ya kuchangia Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja huko Karafii Hotel Michamvi Wialaya ya Kati.
Picha zote na Ramadhani Othman, Ikulu, Zanzibar.

GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHINGTON, DC YAFANA


Wageni wakiwa kwenye foleni ya kupata chai ya Tanzania na vitafunio kama vile Vitumbua, maandazi na kadhalika na wengine wakijionea nguo na vitabu vya kiswahili.
 Wageni wakiendeea kujionea, kula na kusikiliza vivutio vingine vilivyopo Tanzania kwa Walimu wa darasa la kiswahili DMV wakijaribu kuwaelezea uzuri wa Tanzania na vivutio vyake.
 Walimu wa darasa la kiswahili wakiwaelezea wageni waliotembelea banda la Tanzania upikaji wa vitafunio walivyoleta.
 Mmoja ya mgeni aliyetokea Virginia akipata chai na kitumbua huku akisifia utamu wake.
 Walimu wa darasa la kiswahili katika picha ya pamoja.
 Watoto wa darasa la kiswahili wakiimba baadhi ya nyimbo za Tanzania
 Mgeni akipata maelekezo ya vitabu vya kiswahili huku akiwa na kibakuli cha maandazi.
 Banda la Tanzania katika picha ya pamoja.
 Mzee Safari (kulia) akimuelezea moja na mgeni kuhusu kitabu chake cha "Nyayo za Obama" alichatunga kwa Kiswahili