WAZIRI
wa Madini Angela Kairuki amesema ili kufikia malengo ya mpango wa taifa
wa maendeleo ambao unaelekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe
imefikia uchumi wa kati, sekta ya madini inalazimika kuongeza mchango
katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10
mwaka 2025.
Ametoa
kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya
madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini
China.
"Ili
kufikia malengo ya mpango wa taifa wa maendeleo ambao unaelekeza kuwa
ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe imefikia uchumi wa kati, sekta ya madini
inalazimika kuongeza mchango katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8
ya sasa kufikia asilimia 10 mwaka 2025," amefafania Waziri Kairuki.
Wakati
Waziri Kairuki anazungumza washiriki wa Kongamono la siku moja la
uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China walikuwa
wakisikiliza kwa makini fursa zilizopo nchini Tanzania.
Pia
mada mmbalimbali zilizowasilishwa katika kongamo hilo ambalo limelenga
kuhamasisha ubia katika sekta ya madini ikiwemo kuvutia mitaji zaidi,
teknolojia mpya kwenye utafiti, uchimbaji na uchakataji wa madini ili
kuyaongezea thamani.
Akifungua
Kongamano hilo la kwanza la aina yake kuandaliwa na Wizara ya madini
kwa ushirikiano na kituo cha uwekezaji Tanzania na ubalozi wa Tanzania
nchini China, Waziri wa Madini Angela Kairuki, ametumia jukwa hilo
kuelezea mipango ya wizara yake katika kukuza sekta ya madini nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania(TIC)
Geofrey Mwambe amesema nia ya Serikali katika maboresho ya sera na
sheria ni kuhakikisha kuwa rasilimali za Tanzania zinawanufaisha
watanzania pamoja wawekezaji.
Ametumia
nafasi hiyo kufafanua fursa mbalimbali zilizopo nchini Tanzania na
kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa kwa
kuzingatia mazingira ya uwekezaji ni mazuri na nchi yetu ni salama.
Akikaribisha
washiriki wa kongamano hilo Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa
Kairuki amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kutumia fursa za
uwekezaji wakati wa mkutano wa FOCAC uliofanyika Beijing mwezi Septemba
mwaka huu
Wakati
huo huo kwa upande wao wawekezaji kutoka China ambao wamewekeza
Tanzania na wawekezaji watanzania wameeleza kufurahishwa na mabadiliko
yanayofanywa na Serikali katika sekta ya madini lakini zaidi kuhusu
kongamano hilo ambalo wamesema ni la faida.
Kwa
kukumbusha tu miongoni kwa mada zilizowasilishwa ni pamoja na fursa na
mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini nchini pamoja na
marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017 na utafiti wa madini
nchini Wadau wengine walihudhuria kongamano hilo ni kutoka STAMICO na
Tume ya Madini nchini.
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki akizungumza mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi
wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na
China lililofanyika jijini Beijing nchini China hivi karibuni.
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu ufunguzi
wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na
China lililofanyika jijini Beijing nchini China hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment