Na Bashir Yakub.
Wapo Watanzania ambao
ndoto zao ni kumiliki shule. Ninapoongelea shule simaanishi lazima yawe yale mashule makubwa. Hata shule za
awali ambazo zinaanzishwa na wajasiriamali wadogo mitaani nazo ni shule
kwa maana hii katika makala haya.
Nyaraka kuu
inayoongoza taratibu za usajili wa shule
binafsi huitwa fomu namba RS8. Huu ndio mwongozo mkuu wa usajili. Kuna mambo ya
msingi na ya kisheria ambayo mtu hutakiwa
kujiandaa nayo iwapo anataka kuanzisha
shule binafsi.Mambo haya huwa yanakamilishwa kwa wepesi na bila usumbufu ikiwa yanapitia kwa wanasheria lakini pia mtu
anaweza kufanya mwenyewe isipokuwa hata akifanya mwenyewe kuna document za lazima ambazo lazima zisainiwe na
kuthibitishwa na mwanasheria.
1.
USHAURI MUHIMU KWA WALIO/WANAOTAKA KUANZISHA SHULE.
Kwanza kabisa kabla ya
lolote ni muhimu kujua shule yako itamilikiwa
namna ipi kisheria.
Utaimiliki binafsi wewe kama wewe,
utaunda kampuni halafu kampuni ndo imiliki shule, au utaweka chini ya
taasisi fulani. Kila kimoja katika haya
kina faida zake halikadhalika hasara
zake. Pamoja na hayo faida na hasara hizo zinazidiana viwango. Katika baadhi ya makala zilizopita niliwahi kuzungumza umuhimu na faida za
kitaalam za kufanya biashara chini ya
kampuni.Kwa ushauri wangu wa kitaalam
hasa katika masuala ya makampuni nashauri kuwa ni vema sana ukianzisha mradi wa shule fungua na kampuni
ili shule iwe chini ya kampuni. Zipo faida nyingi sana utazipata
kupitia kufanya hivyo. Hata wenye mtaji mdogo hasa ndugu zangu
wanaoanzisha nursery mitaani fungua kampuni na nursery yako iweke chini ya
kampuni halafu utaona matokeo yake baada
ya muda.Kufungua kampuni ni bei ndogo sana
na rahisi mno hivyo si jambo la kumuogofya mtu.
2.
MAOMBI YA USAJILI
WA SHULE HUPELEKWA WAPI.
Maombi ya usajili wa huelekezwa kwa kamishna mkuu wa Elimu. Ofisi ya kamishna mkuu wa elimu
Tanzania iko Dar es Salaam. Hata hivyo
nakala ya maombi hayo hupelekwa kwa mkaguzi mkuu wa elimu wa kanda
husika. Kanda husika ni kanda ambayo itaanzishwa
shule husika. Mkaguzi wa kanda ndiye
hujushughulikia karibia mambo yote ya msingi kuhusu usajili wa shule.
3.
MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA KUJIANDAA
NAYO.
Kila biashara huwa ina maandalizi yake kabla
ya kuanza kwake. Shule binafsi nayo kama biashara nyingine yoyote inayo mambo
ya msingi na ya kisheria ambayo mtu anatakiwa kuyazingatia kabla ya kuanzisha biashara hii.Mambo haya pia ndiyo hayohayo
utayotakiwa kuyajaza kwenye fomu maalum
ya kuombea usajili wa shule yako.
( a ) Jina
la shule. Lazima kwanza ujue shule yako itaitwaje.Huwezi kufanya mipango ya
shule bila jina. Pia jina hutakiwa
kujazwa kwenye fomu maalum ya kuombea usajili.
( b ) Lazima
ujue unataka kuanzisha shule ya aina gani. Shule ziko aina nyingi, unataka
shule ya awali(nursery),shule ya
msingi,sekondari ya form iv au v & vi. Pia ujue iwapo shule hiyo itakuwa
kutwa au ya kulala, ya wasichana na wavulana au wavulana tu au wasichana tu.
