Thursday, June 25, 2015

wasafiri wapata kizaazaa baada ya basi lao kuharinika likiwa njiani kutoka Tabora kwenda Dar es salaam leo

Gari la Shabiby Line lenye namba za usajili T 607 CVL likiwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara baada ya kuharibika

Leo hii asubuhi nikitokea Singida kwenda Dar kwa basi la Shabiby Line, lenye nambari za usajili T607 CVL iliondoka stendi ya Misuna Singida mnaomo saa 12.48(moja kasoro 12) za asubuhi. 
Safari ilikuwa nzuri mpaka gari ilipofika nje kidogo ya Manyoni kuelekea Dodoma mnamo saa 2.30 kwa muda wa sekunde chache mpaka dkk moja hivi ulisikika mlio usio wa kawaida ingawa dereva wa gari hilo aliendelea na safari huku nikijiuliza mlio huo ulikuwa wa kitu gani ghafla ukasikika mlio mkubwa sana kiasi cha kupelekea taharuki ndogo miongoni mwa abiria, hapo ndipo dereva akaanza kupunguza mwendo na hatimaye kusimama. 
Dereva na wahudumu wawili wa gari hilo wakateremka kwenda fuatilia kilichotokea. Lakini hawakurudi garini mpaka abiria wakaanza kuteremka toka garini ili kujua kulikoni. 
Nikiwa miongoni mwa abiria walioteremka hapo nje ya gari hatukukuta mtu yeyote baadaye dereva na wahudumu wakaonekana kama mita 500 kutoka ilipo gari wakiwa wamesimama. 
Baada ya kulikagua gari uvunguni ikaonesha kipande cha propela shaft kinakosekana. Hivyo tukaelewa kuwa hilo ndilo lililotokea, lakini mimi na abiria wenzangu tuliendelea kusimama pale nje ya gari kwa muda upatao nusu saa hivi bila dereva na wenziwake kurudi ilipo gari kuondoa sintofahamu hiyo. 
Waliendelea kubaki kule mpaka baadhi ya abiria walipoamua kuwafuata walipo. Ndipo wakatoa maelezo kuwa propela shafti ilichomoka na wameshawasiliana na ofisi zao za Dodoma na kuwa gari imetumwa kuja tufaulisha. 
Baada ya kukaa mpaka saa 5.30 bila gari kutokea toka Dodoma kutufaulisha, kitu kilichoanza kuleta jazba kwa abiria ambao walimweka kiti moto dereva ambaye alipata wakati mgumu sana kujibu maswali ya abiria wengi wakimshutumu kwa uzembe wa kutosikia mlio usio wa kawaida katika gari muda mfupi kabla ya kuharibika. 
Kabla ya dereva kuwekwa kiti moto baadhi ya abiria walijaribu kupiga simu katika moja ya namba iliyosemekana ni ya meneja wa kampuni hiyo ya Shabiby Line lakini hawakupata majibu ya kuridhisha kitu kilichopelekea jazba miongoni mwa abiria.
Hali iliendelea kuwa ya sintofahamu mpaka saa  6 mchana dereva wa gari hiyo alipokuja na kusema kuwa hakuna gari toka Dar itakayofika pale porini ila kuna Hiace na Coaster zimekodiwa kutusogeza Dodoma ambako tumea ahidiwa gari itatuchukua kuendelea na safari ya Dare es Salaam, ambako badala ya kufika saa 9 mchana sasa tutafika Dar saa 3 usiku. 
Kibaya zaidi kuna watu ambao mwisho wa safari zao si Dar tu bali pamoja na Zanzibar, Bagamoyo na kwingineko ambao sasa hawatoweza kwenda leo. 
Adha hiyo pia imenikuta mimi mwandishi wa habari hii ambaye kwenda kwangu Dar es Salaam ni kuipokea familia yangu inayowasili leo toka nchini Uingereza ambao sijaonana nao tangu mwaka 2010, kwa bahati mbaya kwangu nilimwahdi mwanangu mdogo Ndisha kuwa ningekuwepo Airport kuwapokea hili sasa halitowezekana kwani ndege iawasili Dar saa 3 usiku muda ambao unatarajiwa basi tutakalopanda lifike Ubungo.
Maoni ya abiria wengi wameilaumu kampuni hiyo kubwa ya usafiri wa abiria kwa kutokuwa na mipango mizuri hasa katika mawasiliano na abiria hasa gari linapoharibika. 
Leo iliwachukua staff wa gari hilo nusu saa kuwaeleza abiria tatizo liliotokea na mipango ya kujikwamua toka porini kukiwa hakuna huduma yeyote na gari likiwa na abiria watoto na mchanga mmoja. 
Ni juu ya utawala wa Kampuni ya Shabiby kuelimisha wafanaykazi wake kuwa na lugha za ki staarabu kwa wateja wao.

Baadhi ya abiria wakiwa wamelala juu ya mawe bila shaka kwa njaa.
Dereva wa gari hilo katikati akiwa kajiegesha katika jiwe 
Baadhi ya familia zenye watoto katika msafara huo uliokwama Sukamahela
Tumekwama! abiria wakijadiliana la kufanya!
Hapa ndipo kipande cha nyuma cha proprla shafti kilipochomoka
Ubovu kama huu inaelekea si wa siku moja, bila shaka gari hii haijafanyiwa uangalizi kwa kipindi kirefu jambo ambalo ni hatari kwa abiria na waliomo garini.
Tukifaulishwa.

Ndani ya Hiace

Basi la Shabiby likwa tupu baada ya abiria kufaulishwa baada ya masaa mengi ya sintofahamu
Picha na habari na Mkala Fundikira wa TBN Kanda ya Magharibi akiwa  Dodoma

No comments:

Post a Comment