Tuesday, November 27, 2012

Serikali yasisitiza kushirikiana na wadau kuendeleza kilimo


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara mara ya kuongoza mkutano maalum wa Mpango wa kukuza kilimo kusini mwa Tanzania (SAGCOT), akizungumzia umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya kilimo, kulia ni Waziri wan chi Ofisi ya waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu na Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Bw. Christopher Chiza.



Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi na wadau wengine ili kufikia mapinduzi ya kilimo hapa nchini na hivyo kupatikana usalama wa chakula na maendeleo.

Msimamo huo umetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano mkubwa wa kilimo unaofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Mkutano huo wa siku mbili umetayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Kituo cha mpango maalum wa uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Mkutano huo unalenga kuvutia wawekezaji katika maeneo ya kilimo, biashara na miradi ya maendeleo kijamii na kiuchumi katika eneo la SAGCOT.

“Ushirikiano uliopo kati ya serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo, wakulima na wadau wengine wa kilimo umesaidia kuendeleza sekta hii hapa nchini,” alisema.

Waziri Mkuu aliyashukuru makampuni 20 ambayo tayari yameshatoa ahadi ya kuwekeza katika sekta ya kilimo Tanzania katika miaka ijayo na wakati huo huo akaitaka sekta binafsi kufanya uamuzi zaidi wa kuwekeza zaidi katika sekta hiyo.

Hata hivyo alisisitiza kwamba wawekezaji wote katika ukanda wa SAGCOT watapewa kipaumbele pale ambapo uwekezaji wao unalenga pia kushirikisha wakulima wadogowadogo..

“Ni muhimu kusisitiza kwamba tunahitaji zaidi uwekezaji ambao utajali kushirikiana na wakulima wadogo na wajasiriamali wadogo na wa kati,” alisema.

Alisisitiza kwamba hata mapendekezo ya sera za uwekezaji katika kilimo zitoe kipaumbele kueleza jinsi wakulima wadogo na watanzania wa kawaida watakavyofaidika na uwekezaji katika ukanda wa SAGCOT.
Waziri Mkuu aliwahakikishia wawekezaji kwamba kupitia sheria mbalimbali Tanzania inatoa vivutio vingi na vizuri kulinganisha na nchi nyingine za Afrika.

“Kuwekeza Tanzania pia kunawahakikishia soko la uhakika katika eneo hili la Afrika,” alisema.
Alisema Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohakikisha usalama wa wawekezaji.

Akitoa mada katika mkutano huo, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza alitaja baadhi ya maeneo yanayolengwa katika uwekezaji SAGCOT kama kilimo cha miwa, matunda, ufugaji, nafaka na mazao ya misitu.

Katika siku ya pili ya mkutano huo wawekezaji watapata fursa ya kutembelea maeneo maalum ya miradi pamoja na kuangalia miradi ya kuimarisha miundombinu katika ukanda huo wa SAGCOT.

SAGCOT ni mpango unaoshirikisha sekta binafsi na ya umma unaotegemewa kuleta mapinduzi makubwa katika usalama wa chakula nchini kwa kushirikisha pia wakulima wadogo wadogo katika mazingira endelevu.

WADAU WAJITOKEZA KUCHANGIA HARAMBEE YA UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI ILIYORATIBIWA NA TEA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka (kulia) akiongozana na mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro ambapo katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 278 zilipatikana.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dk. Naomi Katunzi akizungumza katika harambee hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.
Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro akipokea mchango wa shilingi milioni tatu kutoka kwa  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa ukiwa ni mchangop wake kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Inocent Mungi akikabidhi mchango wa shilingi milioni tano kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Vupe Ligate akipeana mkono na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Matifa, Dk. Asha Rose Migiro baada ya kuchangia katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike ambapo jumla ya shilingi milioni 278 zilipatikana katika harambee hiyo.
Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Rex Energy, Francis Kibisa kwa mchango alioutoa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike
Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro (katikati) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni tano kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya KCB Tanzania, Christiane Manyeye (kulia) na mwakilishi wa ubalozi wa Kenya, Boniface Makao wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari akikabidhi mchango wa dola za kimarekani 1,000 kwa  Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiromgeni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya  ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mstaafu Dk. Asha Rose Migiro (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani, Mkuu wa Kitengo cha mahusiano wa Shirika la Nyumba (NHC), Susan Omari baada ya shiriki hilo kuchangia mabati 1,000 yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la THT wakitumbuiza katika harambee hiyo.
Mkurugenzi wa Radio One, Deogratius Rweyunga akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam 
Mmiliki wa Blog ya 820,  Shamim Mwasha, akitoa mchango wa shilingi laki 6.5 alizokusanya kutoka kwa wasomaji wa mtandao wake.
Baadhi ya wadau waliojitokeza katika harambee hiyo

MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI, KENYA

 Mwanasheria wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo. Kushoto ni bwana Wilbert Kawa Katikati ni bwana Dr. Richard Sezibera na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano Uganda. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Kenyetta  jijini Nairobi
 Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samweli Sitta pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyemba (wa pili kulia) , Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika (kushoto)  na Mhe Ole Nangoro Naibu Waziri Kilimo na Mifugo (kulia) wakifuatilia kwa makini jambo katika Mkutano wa Baraza la Mwawaziri wa Jumuiya  Jijini Nairobi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda (kulia) akifuatilia kwa makini  mkutano unaoendelea Nairobi katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUWAKAMATA MASHABIKI KATIKA KIOTA CHA THAI VILLAGE MASAKI-JIJINI DAR.