Kama shule yako ni sekondari lazima ujue itakuwa inashughulika na michepuo
ipi sanaa, biashara,kilimo, sayansi,
elimu ya ufundi au kitu gani.Haya lazima ujiandae nayo na uyajue.Pia taarifa hizi huwa zinahitajika unapokuwa unajaza fomu ya usajili hivyo ni muhmu kuziandaa.
( c ) Jambo
jingine ni tarehe au kipindi ambacho shule inatarajiwa kufunguliwa. Taarifa hii
hutakiwa kwasababu mamlaka za usajili zinajenga dhana(assume) kuwa mtu anapoamua
kujaza fomu ya usajili basi huwa yuko tayari
kuanzisha shule na hivyo lazima awe na tarehe
ambayo shule yake itaanza.Hivyo lazima uandae tarehe kama una mpango huu.
( d ) Pia
huwezi kuanzisha shule bila kuwa na Meneja
wa Shule. Sheria inataka kabla ya usajili lazima awepo meneja na atajwe katika
fomu ya usajili.
( e ) Anuani kamili ya mahali ambapo shule inakusudiwa kufunguliwa ni jambo jingine linalopaswa kufafanuliwa kupitia fomu hii. Anuani hapa si tu P.O BOX……… hapana. Unataja mtaa,kitongoji,kata,wilaya, na mkoa. Hii ndio anuani.
( e ) Anuani kamili ya mahali ambapo shule inakusudiwa kufunguliwa ni jambo jingine linalopaswa kufafanuliwa kupitia fomu hii. Anuani hapa si tu P.O BOX……… hapana. Unataja mtaa,kitongoji,kata,wilaya, na mkoa. Hii ndio anuani.
( f ) Pia
uandae hati ya Umiliki wa Ardhi au Mkataba wa Pango wa eneo ambalo shule
itafunguliwa.
( g )
Utatakiwa kuonyesha sifa na idadi ya walimu watakaoajiriwa, uwiano wa walimu na
wanafunzi kwa maana ya wastani wa mwalimu mmoja kufundisha wanafunzi wangapi
(Teacher-Students ratio)
( h ) Utatakiwa
kueleza vifaa vitakavyokuwa shuleni na pia kuonyesha kiwango cha juu zaidi
(maximum) cha wanafunzi wanaoweza kusoma kwa wakati mmoja katika shule
itakayofunguliwa.
( I ) Kutaja
kiwango cha ada unachokusudia kuwatoza wanafunzi wa shule hiyo, huku ukipambanua
pia tozo nyinginezo kama vile gharama za bweni na aina ya vifaa ambavyo
wanafunzi wenyewe wanapaswa kuja navyo shuleni.
4.
VIAMBATANISHO MUHIMU.
Vimbatanisho muhimu vya
kuandaa ni Hati za Idhini za matumizi ya Ardhi chini ya taratibu za mipango miji
kutoka mamlaka husika hasa manispaa, Mhandisi wa Wilaya au Mji, serikali za
vijiji, na kadhalika.
Cheti kutoka kwa bwana afya
kuthibitisha kwamba eneo litakalotumika kwa ya ajili ya shule linakidhi vigezo vya afya na usalama wa
wanafunzi, pia ambatanisha taarifa za wafanyakazi wasio walimu,na nakala ya
ramani ya majengo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
16 comments:
asante kwa msaada wako
Umtusaidia, ila ungtuambia sifa anazotaliwa kuwa nazo meneja wa shule
Good
Ahsante sana ila narusiwa mwenyewe kua manager wa shule hiyo?
Thanks
Naota sana iyo ndoto ila maskin sina hata milio 1. Sjui km ntaweza kumiliki angalau nasar ya watoto.
Asante kwa maelezo na elim nzuri, mungu akubariki
Good
Big up.
Big up.
Good
Uko vizuri kaka
Ada ya kufungulia je?
Asante kwa ushauri mzuri
I like it
Post a Comment