Thursday, June 25, 2015

MAKAMPUNI 1500 YA NDANI NA 400 TOKA NJE YA NCHI KUSHIRIKI MAONESHO YA SABA SABA MWAKA HUU

 Gari likiwa limebeba takataka katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
  Mabanda ya maonyesho ya sabasaba yakiendelea kufanyiwa kukarabati kwaajili ya maonyesho yatakayoanza Juni 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Wazee wa kilimo kwanza wakiwa katika maandalizi ya maonyesho ya sabasaba.
 Wanawake nao katika harakati za kuweka mazingira ya kupendeza katika mabanda ya maonyesho ya sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
 Mafundi wakitoa mizigo kwaajili maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Mwonekano wa nje katika viwanja vya sabasaba ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja hivyo.

HABARI NA PICHA NA EMMANUEL 
MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

ZIKIWA  zimebaki siku 4 kufuguliwa kwa maonyesho ya Saba Saba hapa nchini, Makampuni 1500 toka ndani ya nchi na  mengine 400 toka nje ya nchi yanatarajiwa kushiriki maonyesho  hayo.

Akizungumza na Globu ya jamii leo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko ya Nje  wa Tan Trade, Mrs  Anna Florence Bulondo amesema katika maonyesho hayo, Banda la maonyesho  la Wizara ya Elimu litakuwepo katika maonyesho hayo kwa mara ya kwanza.

Pia amesema nchi 25 toka sehemu mbalimbali  duniani  zinatarajiwa kushiriki maonyesho hayo.

Aidha amevitaja viingilio katika maonyesho hayo kuwa ni shilingi 3000 kwa watu wa wazima  hiyo ikiwa Julai  1-6 huku akieleza kuwa siku ya kilele Julai 7 kiingilio kitakuwa shilingi 4000 kwa watu wazima na watoto wakiingia katika maonyesho hayo kwa shilingi 1000  mpaka mwisho wa maonyesho.

No comments:

Post a Comment