Vijana wa SKYLIGHT BAND wakiongozwa na Sam katika kuhakikisha mashabiki wa SKYLIGHT BAND wanapata flava za ukweli zikiwemo Kwaito, Ragga, Reggae, Dance Hall, Nigerian Flava, Sebene na zingine kibao. Kushoto ni Joniko Flower na kulia ni SONY MASAMBA. Wanapiga show ya kufa mtu kila Ijumaa katika ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam.
Mary Lukas sambamba na Joniko Flower wakitoa burudani.
SONY MASAMBA akishusha mistari.
Msanii wa SKYLIGHT BAND Aneth Kushaba AK 47 akionyesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki.
Aneth Kushaba AK 47 akiwapa raha mashabiki wake (hawapo pichani).
CEO wa Ndege Insurance Dkt. Sebastian Ndege sambamba na mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakiserebuka.
Warembo wakisakata rhumba kwa raha zao.
Pichani Juu na Chini ni Umati wa mashabiki waliojitokeza katika Kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam kushangweka na SKYLIGHT BAND mwishoni wa wiki, ni Kila Ijumaa wako hapo.
Namba ya Mashabiki ikizidi kuongezeka kama inavyoonekana pichani, palikuwa hapatoshi. Usikose Ijumaa hii.
Couples waliong'ara siku hiyo ni hawa hapa.
Blogger King Kif (kushoto), Mdau John Mwansasu na wadau wengi wakipozi kwa picha.
Mashabiki wapya All the way from Nairobi wakipata ukodaki na Msanii wa SKYLIGHT BAND Aneth Kushaba AK47.
Watasha nao ndani nyumba chezea SKYLIGHT BAND wewe......!!!
Bongo Movie Star Steve Nyerere, Mboni Masimba a.k.a Kim Kardashian wa Bongo na Mdau John Mwansasu wakipata Ukodaki.
Mdau akipozi na warembo.
Warembo katika pozi ndani ya SKYLIGHT BAND.
Adrian Hillary Stepp, Blogger Cathbert Angelo wa Kajunason Blog na Blogger King Kif.
The Don Shaban Mazua (kushoto) akila ukodaki na wadau.

sharobaro

Mh Naibu Balozi wetu wa Uingereza na Irene wameremeta

 Maharusi wakivalishana pete baada ya kula viapo
 Dendazzzzz......
 Maharusi wakikabidhiwa cheti cha kumeremeta
  Maharusi wakifungua mziki kwenye mnuso wa kumeremeta kwo
 Maharusi na wanafamilia
 Maharusi katika picha ya pamoja na familia. Kutoka Kulia ni Mama wa Bwana harusi Kilumanga, Maharusi, Mama Irene na Dada wa bwana Harusi Mariam Kilumanga
Mashaaallah...
Mh Chabaka akimlisha mai waifu wake  Irene keki

Monday, November 26, 2012

WILDAF yaendesha Mkutano kwa Wadau wake wa Kupiga Vita Ukatili Dhidi ya wanawake nchini

Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Washiriki wa Maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya Mabango yenye Ujumbe wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya Wawanake.
Maandanamo yakipokelewa na Muwakilishi wa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora Msechu (wa tatu kulia),Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema (pili kulia) pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Charles Kenyera.
Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan akikata utepe uliokuwepo kwenye basi aina ya Toyota Coster,ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Safari ya Wadau wa Wildaf wanaokwenda Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali katika mikoa ya kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya Wanawake.
Wadau wa Wildaf wakipanda kwenye Basi hilo tayari kwa Safari ya Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali katika mikoa ya Kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya Wanawake.
Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Ukaribisho katika Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.
Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula (pili kupia) akitoa neno la Ukaribisho katika Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.Wengine Pichani toka kulia ni,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora Msechu,Mkugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Judith Odunga pamoja na Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan.
Muongozaji wa Mkutano huo,alikuwa ni Bw. Deus Kibamba
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini,DCP Rashid Omar akiwasilisha mada ya aina mpya ya Karatasi maalum itolewayo na Polisi iwapo mtu anapatwa na tatizo la Majeraha (PF 3) iliyofanyiwa Marekebisho na kuongezewa baadhi ya Vipengele Muhimu,wakati wa Mkutano uliofanyika leo wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya Wanawake,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akisoma Hotaba yake mbele ya Mamia ya Wadau wa Wildaf waliohudhulia Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akikata Utepe wa Kuashiria Uzinduzi rasmi wa aina mpya ya PF 3 mara baada ya kutoa Hotuba yake huku akisaidiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa Makini.
Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kipolisi ya Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema akiteta jambo na Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Mrisho Mpoti na Mjomba Band wakitoa Burudani wakati wa Mkutano huo.